Je, bado Zanzibar mmechoka Mgombea Urais kuchaguliwa Dodoma? Na kupokezana Urais wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika Je?

Jul 30, 2013
96
36
1593157455609.png

Bendera ya Tanganyika

Kabla ya Uchaguzi wa Mwaka 2015, CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, kilieleza nia yake ya kutaka kuachiwa mamlaka ya kumchagua mgombea Urais wa Visiwa hivyo, badala ya utaratibu wa sasa unaoshirikisha wenzao wa Tanzania Bara.

Pamoja na hatua hiyo, chama hicho pia kilifikiria kurejea mtindo wa kupokezana kiti cha urais wa Tanzania kati ya bara na visiwani kama ilivyokuwa awali, ili kuweka usawa katika Muungano.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa huenda ikazua mpasuko na malumbano mapya kuhusu suala la urais ndani ya CCM.

1593157987648.png

Vuai Ali Vuai
Akizungumza katika mahojiano maalumu visiwani humo, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) 2013, Vuai Ali Vuai, alisema kuwa suala hilo linajadiliwa na kwamba ana matumaini kuwa litapatiwa ufumbuzi.

“Ndani ya CCM tuna utaratibu wetu wa kupata viongozi, lakini hilo suala la kuchaguliwa mgombea urais kutoka kwenye vikao vya Dodoma hata sisi limetugusa… Kwa sasa tuko kwenye mchakato wa kulijadili ili tupate ufumbuzi,” alisema Vuai na kuongeza:

“Siyo tu kuchaguliwa mgombea urais, hata suala la kupokezana urais na jinsi ya kupata viongozi wengine kama wabunge na wawakilishi tunalijadili kwa kina. Ninaamini tutapata ufumbuzi… Siwezi kusema lini kwa kuwa chama chetu ni kikubwa mno, lakini tunalijadili.”

Vuai alitoa kauli hiyo, huku kukiwa na malalamiko ya Wazanzibari wengi kuhusu Muungano, ambapo wengine wanahoji iwapo kuna haja ya kuendelea na utaratibu wa sasa kupata mgombea na Rais wa Zanzibar ambao ni lazima upate baraka za CCM Bara.

1593157540653.png

Bendera ya Tanganyika

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema jambo hilo halijafikishwa kwenye vikao rasmi vya chama.

“Kama wao wanalifikiria hilo, acha waendelee, labda ungewauliza kama wameshalifikisha kwetu. Ukiniuliza mimi nitakujibu kuhusu utaratibu tulionao sasa, ila kama wao wana hoja nyingine, basi watazileta kwenye vikao husika zitajadiliwa,” alisema Nape.

Swali langu ni;

Je, Zanzibar mumeufyata au Msimamo bado upo Palepale?

Nawatakia Uchaguzi mwema.
 
Asante kwa swali hili, nami huko nyuma niliwahi kulizungumza
Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Mustakabali wa 'Urais' wa JMT?

Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano, 2015 Si Zamu ya Zanzibar?

Na kwa huu utaratibu wa CCM kujitokeza kwa wingi kwenye urais kila baada ya miaka 10, hakuna possibility kabisa kukatokea Mzanzibari akawazidi wa Bara kwa sifa za kuchagulika urais wa JMT, hivyo kama tuna dhamira ya dhati kuonyeshea urais wa JMT ni haki kwa wote, ili rais aweze kutoka Zanzibar, ni lazima hili kifanyike.

Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

P
 
kimantiki ni makosa mzanzibari kuongoza nchi nzima yani hata mkoa mmoja wa bara haujai eti yakhe aje kuongoza serikali ya muungano ataweza wapi? rais wa muungano sharti atoke bara! baba mwenye mtoto mmoja hawezi kumudu kulea watoto kumi!

pia rais wa zenj lazima akubalike bara au ili bara kujihakikishia usalama wa nchi na muungano sasa ni lazima rais atoke bara au awe amefanya kazi bara!

hiyo ndio njia sahihi kulinda usalama wa nchi na watu wake mengine ya muungano ruksa wajadili ili si hili la urais ni very sensitive!! watulie tuli machogo tuwachagulie chuma kama Magu ila chonde chonde NEC rais asiwe mtoto wa rais wa zamani hii si nchi ya kurithishana urais kimila hii ni Republic! tuiheshimu!
 
Huu ni ubaguzi, Kila Mtanzania ana haki ya kuwa rais wa JMT. Wanzanzibari wote japo kwanza ni Wanzanzibari ndipo wanakuwa Watanzania lakini kwa Utanzania wao, wana haki zote za uraia wa Mtanzania ikiwemo kugombea urais wa JMT bila kubaguliwa.

Basi kama hii nchi ni moja kweli isiyo na ubaguzi ,basi mtu wa bara aruhusiwe kuwa Rais wa Zanzibar , sio ubaguzi kwetu iwe halali halafu inapokuja kwao iwe tofauti, na Mtu wa bara aruhusiwe kumiliki ardhi Zanzibar, la sivyo huu muungano wa kinafiki ufe. Kama Zanzibar inatambuliwa basi na Tanganyika pia itambuliwe, kuwe na exclusive rights za Watanganyika kama walivyonazo Wazanzibari

.Either tuwe Federation inayotambuwa uwepo wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar au tuwe Union inayotambua nchi moja tu ya Tanzania, huu mwingine ni ujinga
 
good thought!
 
Back
Top Bottom