Je, bado kuna umuhimu wa kuhamisha makao makuu ya nchi Dodoma?

huu ni ujinga, Rais aache kufanya mambo ya muhimu kwanza ya kutatua kero za wananchi aanze kuhangaika na ujinga wa kuhamia Dodoma.
 
Huo ni upuuzi....serikali inatakiwa ipunguze matumizi kipindi hichi ambacho haina pesa we unataka waanze kujitia magharama yakuhama
 
Labda mleta mada tunaomba uainishe faida za kuhamia Dodoma ni zipi kwa mwananchi wa kawaida ili tuone kama kuna umuhimu wa serekali kuhamia Dodoma.
 
Ni kweli.......wengi tumelifikilia hili lakini tukaliona kuwa tija yake kwa sasa ni sawa na ile ya kuanza kushughurikia jambo la katiba mpya .........hebu tumpe muda kwanza ajipange.
 
wewe ndio mjinga. labda una maslahi na dar kama walivyo viongzi wengi. hivi unajua gharama za kwenda dodoma kila wakati? na ni nchi gani mji wa kibiashara ndio makao ya serikali na mji mkuu umebaki kama eneo la kutafuna fedha za masurufu. dodoma ni nyonya damu kwa walipa kodi wa tanzania
 
Labda mleta mada tunaomba uainishe faida za kuhamia Dodoma ni zipi kwa mwananchi wa kawaida ili tuone kama kuna umuhimu wa serekali kuhamia Dodoma.

  1. Dodoma ni katikati ya nchi - ni rahisi kutoa huduma kote.
  2. Dar kunamsongamano na haipo kwenye mpangilio mzuri wa miundo mbinu- hasa upande wa usafiri, maji na huduma zingine muhimu kwa jamii.
  3. Dodoma hali ya hewa ina mazingira mazuri ya kufanya kazi.
  4. Dodoma kuna ofisi majengo yanayoweza kumaliziwa au kukaliwa na wizara mbalimbali.
  5. Dodoma ni chaguo la MUNGU
  6. Dar imesha furika na imekabwa sana - karibu idadi kubwa ya watu wanaendelea kuzaliwa na kukimbilia Dar.
Mhe. Rais John Joseph Pombe Magufuli tunaomba busara zako za kuhamia Dodoma. Dodoma sio mbali na Mwanza, Arusha, Mbeya, Zanzibar, Tandaimba, Rukwa hata Rwanda, Malawi, Kenya, Kongo, Uganda.... Network inaikubali Dodoma.
 
Heko, asante kwa kumuelewesha.
 
Nafikiri kama ni kuhama, ni kuhamisha wizara moja baada ya nyingine na si kuhamisha wizara zote kwa wakati mmoja. Na hili linawezekana kabisa.
 
Kama kuna kitu ambacho Magufuli hawezi na hatakaa aweze ni kuhamia Dodoma, ataweza vyote lakini kuhamia Dodoma hataweza milele.
 
Huo ni upuuzi....serikali inatakiwa ipunguze matumizi kipindi hichi ambacho haina pesa we unataka waanze kujitia magharama yakuhama

Uwezo wa akili wanaukawa ni huo wanadhani kuhamisha serika sawa na mtu wa chumba kimoja
 
huu ni ujinga, Rais aache kufanya mambo ya muhimu kwanza ya kutatua kero za wananchi aanze kuhangaika na ujinga wa kuhamia Dodoma.

Yaani Nyerere alikuwa mjinga kupanga mipango ya kuhamia Dodoma? Acha hizo kuhamia Dodoma si ujinga kwanza itapunguza foleni jijini Dsm na watu watachapa kazi , kero hazitakwisha hata Kama Serikali haikuhamia Dodoma, kumbuka. Malawi, Nigeria walikuja kujifunza Dodoma pale CDA jinsi ya kuhamia miji mipya wao wamehamia tayari lakini Tanganyika ambaye alikuwa Mwalimu wao mpaka Leo bado anaishi kwa visingizio tu.
 
Back
Top Bottom