Je, bado kuna umuhimu wa kuhamisha makao makuu ya nchi Dodoma?

Hili kwa Serikali hii ya CCM haliwezekani Mkuu,huo ulikuwa ni mpango tu ambao utekelezaji wake ni kama ndoto vile.........binafsi nishasikia ahadi nyingi sana kutoka Serikalini na hazijatekelezwa so sishangai na hili lisipotekelezwa,ndio staili ya utendaji kazi wa viongozi wetu.
 
tumechoshwa na maneno ya kanga ambayo yamesemwa sana tangu enzi za mwalimu..kama kweli kuna mpango wa kuhamia DOM nilitarajia majengo ya taasisi mbalimbali yangekuwa yanajengwa Dodoma na siyo Dar..kila nchi ina mji mkuu na mji wa kibiashara...ni wakati sasa dar ibaki kuwa mji wa kibiashara na Dodoma iwe mji mkuu kwa dhati..

Umeambiwa dodom hamna serikali?? Sijui unaelewa nini ukisikia serikali
 
Hiyo sawa nakuuliza ufipa makao makuu itajengwa lini lazima tu utapata jibu
 
Kuna tetesi ya kuwa hata Makao ya Serikali za Mitaa yataamia Dar. Ramani za Dunia zinaonyesha makao makuu ya CCM na Bunge ni Dodoma. Ukweli hata CCM hawapo Dodoma, na wabunge karibu wote wana maofisi na familia zao Dar. Majengo, ofisi na watendaji wote wapo Dar. Hata ofisi ya kina Jaji Warioba ya Katiba ni Dar.

Hata Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hana mpango wa kuboresha Dodoma, CDA ilianzishwa miaka ya 70 hadi leo wanajiita wana mamlaka ya kujega makao makuu huku hata mamlaka hawana, zaidi yamamlaka walionayo wa kutojenga makao makuu.

Dodoma ni mahali pazuri kuwa Mji Mkuu, lakini kama kawaida ya wa TZ maneno huwa hayaumbi.et

Mh. Raisi Kikwete alijaribu kwa kuanzisha UDOM, ninampongeza kwa hilo. Viongozi wengi wa juu hapa Dodoma ni hawafai kabisa, hata wagogo wenyewe kama aliyekuwa Waziri Mkuu Malecela ndio amehamisha hata kiwanda cha Magodoro Dodoma.
 
Na kwa sasa mji wa dodoma umejaa kwelikweli hakuna tena hiyo nafasi ya kuamia pale.
Ukiangalia majengo ya wizara halmashahuri na mkuu wa mkoa yapojengwa na ukifikilia Miundo mbinu ya barabara na vitu vingine, hakika dar ipo vizuri kuliko Dodoma.

Unless waende porini huko wakajenge upya mji mwingine na kupima upya lakini sio Dodoma mjini.


NOTE:
Uchimbajiwa Uranium Manyoni na Bahi ambapo Machimbo yatakuwa ni ndani ya 50Km ambazo kitaalamu hakutakiwi kuwa na Makazi ya watu hili ni Jangaa kuu na ndio kifo cha Dodoma na miji ya pembezoni ukiwemo Bahi na Manyoni.

Kitaalamu hutakiwi kuishi 50KM karibu na Mgodi wa Uranium maana disaster ikitokea Mtakufa wote, Upepo mkali ukivuma Residual zote zitatua Mjini.
 
Wahamie Dododma jangwani! waache kula raha Dar labda Nyerere akifufuka tunaweza kushudia Serikali ikihamia Dodoma, maana yeye ndiye alikuwa mwenye hayo mawazo.

tumechoshwa na maneno ya kanga ambayo yamesemwa sana tangu enzi za mwalimu..kama kweli kuna mpango wa kuhamia DOM nilitarajia majengo ya taasisi mbalimbali yangekuwa yanajengwa Dodoma na siyo Dar..kila nchi ina mji mkuu na mji wa kibiashara...ni wakati sasa dar ibaki kuwa mji wa kibiashara na Dodoma iwe mji mkuu kwa dhati..
 
Wahamie Dododma jangwani! waache kula raha Dar labda Nyerere akifufuka tunaweza kushudia Serikali ikihamia Dodoma, maana yeye ndiye alikuwa mwenye hayo mawazo.[/QUOTE
Angalia uongo uliosambazwa duniani. Soma hizi links tatu:
  1. Dodoma - Wikipedia, the free encyclopedia
  2. Dodoma, Tanzania - The new capital city of Tanzania
  3. Map of Major Cities of Tanzania, Tanzania Cities Map
Links zote zinaonyesha Makao Makuu ya Tanzania ni Dodoma.

Je hii ni fact or ni udaku tu. Labda wangebadili na kuwe wakweli.
 
Hayo yamebaki maandiko tu we jiulize kwanini Wizara karibia zote ziko Dar na bado wanazidi kujenga majengo na Idara na wakala wa wizara hapo Dar kwanini wasingejenga Dodoma? Chezea Dar weye Dodoma hakuna Bahari, Hakuna sehemu za kujirusha, hakuna Makampuni na wafanyabiashara wakubwa wakuwajaza watu bahasha kijana.

Wahamie Dododma jangwani! waache kula raha Dar labda Nyerere akifufuka tunaweza kushudia Serikali ikihamia Dodoma, maana yeye ndiye alikuwa mwenye hayo mawazo.[/QUOTE
Angalia uongo uliosambazwa duniani. Soma hizi links tatu:
  1. Dodoma - Wikipedia, the free encyclopedia
  2. Dodoma, Tanzania - The new capital city of Tanzania
  3. Map of Major Cities of Tanzania, Tanzania Cities Map
Links zote zinaonyesha Makao Makuu ya Tanzania ni Dodoma.

Je hii ni fact or ni udaku tu. Labda wangebadili na kuwe wakweli.
 
2326874_dodoma_967a0.jpg


Serikali imeshauriiwa kuendeleza mchakato wa kuhamisha ofisi zote zake mkoani Dodoma kwenye makao makuu ya nchi yetu ili kuweza kupunguza msongamano wa watu na magari.Hayo yalisemwa na Mtanzania Mzalendo, John Lyasenga wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam.

Kutokana na jiji la Dar es Salaam kuwa na msongamano wa watu na foleni za magari, kuna umuhimu kwa Serikali kufikiria suala hili la kuhamishia ofisi zake na huduma zingine muhimu kwa mji huo mkuu wa Tanzania kwa ni kwa kufanya hivyo kutaleta fursa kwa wakazi wa mji huo,"alisema Lyasenga.


Aidha aliongeza kuwa faida za kuhamia Dodoma ni pamoja na kuwepo kwa fursa mbalimbali kama vile ajira ,kuongeza pato la mkoa kupitia ujenzi wa viwanda vitakavyoongeza uzalishaji na kupunguza maafa kwa jiji la Dar es Salaam kama vile mafuriko kutokana na wingi wa watu.
Mkoa wa Dodoma ina ukubwa wa eneo 41,000 kilomita za mraba na idadi ya watu ni 2,083,588 kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.

Aliongeza kuwa, hali ya hewa ya mkoa huo ni nzuri,ukilinganisha na mkoa wa Dar es salaam wenye kilomita za mraba 1,397 huku hali ya hewa, ikiwa ni joto wastani na idadi ya watu ikizidi kuongezeka hadi kufikia milioni 4,364,541 sawa na asilimia 4.3 kwa mwaka kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.

Chanzo kutoka Mjengwa blog
 
Hili wazo ni la siku nyingi sana but hakuna anayejali.

Mimi pia nakualiana nalo kwa asilimia nyingi, msongamano unaozidi Dar ni kutokana na makao makuu ya serikali kuwepo hapo na shughuli nyingi za serikali kujazana hapo jambo ambalo Nyerere alishaliona toka wakati ule. Pengine shughuli za serikali zinazidisha uzururaji wa wengi jijini Dar.
 
Mkapa asingeweza kutokana na jina lake halikumruhusu kuhama (mkaa hapa)
 
Suala la kuhamishia wizara/serikali kwa ujumla kwenda DODOMA limekuwepo toka 1970 lakini mpaka leo ni SIASA tu (TAMISEMI pekee ndio waliohamia huko) je inahitajika nini cha ziada kuhamia huko. Nionavyo zinatumika pesa nyingi kuhudumia safari za watumishi & viongozi kati ya DAR ES SALAAM & DODOMA. Hakuna mgombea yeyote aliyeliona hili wajameni? Nigeria waliweza kuhamia Abuja (kutoka Lagos), South Afrika kuhamia Pretoria iweje sisi tushindwe?
 
Tunakuomba Rais Magufuli uhamishe serikali yako ihamie rasmi Dodoma toka Dar.

Katika kipindi hiki cha kupunguza matumizi katika Serikali yako, tunakuomba uhamishe wizara zote kutoka Dar ziende Dodoma ambapo ndio makao makuu yetu ya Nchi yalipo.

Naamini hili litawezekana hasa wakati huu ambapo umeanza na kasi ya 4g. Hakika hapa ni kazi tu.
 
Back
Top Bottom