Je, atatokea mwenye kuumiza zaidi Watanzania kuliko mwendazake?

Kama system yao wanakiri haina mfumo mzuri wa kufanya vetting, wanawekana kwa mapenzi yao na kujuana, naona kuna dalili zote uwepo wa makundi chamani kwao ukaja kuleta mtafaruku mwingine ambao ili kuuzima utasababishwa ateuliwe mtu wa haraka wasiemjua alipotoka matokeo yake tutajikuta tunarudi kule kule.

Kama tukizungumzia ubaya, upo ubaya wa aina nyingi, sio lazima uwe uuaji na utakaji pekee, hata kurithishana vyeo kama tunaishi kwenye nchi ya kifalme nao ni ubaya ambao unajenga hisia za utengano, kwamba wapo special wanaotakiwa kula keki ya taifa peke yao, hili nalo linatakiwa kupigiwa kelele za kutosha, wasomi wamejaa kila kona nchi yetu watumiwe.
 
Tukusanyike mkapa basi tuulizwe walioumizwa wakae upande wao na ambao hawajaumizwa wakae huku tuone. Kisha walioumizwa waseme kwa nini waliumizwa kama wana guts hizo.
 
Kupinga maovu ndani ya nchi ni wajibu wa raia wote wenye kujitambua bila ya kujali aliyefanyiwa maovu anakuhusu au LA na si wajibu waliotendewa maovu peke yao.
~~~~~~~~~~~~~~~~

Gambo: Ulikuwa uporaji shughuli ya kufunga maduka ya kubadilisha fedha za kigeni​

Tuesday June 15 2021​

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amesema shughuli ya kufunga maduka ya kubadilishia fedha za kigeni iliyofanyika nchini takribani miwili iliyopita, ilikuwa ni uporaji wa kuumiza watu.



By Habel Chidawali
More by this Author

IN SUMMARY​

  • Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amesema shughuli ya kufunga maduka ya kubadilishia fedha za kigeni iliyofanyika nchini takribani miwili iliyopita, ilikuwa ni uporaji wa kuumiza watu.


Advertisement
Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amesema shughuli ya kufunga maduka ya kubadilishia fedha za kigeni iliyofanyika nchini takribani miwili iliyopita, ilikuwa ni uporaji wa kuumiza watu.
Akizungumza jana Jumatatu Juni 14, 2021 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa bajeti kuu ya Serikali, Gambo amedai mchakato huo ulikuwa kama nia ya baadhi ya watumishi wa Serikali kutaka wafanye wao biashara hiyo.
Novemba 20, 2018 maduka zaidi ya 20 yalifungwa jijini Arusha baada ya ukaguzi uliofanywa na maofisa wa Serikali wakishirikiana na vyombo vingine vya dola.
Aprili, 2021 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga alisema kati ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni 87 yaliyofanyiwa ukaguzi jijini Dar es Salaam, 82 yalikutwa na viashiria vya utakatishaji wa fedha.
Katika maelezo yake, Gambo ambaye amewahi kuwa mkuu wa Mkoa Arusha amedai Serikali ilikuwa ikipandisha viwango vya mitaji kwa lengo la kutaka wafanyabiashara washindwe lakini walipoendelea kufanya biashara zao waliona hakuna namna zaidi ya kuvamia.
"Mlichukua fedha zao, magari, viwanja vyao na mali nyingine watu wakabaki hawana kitu hivi lengo la Serikali ilikuwa nini," amesema Gambo.
Gambo amezungumzia pia sekta ya Utalii akisema imeachwa kabisa bila kuwekewa mkakati katika bajeti jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wa nchi.
Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imeshindwa kubuni mbinu ya kuvutia ili kuongeza watalii badala yake imefikiria kuongeza tozo inayoweza kusababisha watalii kupungua nchini.
"Hii bajeti imeacha kabisa kutaja sekta ya utalii, wenzetu wanafikiria kuvutia watalii sisi tunawaza kuongeza tozo, mnawaza nini nyie," amehoji Gambo.
Ametolea mfano wa kupungua kwa watalii kwamba kumesababisha baadhi ya wawekezaji kupunguza gharama kwenye mahoteli yao kutoka Dola 200 za Marekani hadi Dola 100.

Tukusanyike mkapa basi tuulizwe walioumizwa wakae upande wao na ambao hawajaumizwa wakae huku tuone. Kisha walioumizwa waseme kwa nini waliumizwa kama wana guts hizo.
 
Kizazi hiki kitapita,atakuja mwingine miaka 30 ijayo but Mungu atoruhusu atamzima kama alivyomzima sokoine na jiwe.Mungu apendi watz waonewe ongoza vyema uishi miaka mingi kama JK na Mwinyi.Usipambane na watu huwezi washinda Pambana na maendeleo na sio watu.
Ukiwa mtawala huwezi ukawashinda freemason, wachawi, matajiri, mabeberu,wakuu wa dunia,wasomi,nk.Njia pekee ya kuwashinda watu ni kutenda haki.
Ukitimiza watu ni lzm watakumaliza tu.
 
Mwigulu,kigwangala, bashiru, bashite hawa ni madikteta.
Watz msiwape watu uongozi waliopitia makuzi ya shida wataumiza watz.
Thus wenzetu uangalia historia ya asili ya mtu awaokotezi viongozi Ili mradi tu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kiukweli hakuna Rais bora kama Magufuli, kwa aliyoyafanya ndani ya nchi hii kwa muda mfupi yaliwafurahisha na kutugusa wananchi wengi sana

Enzi za Jakaya Serikali yake ilikuwa ikisumbuliwa na skendo za ufisadi kama escrow, Richmond, Epa, Dowans, pesa/chenji ya radar, etc, ujambazi wa kuteka magari kuiba benki kuvamia vituo vya polisi, ugaidi kibiti, watumishi hewa na vyeti feki, udumavu sekta ya Afya, ufisadi uliotamalaki kila sekta kuanzia wizarani mpaka kwenye Govt agencies kama Nssf, nhc, pssf, nida, tanesco etc na mengine mengi mengi
Na haya madhaifu ya Jakaya ndio ulikuwa mtaji mkuu wa Chadema na wapinzani wengine

Sasa mlitaka MAGUFULI aliyoingia madarakani afanye nini,,,,!????

Na siku zote huwezi kupendwa na kila mtu hata uwe Mungu, ukitenda haki basi waovu watakuchukia, Ukiziba mianya ya wizi na ufisadi basi wale mafisadi watakutangazia ubaya kila kona,
Magufuli alipendwa na walio wengi na ndio maana wananchi wengi sana walimlilia ktk msiba wake

Ama kwa hakika ndani ya muda mfupi tumeona kazi iliyotukuka ya uongozi wa awamu ya Tano

Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani JPM
 
Kiukweli hakuna Rais bora kama Magufuli, kwa aliyoyafanya ndani ya nchi hii kwa muda mfupi yaliwafurahisha na kutugusa wananchi wengi sana

Na siku zote huwezi kupendwa na kila mtu hata uwe Mungu, ukitenda haki basi waovu watakuchukia, Ukiziba mianya ya wizi na ufisadi basi wale mafisadi watakutangazia ubaya kila kona,
Magufuli alipendwa na walio wengi na ndio maana wananchi wengi sana walimlilia ktk msiba wake

Ama kwa hakika ndani ya muda mfupi tumeona kazi iliyotukuka ya uongozi wa awamu ya Tano

Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani JPM
Kupora hela za watu ndio kunakufurahisha ?
 
Hata Nyerere aliumiza Sana watu wengi
Na akaitwa Mtukufu...
Walioshi enzi za Nyerere wanashangaa sana..
Nchi haina Tv
Kuna radio moja Tu ya serikali
Magazeti mawili Tu moja la serikali
Lingine la chama..
Kauli yake ni sheria...
Akikosea yeye analaumiwa Kawawa..
Watu wakanyang'anywa mashamba na ardhi..
 
Kupora hela za watu ndio kunakufurahisha ?

Kuboresha sekta ya Afya kwa ujenzi lukuki wa vituo bora vya afya nchi nzima, kukomesha wizi na ufisadi, kukomesha ujambazi na hata ule ugaidi wa KIBITI, kuweka usimamizi mzuri ktk sekta ya madini,,, WEWE HAUKUFURAHISHI..!???
 
Hata Nyerere aliumiza Sana watu wengi
Na akaitwa Mtukufu...
Walioshi enzi za Nyerere wanashangaa sana..
Nchi haina Tv
Kuna radio moja Tu ya serikali
Magazeti mawili Tu moja la serikali
Lingine la chama..
Kauli yake ni sheria...
Akikosea yeye analaumiwa Kawawa..
Watu wakanyang'anywa mashamba na ardhi..
Hao wananchi wenyewe walikuwa na uwezo wa kuzisikiliza? Nguo za kuvaa tu walikuwa hawana.

Nyerere aliongoza ktk maIngira magumu sana huku asilimia 80% ya watanzania wote wakiwa hawajui kusoma wala kuandika.
 
Back
Top Bottom