Je, atajiuzulu au atasubiri kura Wabunge ya kutokuwa na imani naye?

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
612
1,045
Tupo katika kipindi kingine cha mapambano yasionekana kwa macho, baada ya muhimili wa Bunge kutikisika kwa kauli ya aliyekuwa spika wa bunge sasa ni zamu ya Msimamizi wa shughuli za serikali.

Mwezi ujao vikao vya 9 katika bunge vinakwenda kuanza wakati wowote kuanzia hivi leo bunge linaweza kuja na agenda ya kutokuwa na imani nae.

Mjadala ulioibuka hivi karibuni wa suala la mfanyabiashara maarufu nchini Salome Mgaya Maarufu kama Mama Bonge unaweza kuset ajenda ya standard ya kile kitakachokwenda kujadiliwa Bungeni.

Katika hali isiyotarajiwa na wengi kinachokwenda kujadiliwa katika mkutano wa 9 utakaoanza November moja ya ajenda moto ni juu ya suala la kiongozi wa Serikali kushiriki kukwepa kodi.

Kuanzia tarehe 17 Oktoba hadi 30 Oktoba kamati za kudumu 4 za bunge zitaanza kukutana.

Familia yamtumia mwanaharakati Martin Maranja Masesa kupitia katika mitandao ya kijamii imevuja sauti ya moja ya wanafamilia mtoto wa msimamizi wa shughuli za serikali (PM) kuwa Martin MM alitumwa kuweka mambo sawa katika mitandao katika sakata hilo la ukwepaji kodi kuwa mzigo uliokamatwa wajitahidi mzee asitajwe.

Samia na chama kimejaribiwa;

Miongoni mwa vyama vikongwe vinavyotolewa mfano katika Afrika na dunia juu ya uimara wake, ukongwe wake na namna ya kinavyoweza kuhimili fukuto zake za ndani kikajisahihisha na kusonga mbele ni CCM. Kimeendelea kuwa ni mfano na hivi karibuni kinaweza kuingia katika rekodi ya kidunia kwa kuwa Chama kikongwe zaidi kubaki madarakani. Chama iko sasa kiko katika mtihani, kimejaribiwa.

- CCM inatajwa kuwa ni chama kinachosimamia misingi yake na chenye kujisahihisha kila pale kinapogundua kuwa kilifanya makosa yenye kukigharimu. Ndiyo maana katika sakata hili TRA wamekuwa wazi juu ya kukamatwa kwa mfanyabiashara Salome Mgaya.

Samia alifanya makosa, kosa kubwa lilikuwa ni kitendo cha kuruhusu kuishi na NYOKA ndani ya nyumba kama mtendaji Mkuu wa serikali akiamini kuwa “zimwi likujualo halikuli likakwisha” …ni kosa vitoto vya Nyoka kuanza kumea upya ndani Serikali.

Endapo ataamua kujiuzulu mapema kabla ya tarehe 1 November, Rais anayo mamlaka ya kuchagua na kupendekeza jina moja kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge wote..
 
Endapo ataamua kujiuzulu mapema kabla ya tarehe 1 November, Mwenyekiti na kamati kuu inayo mamlaka ya kuwajadili na kupendekeza majina matatu na lipatikane jina moja kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge wote..
 
Hakuna mtu wa kujiudhuru kwa miccm hii. Pia usitegemee hili bunge dhaifu sana lilopitishwa tu bila idhini ya wananchi kumpigia kura mhimili mkuu kuwa hawana imani nae.

Tatu bado sana kwa Tanzania hii kumpigia kura kiongozi yoyote iwe kuanzia spika, waziri mkuu mpaka kiongozi bado sana. Mabaya yapo mengi sana kuanzia kwa mawaziri hasa miguru na makatani,lakini wote wanalindana tu hakuna wa kuthubutu kuanza na mtu
 
Back
Top Bottom