Je Askari Polisi anaweza kushitakiwa mahakamani kwa uongo ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,694
239,260
Naomba wajuzi wa sheria wanisaidie mimi na wadau wengine .

Natambua kwamba kuna askari wameshitakiwa kwa makosa mbalimbali akiwemo Mtukufu Zombe.

Sasa swali langu linaegemea kwenye UONGO ( visingizio vya uongo kwa nia ovu ya kushughulikia vyama vya siasa ) , hii lugha ya tumesikia , tumehisi , inteligensia etc.

Mara nyingi hivi vitu vinavyosemwa kuwa vimefahamika kutokana na intelijensia imebainika kuwa havipo , ndio maana nauliza kwa uongo kama huu , askari aliyehusika na tamko hilo anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria hata kwa miaka ijayo kama siyo leo ?

Lengo hapa ni kuhamasisha haki na nidhamu ya kweli ndani ya jeshi la polisi .
 
Ikifanyika hivyo CCM itakuwa ICU
Lengo langu si kudhoofisha ccm , maana tayari iko dhoofuli hali , tunataka kufahamu tu kama jambo hili linawezekana ili labda huko mbele sheria ichukue mkondo wake .
 
Back
Top Bottom