Je, Askari Anaruhusiwa Kutumia Silaha yake Pasipo Amri? Pale Nyololo ilikuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Askari Anaruhusiwa Kutumia Silaha yake Pasipo Amri? Pale Nyololo ilikuwaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by eedoh05, Sep 14, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Kwa sheria za kijeshi, askari wa chini kicheo au aliyechini ya Kamanda wa Oparesheni haruhusiwi kutumia silaha yake hadi apokee amri ya kamanda wake ya kutumia silaha hiyo. Sio hivyo tu, askari anapokuwa kwenye oparesheni yo yote haruhusiwi kufanya cho chote pasipo amri ya kufanya jambo fulani, mathalan, kusonga mbele, kuinama, kwenda kushoto au kulia, hadi aamrishwe kufanya hivyo.

  Swali langu ni hili: Wakati wa oparesheni ya pale Nyololo siku ile Mwandishi wa ''Channel Ten'' marehemu Daud Mwangosi alipouliwa na polisi. Je askari waliokuwa katika oparesheni ile walijifanyia kazi zao pasipo amri ya mkubwa wao? Kama walipokea amri toka kwa kamanda wao, kwa nini kamanda huyo hajafikishwa mahakamani?
   
 2. Root

  Root JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,263
  Likes Received: 12,981
  Trophy Points: 280
  alie rusha bomu alipewa amri kwani bila amri hamuwezi anza rusha mabomu labda iwe kwenye situation ambayo wewe kama askari watu wengi wanataka kukudhuru
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hoja yako ya msingi sana.

  Katika tukio lile hata picha zinaonyesha mtafaruku huku kuna baadhi akiwamo OCD aliyejeruhiwa kuzuia mauaji yake na baadhi ya askari kujaribu kuwazuia wengine, lakini wengine walionekana kama fisi wanaogombania mzoga ulioachwa na simba. Kitendo kile kimenishangaza sana.

  Kawaida askari ye yote hufanya kazi kwa kupata maelekezo kutoka kwa kiongozi nini cha kufanya lini na wapi. Askari hata vitani hawezi kufyatua bunduki bila maagizo ndivyo nilivyofundishwa katika light military training (Jeshi la Kujenga Taifa), isipokuwa tu inapotokea kukutana under-fire vitani na adui inapolazimika ile ya piga nikupiga, napo kilanja ndiye anayeamrisha kufanya hivyo au kukimbia kujinusuru kama wanazidiwa.

  Matukio mengi jeshi la polisi yanaonyesha kwamba hakuna amri moja inayoongoza utekelezaji wa utendaji wawapo katika kuongoza matukio ya waandamanaji.

  Wapo kama genge la wavuta bangi vile, no control.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Iweje apewe amri na aliye juu yake OCD akionyesha ishara ya kuzuia. Kama angetoa amri asingesimama karibu na victim kiasi cha kuhatarisha usalama wake.
   
 5. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,927
  Likes Received: 950
  Trophy Points: 280
  hapo ndipo inapodhihirika udhaifu mkubwa ktk mafunzo ya polisi na mfumo mzima wa uajiri.
   
 6. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  ni Policcm haoooooo!
   
 7. N

  Nguto JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,654
  Likes Received: 629
  Trophy Points: 280
  Hata akipewa amri na mkubwa wake ni kosa la jinai. Polisi hwaruhusiwi kutumia nguvu kupita kiasi wanapomkamata mtu. Hii ina maana hata kupiga hawaruhusiwi. Soma post ya Mzee Mwanakijiji ameweka sheria hiyo!!!
   
Loading...