JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Jibu la swali lililopo kwenye kichwa cha uzi huu ni HAPANA.
Melezo kwa uchache ni kama ifuatavyo;
Askari Polisi anayo haki na wajibu wa kukuhoji baada ya kukutajia haki zako na kukupa maelezo ya onyo, lakini hana
mamlaka ya kukulazimisha kuongea kitu chochote ambacho hutaki kusema/kukiri makosa ambayo hukufanya au kutoa maelezo.
Ikiwa mtuhumiwa amekataa kuongea ni wajibu wa Polisi kukupeleka Mahakamani ndani ya saa 24.
Ungamo la kosa litokanalo na kuteswa linalofanywa mbele ya Askari Polisi kwa namna yoyote ile halitakubalika Mahakamani kama ushahidi