Je, asiye mwanasheria anaweza kumsaidia mtu asiyeweza kujieleza mahakamani na kumtetea?

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Naomba kuuliza,

Kuna ndugu yangu yupo mahakamani hana uwezo wa kujieleza mbele ya mahakama, je mimi raia wa kawaida nisiye mwanasheria naweza nikamsaidia kumtetea na kumsaidia kwenye shughuli zake za kisheria? Kama ni ndio hii sheria ni mpya na imeanza lini ya kumruhusu mtu wa kawaida.

Ahsanteni.
 
Naomba kuuliza, kuna ndugu yangu yupo mahakamani hana uwezo wa kujieleza mbele ya mahakama, je mimi raia wa kawaida nisiye mwanasheria naweza nikamsaidia kumtetea na kumsaidia kwenye shughuli zake za kisheria? kama ni ndio hii sheria ni mpya na imeanza lini ya kumruhusu mtu wa kawaida.

Ahsanteni.

Hauwezi
 
Unachoweza kumsaidia huyo ndugu ni kumpa mbinu zakuzitumia mahakamani ili ashinde.

Miongoni mwa mbinu ni kuwa jasiri, asiwe muongeaji sana, asiulize au kujibu bila kuruhusiwa na muda wote aangalie picha ya raisi iliyojuu nyuma ya hakimu yaani asiangalie chini. Au amuangalie hakimu kama akishindwa kumuangalia usoni basi kwenye paji LA uso.
 
Naomba kuuliza,

Kuna ndugu yangu yupo mahakamani hana uwezo wa kujieleza mbele ya mahakama, je mimi raia wa kawaida nisiye mwanasheria naweza nikamsaidia kumtetea na kumsaidia kwenye shughuli zake za kisheria? Kama ni ndio hii sheria ni mpya na imeanza lini ya kumruhusu mtu wa kawaida.

Ahsanteni.
Anaweza akichukuwa legal powers toka mahakamani kama wakala wa mtuhumiwa.
 
Utetezi inategemea na Aina ya kesi,jinai,mauaji na uhaini huwezi ila Kwa madai hasa ngazi ya mahakama ya mwanzo unaweza

Kuna Ka kiapo huwa kanaapwa nadhani mahakamani au Kwa mwanasheria kanaitwa power of attorney ukiwa nako hako basi hapo unasimama badala ya mtuhumiwa au mshitaki wanasheria njooni mfafanue zaidi
 
Kazi ya kumwakilisha mtu mahakamani ni ya wakili japo kuna exception flan flan hivi....kwa mfano unaweza kumwakilisha ndugu yako mahakama ya mwanzo, na hata baraza la ardhi la wilaya, mahakama kuu kitengo cha kazi, CMA n.k
 
Naomba kuuliza,

Kuna ndugu yangu yupo mahakamani hana uwezo wa kujieleza mbele ya mahakama, je mimi raia wa kawaida nisiye mwanasheria naweza nikamsaidia kumtetea na kumsaidia kwenye shughuli zake za kisheria? Kama ni ndio hii sheria ni mpya na imeanza lini ya kumruhusu mtu wa kawaida.

Ahsanteni.
Fafanua tatizo kwanza.
Hiyo kesi ni jinai au Madai
Ndugu yako ni Mtuhumiwa au Mlalamikaji
Ndugu yako ni Mdai au Mdaiwa

Kama inawezekana eleza kisa kidogo tuichambue.
 
Back
Top Bottom