Kila Mtanzania ana haki ya kupata hati ya kumiliki nyumba au ardhi, vitu ambavyo vinaweza kumsaidia baadae kupata mikopo katika taasisi za Serikali au binafsi.Lakini hadi sasa ni asilimia kumi na tano ( 15 % ) tu ya Watanzania wote wenye kumiliki hati hizi.
Asilimia themanini na tano ( 85 % ) hawana hati za nyumba.Hawa 85 % ambao hawana hati sio kwamba hawapendi kupata hati hizo bali inatokana na ugumu uliojengwa na watu ardhi ambao hutaja gharama kubwa za kutisha.
Ukubwa wa gharama hizo ni moja ya bomu ambalo waziri wa ardhi Mh.Lukuvi hajawahi kulitegua na wala hajui kama lipo.
Kupata hati ya nyumba ugumu wake ni sawa na tajiri alienenwa kwenye biblia kuwa ugumu wa kuuona au kuingia kwenye ufalme wa Mungu ni sawa na ngamia asivyoweza kupenya tundu la sindano.
Taasisi zote za Serikali zina utararatibu maalum uliowekwa wazi juu ya gharama katika kutoa huduma mbali mbali.
Kwa mfano wizara ya afya ina bei elekezi katika kuchangia gharama za matibabu, TANESCO nao wana gharama maalum katika kila huduma wanayotoa, idara ya maji nayo ina mfumo mzuri unaonyesha gharama katika kila huduma wanayotoa.Lakini wizara ya ardhi haina huo utaratibu bali kila mtumishi ana gharama zake ambazo ameziweka kichwani.
Mimi nina nyumba ilioko katika ukubwa wa hatua au mita 70 kwa 40 lakini nimeshindwa kupata hati kwa muda mrefu kwa sababu wahusika wanadai kulipwa milioni tatu hadi tano ( 3, 000,000/= ).
Gharama hizi ni pamoja na kusafirisha vifaa vya kupimia ambavyo wao hudai ni delicate na vinathamani kubwa kupindukia, posho ya wapimaji na usumbufu mwingine.
Gharama hizo zimenishinda na hadi leo sina hati ya nyumba.Gharama hizi ndio hizi hizi ambazo huwakwamisha na watu wengine.
Wizara ilipaswa kuweka bayana gharama zote kuanzia ukubwa fulani wa eneo hadi ukubwa fulani ikiwa na pamoja na kutoa risiti ya Serikali.
Hivi karibuni hapa katika mji mdogo wa Mlandizi idara ya ardhi imetoa tangazo kwa wanainchi wote wa Mlandizi kuwa wajiandikishe kwa ajili ya kupimiwa ardhi au nyumba kwa ajili ya kupata hati ya nyumba.
Gharama zilizotajwa ni aina moja kwa watu wote, uwe una eka moja, nusu eka au robo gharama ni moja.Ikiwa gharama ni moja kwa kila mtu basi wahusika wana uhakika wa kuvuna mabilioni ya hela.
Tunamwomba waziri Lukuvi afike Mlandizi aje atueleze ni vigezo gani hutumika katika upimaji huo na je ikiwa yeye ndie mwenye dhamana na wizara hiyo kwa nini ameshindwa kupanga gharama za upimaji ziwe aina moja na zijulikane pote nchini kwa manufaa ya wote.