Je, Aquilina ameuawa na risasi iliyofyatuliwa na Polisi? Ni vigumu sana kuthibitisha hilo kwa kutumia Polisi wa Tz.

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,442
55,017
..Nitawakumbusha tukio la kuuwawa Daudi Mwangosi.

..zilikuwepo jitihada za kuwaangushia lawama na hata kuwatuhumu CDM.

..kusingekuwepo ushahidi wa PICHA na VIDEO tukio lile mpaka leo lingekuwa linachunguzwa.

..nimemsikiliza RPC Mambosasa na hisia zangu ni kwamba itakuwa vigumu sana kuthibitisha kama ni kweli Aquilina ameuawa na risasi iliyofyatuliwa na Polisi wetu.

..So far, RPC Mambosasa anadai Aquilina amekufa kwa kupigwa na " " "KITU CHENYE NCHA KALI". Hasemi kama ameuawa na risasi!!

..Lingine RPC anasema tukio la kuuwawa Aquilina litachunguzwa kama matukio mengine. Anasema hakutakuwa na "double standards."

..Hii maana yake ni kwamba uchunguzi wa tukio hili siyo priority kwa jeshi la Polisi. Tutegemee matokeo ya uchunguzi wa tukio hili kuchukua muda mrefu, au kutokupata majibu kabisa kama tulivyozoeshwa.

..Kwa hiyo, tujiandae kwa majibu kama, " UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA..."

..Lingine RPC Mambosasa amedai wako Polisi wawili waliojeruhiwa na waandamanaji waliokuwa wakiwashambulia Polisi kwa mawe na silaha zingine za jadi. Kwa hiyo hapo anajenga uhalali wa Polisi kutumia silaha hata za moto kwani wenzao wawili wamejeruhiwa!!

..Kwa kifupi ni kwamba Polisi wanatakiwa wachunguzane wenyewe kubaini kama mmoja wao ndiyo amefyatua risasi na ikamuua Aquilina. Ni ngumu sana kuthibitisha hilo kwasababu ya hulka ya kulindana hata kwenye maovu iliyojengeka Tanzania.

..MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA AQUILINA. MUNGU AWAPE FARAJA, WAZAZI, WANAFAMILIA, NDUGU NA MARAFIKI WA MAREHEMU.

Pascal Mayalla, Richard, chige, MsemajiUkweli
 
Back
Top Bottom