Je, ambao hamkupandishwa daraja mwezi uliopita kuna mtu amepanda au ndio tunasubiri bado?

Tough lady

Senior Member
Jul 24, 2013
151
182
Mshahara umetoka na jina langu lilikuwa kwenye orodha ya wanaopanda madaraja, mwezi wa 6 sikupanda nikitarajia kuwa mwezi huu nitapanda. Je ambao hamkupandishwa daraja mwezi uliopita kuna mtu amepanda au ndio tunasubiri bado?

Kwa mtakaoniuliza kuhusu barua; waliopanda daraja mwezi uliopita manispaa yetu ya Kinondoni walipewa barua baada ya mshahara kutoka. So namimi jina lilikuwa kwenye orodha ila barua hazikuja na ambao waliopanda walipewa barua baada ya kupanda.

Na mtakaosema watu hupanda kwa kutegemea bajeti naomba niwajulishe kuwa daraja huwa linapanda mwezi wowote. Ongezeko (increment) ya mshahara ndio huwa inafanyika mwezi wa 7 tu.

Swali hapa la msingi ni je kuna watu mmepanda ambao mlisubiri kupanda kama mimi?

Nafahamu inabidi niende kwa afisa utumishi ila nataka kwanza kujua kama tuliobaki kuna watu wamepansa au labda wote tutapandishwa baadae au taratibu?😊
 
Mi sijapanda na nilitegemea kupanda mwezi huu sijui tatizo nini, na wengi hapa manispaa ya morogoro hali ni hiyo hiyo, watu wameajiriwa mwaka 2013 mpaka leo kupanda daraja hakuna, Hii serikali Inatutesa sana mpaka morali ya kazi hakuna tena,
Tutawapandisha tukimaliza kumsingizia kesi za ugaidi Mbowe
 
Mi sijapanda na nilitegemea kupanda mwezi huu sijui tatizo nini, na wengi hapa manispaa ya morogoro hali ni hiyo hiyo, watu wameajiriwa mwaka 2013 mpaka leo kupanda daraja hakuna, Hii serikali Inatutesa sana mpaka morali ya kazi hakuna tena,
Unaonaje ukiiacha kazi Ili baadhi ya watu ambao bado hawajapata ajira wapate? Najua wao watakuja na morali ya kazi.
 
Alafu walimu bana!!! Si mnasemaga elimu ni ufunguo ya maisha mbona maisha yenu yamefungwa (kwenye mshahara duni)??
 
Poleni ambao hamjapandishwa mwezi huu! Ni jambo linaloleta maumivu makali. Pambaneni mpaka mwisho ili mpate haki zenu. Binafsi namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuyaangaza haya maccm na serikali yake!!

Hatimaye yamenipandisha aisee! Nimeona mabadiliko. Sina sababu yoyote ile ya kuyashukuru! Maana nilitakiwa kupanda tangu 2018! Hii 2021, ilikuwa nipande kwa mara nyingine tena! Ila ndiyo hivyo tena, eti tulikuwa tunanunua ndege kwanza!!
 
Mshahara umetoka na jina langu lilikuwa kwenye orodha ya wanaopanda madaraja, mwezi wa 6 sikupanda nikitarajia kuwa mwezi huu nitapanda. Je ambao hamkupandishwa daraja mwezi uliopita kuna mtu amepanda au ndio tunasubiri bado?

Kwa mtakaoniuliza kuhusu barua; waliopanda daraja mwezi uliopita manispaa yetu ya Kinondoni walipewa barua baada ya mshahara kutoka. So namimi jina lilikuwa kwenye orodha ila barua hazikuja na ambao waliopanda walipewa barua baada ya kupanda.

Na mtakaosema watu hupanda kwa kutegemea bajeti naomba niwajulishe kuwa daraja huwa linapanda mwezi wowote. Ongezeko (increment) ya mshahara ndio huwa inafanyika mwezi wa 7 tu.

Swali hapa la msingi ni je kuna watu mmepanda ambao mlisubiri kupanda kama mimi?

Nafahamu inabidi niende kwa afisa utumishi ila nataka kwanza kujua kama tuliobaki kuna watu wamepansa au labda wote tutapandishwa baadae au taratibu?😊
Vumilia approval yupo maternity leave
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom