Je, Amani Karume na Jakaya Kikwete ni wajumbe halali wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM)?

Acha JK arudi kutuibia ili mradi ajali utu, kuliko kuibiwa na watu makatili. Chaguzi zote toka awamu hii imeingia madarakani tulikuwa tukiona unyama, ushenzi na uhayawani wa wazi dhidi ya wapinzani. Katika mazingira hayo unapata wapi nguvu ya kutuonyesha kuwa tulikuwa chini ya watu waadilifu? Asiuze twiga tu, hata akipatikana mtu wa kununua uwanja wa ndege wa Chato amuuzie hata kwa bei ya hasara, hii itachangia kujifunza kutenda haki pindi unapopata madaraka.
Hili taifa bado tuna safari ndefu sana, halafu JK akianza kuiba tena tuamze kumlaumu bora aondoke, hii ni dalili ya wazi kabisa ya watu waliokata tamaa, wamekubali kutumiwa na kila mtawala aliyepo madarakani.
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza...

One thing kinaenda kutokea...
Tutapata freedom of speach ila it will come at a great cost.
Maisha yanaenda kua magumu zaidi coz ya rundo la miradi alioiacha JPM ikiwa tkt 50% plus ya utekelezaji ambayo hawawezi kuiacha na ziaid rushwa, madili na kutokuwajibika vinaenda kutamalaki.

Km Tulivyomkumbuka JK wakati wa JPM now tujiandae kumkumbuka JPM wakati wa Samia, hili halikwepeki kulikataa itakua ni kujidanganya wenyewe.

Watu wanamzungumzia January ila wanasahau January ana kismati tu cha kupendwa km JK ila hakuna mtendaji mule..January ni zao la JK amejifunza kwake namna ya kuzungukwa na wapambe mia mia watakaokufikisha mahala ila pia watakaokula na kusaza mezani kwake.
Hisia zako tu. Nchi itaendelea kama kawaida. Ubishani wa mitandaoni na kukumbuka tawala za nyuma kupo tu hata nani awe Rais.
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza...

One thing kinaenda kutokea...
Tutapata freedom of speach ila it will come at a great cost.
Maisha yanaenda kua magumu zaidi coz ya rundo la miradi alioiacha JPM ikiwa tkt 50% plus ya utekelezaji ambayo hawawezi kuiacha na ziaid rushwa, madili na kutokuwajibika vinaenda kutamalaki.

Km Tulivyomkumbuka JK wakati wa JPM now tujiandae kumkumbuka JPM wakati wa Samia, hili halikwepeki kulikataa itakua ni kujidanganya wenyewe.
Tuchukulie uko sahihi, kwani sasa hivi maisha chini ya Magufuli yalikuwa marahisi, ama yalikuwa yanaenda kuwa marahisi? Yaani msitutishe kabisa kutuhadaa kuwa tulikuwa chini ya mtu sahihi. kilichofanyika chini ya utawala huu wa Magufuli ni kudhibiti vyombo vya habari, na kuhubiri yale atakayo, na sisi wananchi kwa kuwa tulikuwa tunaishi kwa hofu,hatukuthubutu kuhoji ama kupendekeza nini kifanyike, zaidi ya kulishwa propaganda mfu na data za kupika.

Mafuta ya kupikia yalipanda maradufu chini yake, sukari pia bei iko juu. Petrol dunia nzima imeshuka kutokana na janga la corona, lakini hapa kwetu bado iko juu. Je ni ahueni gani tumepata chini ya Magufuli ambayo wakiingia wengine itaondoka? Ninachoona ukatili utaondoka kama sio kupungua, lakini maisha yatakuwa haya haya.
 
Tunahitaji mwanzo mpya. Wenye ubavu wa kuuleta huo kwa gharama nafuu huwezi kumweka pembeni JK.

Kwamba kina Ridhiwani? Hizi ni propaganda uchwara tokea Chatto Inc.

Ashukuriwe mola kwa yote.

Ilikuwa muhimu sana JK akaongezewa ulinzi katika kipindi hiki.

Tuko njia panda.
Kweli kabisa
 
Tuchukulie uko sahihi, kwani sasa hivi maisha chini ya Magufuli yalikuwa marahisi, ama yalikuwa yanaenda kuwa marahisi? Yaani msitutishe kabisa kutuhadaa kuwa tulikuwa chini ya mtu sahihi. kilichofanyika chini ya utawala huu wa Magufuli ni kudhibiti vyombo vya habari, na kuhubiri yale atakayo, na sisi wananchi kwa kuwa tulikuwa tunaishi kwa hofu,hatukuthubutu kuhoji ama kupendekeza nini kifanyike, zaidi ya kulishwa propaganda mfu na data za kupika.

Mafuta ya kupikia yalipanda maradufu chini yake, sukari pia bei iko juu. Petrol dunia nzima imeshuka kutokana na janga la corona, lakini hapa kwetu bado iko juu. Je ni ahueni gani tumepata chini ya Magufuli ambayo wakiingia wengine itaondoka? Ninachoona ukatili utaondoka kama sio kupungua, lakini maisha yatakuwa haya haya.
Inawezekana waandishi wa habari wana kiu sana ya kutoa habari, baada ya waandishi kuanza kuzoea uhuru wa kutoa habari kuna watu watasikia habari wasizozipenda kabisa. Labda mama akaze kwenye uhuru wa kutoa habari.
 
Hili taifa bado tuna safari ndefu sana, halafu JK akianza kuiba tena tuamze kumlaumu bora aondoke, hii ni dalili ya wazi kabisa ya watu waliokata tamaa, wamekubali kutumiwa na kila mtawala aliyepo madarakani.

Mkuu acha JK aje aibe lakini tuwe na uhuru wa kumhoji ama kumkosoa, kuliko kuburuzwa bila uwezo wowote wa kuhoji. Kama huyu aliyepita hakuwa mwizi, kipi kilifanya CAG atolewe kwa kudhalilishwa? Au zile propaganda kuwa mali zetu zinalindwa sana zilikuteka nini? Subiri akina JK wakianza kuiba utawahoji ukiwa huru, kuliko kuambiwa mali zako zinalindwa, lakini unawekewa viongozi kwa shuruti huku watu wakiuwawa na kuachwa na vilema, ili hao wanaosema wanalinda mali zako wakae madarakani kwa shuruti. Kwa bahati mbaya kwangu unafiki imekuwa ni ngumu kuushi.
 
Inawezekana waandishi wa habari wana kiu sana ya kutoa habari, baada ya waandishi kuanza kuzoea uhuru wa kutoa habari kuna watu watasikia habari wasizozipenda kabisa. Labda mama akaze kwenye uhuru wa kutoa habari.

Kwani habari zikidhibitiwa hasa usizozipenda ndio maisha yanaboreka? Ukibana uhuru wa vyombo vya habari, unapunguza uwezo wa wananchi kufikiri, na kufanya mabadiliko stahiki kwenye maisha yao. Matokeo yake unakuwa na taifa la watu duni wanaoburuzwa na viongozi tu kwa ajenda zao. Taifa la namna hiyo ni taifa mfu.
 
Huyo jamaa sitamsahau alipopeleka ripoti yake ya mradi wa umeme kule rufiji juu ya mazingira..!! Eti walishauri choo kiwe KM 10 toka eneo unapotekelewa mradi..!!! Yani kama Rais ni Makamba tusitarijie kitu hawa ni wasomi ambao wanajua kusoma vitabu tu ila kushighulisha bongo zao hapana..!! JPM alimshangaa sana, akamuuliza sasa kama choo kiwe km 10 mtu akienda choon mpaka kurudi si asbh mpaka jion atakuwa anafanya kazi yakwenda chooni? Kazi itafanyika saa ngapi?
Hao sio wasomi ni vibaraka wa wazungu
 
Bado natafakari Mkuu Msiba Mkuu

Tunapoteza sana Viongozi wakuu kwa sababu za ajali, matatizo ya Moyo na Ajali

1)Rais wa Jamhuri JPM
2)Rais wa Znz Abeid Karume
3)Rais Mstaafu Mkapa
4) Chief Secretary Kijazi
5) DG wa Usalama wa Taifa Afande Luten General Kombe
6) Waziri Mkuu Sokoine
7) Makamu wa Rais Dr Omar

Hilo la Makamu wa Rais nadhan atateuliwa mtu asie na malengo ya 'Urais' mbele ya safari
Atateuliwa babu babu fulan syle za kina Philip Mangula
Umekuwa kimya hadi nilishtuka
 
Shigela ni mwanaCCM tokea umoja wa vijana. Sio fisadi .Mimi kama mimi I will go for Shigela.January ni kundi lile la kina Kinana nikifukiria Tembo wetu,biashara za madawa i feel sorry for Tanzania. Nchimbi yeye tatizo uchawi. Yule atamchomoa hata Samia wetu ili tu awe Rais. Alimfanyia mbaya Kipi Malecela kisa uenyekiti wa umoja wa vijana. Nchimbi nae ana elements za ufisadi kipindi kile alikuwa team Lowasa.
Nchimbi team Lowassa
 
wezi watarudi wafanyabiashara fisadi watarudi wauza unga watarudi nidhamu kazini hakuna kama kikwete ndio muamuzi wa kuchagua nani awe
Bora tu kuwe na amani na kuheshimu haki za binadamu, hata wakiwepo hao mafisadi, wasukuma wametutesa sana, naomba Mungu isije kutokea msukuma kupewa uongozi wa juu tena
 
..Na wapinzani ambao wangeweza kupiga makelele na kuibua ufisadi ndio hao Magufuli kawasambaratisha na kuwafyekelea mbali.

..Sasa hivi CCM kuwa waadilifu au mafisadi ni suala la hiyari na utashi wao wenyewe, hakuna wanayemuogopa huku nje.

..Na mwana-CCM yeyote atakayeonewa hana chama cha kukimbilia kama ilivyotokea kwa Dr.Slaa, Mzee Wassira, na Makongoro Nyerere.

..CCM ya aliyoiacha Magufuli ikiamua kumbamiza mwana-CCM yeyote yule basi huyo hana mahali pa kwenda kuponya majeraha yake.

NB:

..sijui CCM wataendelea kudukuana?
Magufuli ametuharibia sana. Amefanya viongozi wajue kumbe unaweza kupora uchaguzi na usifanywe chochote. Unaweza kuvunja katiba na usifanywe chochote. Unaweza kuua na usifanywe chochote. Kwa kifupi vitu vyote ambavyo vilikuwa vinaonekana haviwezekani au watu walikuwa wanaona aibu kufanya amevihalalisha. Tanzania haitakuwa ile ile tena.
 
Back
Top Bottom