Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Simple Logic...
Na G Mallisa,
Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii Chadema ilisimamisha wagombea 85% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu. Kati ya hao 92% walienguliwa na TAMISEMI kwa sababu mbalimbali. Kwa lugha rahisi ni kwamba kati ya wagombea 100 wa Chadema, 92 walienguliwa, na 8 tu ndio waliopitishwa.
Wakati wagombea 92 wakifyekelewa mbali, media hazikuongea, wanaojiita wanaharakati hawakuongea, viongozi wa dini hawakukemea, wanazuoni walikaa kimya.
Chadema ilipoamua kuwaondoa wale 8 waliobakia, media zinaongea, wanaharakati (uchwara) wanaongea, wanazuoni wanaongea, kina Chakubanga wanaongea. Wote wanaitupia lawama Chadema. Wanadai imewanyima wananchi haki ya kuchagua.
Sasa niulize swali, je aliyewanyima wananchi haki ya kuchagua ni aliyefyeka wagombea 92 bila sababu za msingi, au aliyeamua kumalizia 8 waliobakia, kupinga dhuluma waliyofanyiwa wale 92??