Je, aliyetoa 'Taarifa' hii ya 'Majonzi' kwa Vyombo hivi 'Viwili' vya Habari alikuwa ni Mtu Mmoja tu au wapo wengi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,427
108,532
Nipashe Online

Diwani mteule wa Kata ya Kikongo (CCM) Wilaya ya Kibaha, Fatuma Ngozi amefariki dunia na wajukuu wake wawili usiku wa kuamkia leo baada ya nyumba yake kuchomwa moto na watu wasiojulikana.

HabariLeo Online

DIWANI MTEULE AFARIKI KWA MOTO KIBAHA

Diwani Mteule wa Kata ya Kikongo wilayani Kibaha Vijijini Mkoani Pwani Fatma Kingozi na wajukuu zake wawili wamefariki baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea saa nane usiku wa kuhamkia leo ambapo baadhi ya mashuhuda wanasema kuwa mbali ya kufariki kwa diwani huyo mteule watu wengine watano wameokolewa kutoka katika nyumba hiyo.

Tayari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchanguzi zaidi kubaini chanzo cha moto huo umeanza na ukikamilika taarifa itatolewa.

TCRA huku mkiwa wepesi Kutuzimia 'Internet' na muwe pia wepesi 'Kuvionya' na Vyombo vya Habari vyenye 'Uzushi' wa Kuchochea Chuki na Hofu.
 
Kuwa mpinzani sio kwamba usiwe mzalendo kuwauwa hao watoto ni ishara kuwa wewe unaweka maslahi ya chama mbele kuliko hata uhai wa hao ndugu ambao ulitaka kuwaongoza

Hakikutenda haki chama lakini wewe unamuadhibu ambaye yeye pengine hakutegemea kushinda sema malengo ya viongozi wake ni yeye kushinda

Mtanzania mwenzako ni ndugu yako Pasipo na haki tupakosoe lakini wenyewe kutokutenda haki sio kwamba na sisi tusitende haki

Lipa wema kwa ovu huo ndio uungwana

Nawasilisha
 
Mkanganyiko mwingine ni taarifa kutofautiana majina,ina maana kuna watu wawili,Fatuma Ngozi na Fatma Kingozi,haieleweki taarifa ipi ni sahihi.
 
Kuwa mpinzani sio kwamba usiwe mzalendo kuwauwa hao watoto ni ishara kuwa wewe unaweka maslahi ya chama mbele kuliko hata uhai wa hao ndugu ambao ulitaka kuwaongoza

Hakikutenda haki chama lakini wewe unamuadhibu ambaye yeye pengine hakutegemea kushinda sema malengo ya viongozi wake ni yeye kushinda

Mtanzania mwenzako ni ndugu yako Pasipo na haki tupakosoe lakini wenyewe kutokutenda haki sio kwamba na sisi tusitende haki

Lipa wema kwa ovu huo ndio uungwana

Nawasilisha
Kwahiyo hiyo nyumba imechomwa na wapinzani?
 
Back
Top Bottom