Je, alcohol Spraying ina madhara yapi kiafya?

luvcyna

JF-Expert Member
Feb 24, 2009
1,848
1,938
Ndugu zangu wa JF salam kwenu,

Kwa wataalam na wenye uelewa wa mambo ya afya naombeni elimu kidogo kuondoa hofu niliyonayo na umri huu akili imevurugika kabisa.

Nilitoka safari jana nikiwa nadrive my own vehicle kwa hofu ya hili janga la corona. Nyumbani kwangu kuna utaratibu wa kumspray kila mtu anayeingia getini mwili mzima kuanzia kwenye nywele mpaka miguuni kwa kutumia huzi spraying bottles za kawaida ambapo tunaweka detol mil 20 na kuchanganya na maji nusu lita.

Now kwa hofu iliyonitanda niliona nijisanitize mwili mzima kwa kutumia hiyo spray i mean mpaka usoni kushuka miguuni.

Tatizo lilianza baada ya kama nusu saa nikahisi kifua kimenibana na kikohozi kisichoisha.
Nimeendelea kukohoa sana mpaka hivi sasa na leo siku ya tatu ninaanza kuona joto la mwili likipanda na kiuno kuuma.

Nimebaki na maswali mengi kichwani na uzee huu, ni hili gonjwa limeshapiga hodi au ni madhara ya ku in hell alcohol nyingi kifuani?

Naombeni mawazo yenu jamani kuna madhara yanayoletwa na ku in hell alcohol nyingi kiasi cha kufikia kupata homa hivi?

Nitashukuru sana kwa majibu yenu. Mniwie radhi kwa maelezo marefu, hofu imenitanda
 
Uchovu wa safari. Pumzika utakua sawa, achana na hizi taharuki zisizo na msingi za corona.
 
Mkuu wewe kapime tu.

Huu ni mtihani mwingine tena..
Naona nikiyapata najibu yatanisumbua zaid kama sio mazuri.

Nimebaki najiuliza tu wife ananiambia kwani kwwnye maisha yako ndio mara ya kwanza kukohoa na kupata homa?

Ngoja nikazitafute tu hizo anti inflammatory tablet nitwange sijui kama bongo wanaziuza wapi
 
Huu ni mtihani mwingine tena..
Naona nikiyapata najibu yatanisumbua zaid kama sio mazuri.

Nimebaki najiuliza tu wife ananiambia kwani kwwnye maisha yako ndio mara ya kwanza kukohoa na kupata homa?

Ngoja nikazitafute tu hizo anti inflammatory tablet nitwange sijui kama bongo wanaziuza wapi
Anti inflammatory ni nyingi tu kama Cetrizine....pesa yako tu
 
Back
Top Bottom