Je aishi vipi na mama wakambo kwani mama wa kambo simama..../// | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je aishi vipi na mama wakambo kwani mama wa kambo simama....///

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by bakarikazinja, Feb 18, 2011.

 1. b

  bakarikazinja Senior Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilimkuta akilia huku kichwa amekiweka juu ya meza na mikono miwili imeshika kichwani mithili ya mtu aliyekata tamaa nilimsogelea karibu na kumuuliza yaliyo msibu akanijibu baba yake anataka kuoa mke mwingine na ule ulikuwa ni mwezi wa tato toka mama yake mlezi afariki kwa hasira huku akitweta alinijibu haiwezekani baba hao mwanamke mwingine wala kamwe sitakubali hili wazo lake kwani sasa naona anataka kunitia kwenye chungu cha moto na kunipalia makaa kisha akaniuliza kwani wewe siunajua mama wakambo si mama nikamwambia subiri nitakupa jibu lako ndio nikakimbilia wana jamvi mnishauri ni mwambie nini maskini rafiki yangu huyu kwani mimi sina uzoefu na hili swala//
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Aliyesema mama wa kambo si mama nani? Hebu acheni fikira mbaya hata hajamuona huyo mama kashaanza kumfikiria vibaya.

  Mimi sioni shida ya huyo Baba kuoa sababu anahitaji mwenza
   
 3. s

  seniorita JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  jamani miezi mitano tu, kwani kamaliza kuomboleza? huyo baba must give his child enough time to grieve for his/her mother na sio kuongeza another psychological trauma before one is over...then baba must give his children enough time to prepare them for his new wife...so wa kumshauri ni huyo baba....
   
 4. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Huyo baba kama anataka kuoa baada ya miezi mitano mke kufariki inaonyesha alikuwa na uhusiano na huyo mama toka zamani sasa wanataka kuhalalisha tu. Na huyo rafiki yako kama ameweza kukuuliza maswali hayo basi sio mtoto ameshapata akili za kiutu uzima sidhani kama atashindwa kuishi na huyo mama wa kambo
   
 5. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135

  Dena upo mpenzi ulipotea sana lol
   
 6. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Nimerudi na nilisalimia labda hukuona salamu zangu.

  Nipo mwaya huna ndugu Gongo la Mboto??? Mie nina mmoja lakini kanusurika
   
 7. LD

  LD JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Na hapa napo naishangaa akili za wanaume.
  Yani kafariki miezi mitano tu anataka kuoa mke mwingine hadi watoto wanajua?? Inamaana hata machungu yameshaisha yani!! Duuu na huyo anayetaka kuolewa akiambiwa yeye ndo kamuua huyo mama asilalamike kwa kweli.
   
 8. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Sina mpenzi dah hii nchi yetu nayo bana taaaaaabu tupu
   
 9. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Unatamani hata usirudi nchini kabisa.

  Haya nenda katoe damu basi nasikia kuna uhaba sana
   
 10. b

  bakarikazinja Senior Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maty na shukuru sana kwa ushauri wako pamoja na ld na dena hata mimi nilishindwa cha kumshauri huyu rafiki yangu lakini nikajua humu jamvimvini alialibiki neno na wala alishindikani neno
   
 11. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Kiukweli kabisa hapa nachokiona mimi tatizo kwa huyu mshichana ni muda tu wa huyo mdingi wake kuoa kama maty alivyosema huyu mdingi alikuwa na uhusiano na huyo mwanamke kabla ya mama yake msichana kufariki.

  Kwa hali ya kawaida ndani ya miezi sita huwezi kutaka kuoa kwa kipindi kifupi kiasi hicho.

  Maana kufiwa na mke/mume ni balaa unakuwa kama unamuona vile bado yuko ndani machungu hayajaisha.

  Yeye amwambie mdingi asubiri kidogo muda angalau mwaka/miaka

  Ila huyo msichana aache fikira ya kuwa hawezi kuishi na mama wa kambo
   
 12. Dinnah

  Dinnah JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mama wa kambo anaweza kuwa mama kama tu baba akiwa amepata bahati ya kupata mke mwenye huruma na kukuchukulia kama mwanae, pia hata kama mama wa kambo akiwa mbaya, baba akiwa makini anaweza kuwa mkali na kummuonya mara kwa mara huyo mama kuhusu watoto wake na mambo mengine ya kifamilia. mwambie tu amshauri baba ake kuwa aubiri kidogo hata akupe muda na wewe wa kuzoeana na mama mpya na yeye pia ili amwelewe ni mtu wa aina gani kwa kuwa tangu mama ako amefariki ni kipindi kifupi.

  kitu kingine naona kama huyo rafiki yako kashafikia age fulani ya mtu mzima kwa hiyo hakuna atakaloweza fanyiwa yeye bila ufahamu wake, na miaka ishaenda karibu na yeye ataendelea na maisha yake,ikiwa bado unasoma college basi kakae hostel kuepusha shari
   
 13. b

  bakarikazinja Senior Member

  #13
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nashukuru sana nilimwambia hasa kama vile dinna uliyo nishauri na hali ni elewa lakini cha kushangaza bado ana asila na baba yake hataki hata kumuona machoni pake kisa e anasema uamuzi wake mbaya na hili ni vipi au nimuache yeye mwenyewe ajuane na baba yake au niendelee kumshauri
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Huyo rafiki yako ana umri gani?
  Bado anasoma au?
  Nitarudi b'dae.
   
 15. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,361
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280
  Lakini inaonekana Baba ana upendo na watoto mpaka amewaeleza hiyo issue, sasa watoto wamuombe baba yao avute subira angalau mwaka upite hivi, baba naye akili mkichwa aweke hawara huko pembeni aendelee kuwalea watoto kwenye nyumba nyingine/hiyo wanayoishi.

  Nami naunga mkono hoja kuwa ndani ya miezi sita inatia shaka, hakika huyo mzee alikuwa na uhusiano na huyo mwanamke hata kabla mkewe hajafa.
   
 16. b

  bakarikazinja Senior Member

  #16
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni kweli anaupendo na watoto wake tena sana ila ili swala la kuoa ndio limewauzi sana kuhusu umri husniyo ni miaka 22yrs
   
 17. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kumbe mkubwa tu. mwambie asiwe na wasiwasi, kuna wamama wengi wa kambo ni wazuri tu.
  Mimi mama yangu alilelewa na mama wa kambo na hakuwa na shida yoyote.
  Anachotakiwa ni kuwa na nidhamu na kumsikiliza huyo mama kama mama yake mzazi.
  Inabidi amsome vizuri huyo mama ni nini anapenda na nini hapendi. Aondoe mawazo potofu juu yake.
   
 18. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kiukwel wanaroho mbaya asilimia kubwa!wangekua wanamalez mazur wala uyo mtt asingeumia roho nawajua fika mana nimeishi nao.
   
 19. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Mimi nimelelewa na mathe wa kambo, sina tatizo naye hata sasa. Kuhusu huyo dingi, hembu give him a break jamani! Nadhani wengi mnajua maisha ya kuwa na mke... Kule kupewa care kama za mtoto, kupelekewa maji kwa bafu, nguo unajua kuchafua hujui kufua, mataim unasahau hata kubrash kiatu! Nadhani wamama wakisafiri wanajua jinsi wanavyokutaga nyumba zao, chupi juu ya kikombe na soksi kwenye friji. So inawezekana dingi ataka kuoa karibuni coz amechoka kusimamia show mwenyewe. A house needs a manager bwana!
   
 20. LD

  LD JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  CHUPI JUU YA kikombe!! Kweli wanaume hawakui!!
   
Loading...