Je Afrika kutawaliwa na china miaka michache ijayo..!!!?

Omary Ndama

JF-Expert Member
Apr 16, 2017
3,367
4,056
Yafahamu mataifa 10 yanayodaiwa na China barani Afrika

Reli ya Kisasa iliyojengwa Kenya

10. Congo DRC - Usd 3.4 Billion.

Taifa hili lilikuwa Taifa la kwanza kabisa kuingia Mikataba ya Mambo ya madini na Taifa la China.

09. GHANA - Usd 3.5 Billion.

Hali ya Ghana kiuchumi ni Mbaya kwa sasa kiasi kwamba imebidi wayakubali Masharti kadhaa ya IMF ili waweze kupewa Masaada wa pesa ili walipe deni la China.

08. NIGERIA - Usd 4.8 Billion

Kutokana na deni hili kuwakaba koo, Taifa hili kubwa la Afrika ya Magharibi sasa imebidi liikubali Shilingi ya China (Chinese Yen kutumika kama fedha ya kigeni katika Taifa lao - Foreign Currency)

07. CAMEROON - 5.5 Usd Billion

China imekubali kuwasamehe Cameroon sehemu ya Deni hili kwa masharti ambayo hayajawekwa hadharani.

06. ZAMBIA - 6.0 Usd Billion.

China imechukua Shirika la Umeme la Zambia kama Sehemu ya Malipo ya deni hili mara baada ya Zambia kushindwa kulipa...Republic of Zambia sasa unaweza kuiita.
05. SUDAN - 6.4 Usd Billion

Sudan kwa sasa wamepeleka Ombi maalumu huko China kuomba Msamaha wa Sehemu ya Deni,

04. CONGO BRAZAVILLE - 7.3 Usd Billion

Deni hili kwa sehemu kubwa Limesababishwa na Rushwa iuliyoshamiri nchini humo, fedha nyingi zimeliwa bila manufaa yoyote, Hali tete.

03. KENYA - 7.9 Usd Billion

Mabilioni haya mengi yalikopwa kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu, lakini fedha nyingi zimeliwa na wajanja, Deni hili kubwa limechochewa hasa na Rushwa, Reli ya SGR kenya imejengwa kwa Gharama mara 4 zaidi ya Gharama za viwango vya kimataifa ..hata hivyo kenya imeongeza Ushuru wa Mafuta na bidhaa mbali mbali ili iweze kulipa deni hilo, na pia imeomba Msaada IMF na kuyakubali Masharti yao.

02. ETHIOPIA - 13.5 Usd Billion

Walikopa mapesa mengi kwa ajili ya maradi wa reli ya kutoka Ethiopia kwenda Djibouti, deni hili kubwa leo linawagharimu.

01. ANGOLA - 25 Usd Billion.

China wanaendelea kuchukua Mafuta kwa wingi huko Angola kama Sehemu ya malipo ya deni lao.
 
Mimi nachojua Tanzania tunatawaliwa kama wamechukua gesi yetu yote ambayo wanaitumia kwao kwa bei ndogo sisi huku tukiendelea kusema ni ghari kwa gesi asilia kuwa gesi kwa ajili ya matumizi ya majumbani tena mkataba wa karne moja unategemea nini...Mkuu unaizungumzia Nigeria wakati hapa hapa mifano ipo mingi...
 
Mimi nachojua Tanzania tunatawaliwa kama wamechukua gesi yetu yote ambayo wanaitumia kwao kwa bei ndogo sisi huku tukiendelea kusema ni ghari kwa gesi asilia kuwa gesi kwa ajili ya matumizi ya majumbani tena mkataba wa karne moja unategemea nini...Mkuu unaizungumzia Nigeria wakati hapa hapa mifano ipo mingi...
Du ipo kazi. Hivi wamechukua gesi yote kuanzia mtwara, songas, visiwa vya mafia na ile ya tanga? au ni ya mtwara tu?
 
Back
Top Bottom