Je, Afrika inaweza kupambana na Corona bila ya msaada wa Umoja wa Mataifa?

CARIFONIA

JF-Expert Member
Aug 17, 2013
518
901
Kwanza kabisa napenda kuto salamu zangu za dhati kwa wote member wa jukwaa hili, matumaini yangu ni kwamba wote tu wazima na tunaendelea na ujenzi wa taifa letu.

Pasipo kupoteza muda ngoja nijikite kwenye mada kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, ni wazi kila mtu anatambua kua kwa sasa dunia nzima inapita katika changamoto mbalimbali na changamoto hizi zimesababishwa na kuzuka kwa huu ugonjwa wa corona na athari zake zimejitokeza katika kila sekta lakini athari kubwa ni kua ugonjwa umesababisha vifo vya wapendwa wetu na pia vimeaharibu kwa kiasi kikiubwa uchumi wa kila nchi.

Ni kiludi katika kichwa cha hoja yangu hapo juu ni je sisi kama wa Africa tunaweza kupambana katika vita hii pasipo msaada kutoka umoja wa mataifa? Nimeamua kuuliza swali hili ili tu kuweza kupata maoni kutoka kwenu wadau. Kwani mimi nimekua na mashaka sana na huu umoja wa mataifa hasa linapokuja swala linavyo toa mahamuzi kwa hizi nchi za dunia ya tatu hususani sisi Africa.

Umoja wa mataifa kupitia mashirika yake mbalimbali yamekua na mahamuzi yanayotia mashaka sana kwa nchi maskini na mara nyingi umoja huu unashindwa kuchukua hatua kwa nchi za magharibi pale zinapokwenda kinyume na kanuni walizojiwekea, mfano mzuri ni mahakama ya umoja huu imekua ikilaumiwa sana kwa kuangalia sana hizi nchi maskini huku ikizikingia kifua nchi za magharibi, mfano mzuri ni raisi msataafu wa marekani Bwana Bush alipokua madarakani alihivamia nchi ya Iraq pasipo idhini ya umoja wa mataifa kwa madai nchi hiyo inamiliki silaha za nyukilia Kitu ambacho mpaka leo marekani aijaweza kuthibitisha kama walikuta silaha hizo za nyukilia, licha ya mamia ya watu kupoteza uhai wao lakini pia uchumi wa Iraq umeharibika na umoja wa mataifa aujachukua hatua yoyote ile kwa Bwana Bush

Tukirudi kwenye janga la corona tunaona shiraka la afya duniani WHO ambavyo limekua likitutia mashaka sana hasa kwa nchi zetu hizi za Africa na watu wanashindwa kutambua shirika hili limekua likitoa tahadhari au vitisho kwa Africa mahana kila kukicha linakuja na tamko jipya kiasi kwmba watu wanashindwa kuelewa washike lipi, na matamko yao mengi ni kama yanalenga kuogopesha watu na wala sio kutusaidia.

Hivi karibuni raisi wa madagasica katangaza dawa yake kua inatibu corona lakini shirika hili limekua la kwanza kutoa matamko ya kuipinga dawa hii na madai yao ni kua dawa hii inaweza kua na madhara kwa binadamu, hapa swali la kujiuliza dawa hii ilikua inatumika tangu zamani kutibu magonjwa mengine kama maralia na aikua na madhara kwa watumiaji iweje bahada ya kutangazwa kua inatibu corona ndio inahanza kutiliwa mashaka. Je inshu ni kwa kua imegunduliwa na Africa.

Na sio kwamba na ipigia promo dawa hii ila najaribu tu kufikiria je ni madawa mangapi shirika hili limetoa kibali kutumika kwa binadamu licha ya kua na madhara makubwa kwa binadamu kisa tu wagunduzi wake ni wazungu?

Binafisi mimi nahamini hakuna ugonjwa usio kua na tiba kila ugonjwa unatibika, sema kinachofanyika ni kutuaminisha kwamba kuna bahadhi ya magonjwa hayana tiba ili wafanye biashara, kwa ufupi hawa jamaa ni wataalamu wa kutengeneza matatizo na kuyatafutia ufumbuzi ili wafanye biashara Mfano mzuri ni computer wametengeneza kirusi kinachoweza kuharibu programu za computer then wakaja na solution la kupambana na virusi hivyo ambayo ni antviruse hizi zote ni mbinu za kibiashara.

Na hii corona nahisi mambo ndio yale yale wanangoja wangundue chanjo zao hata kama zikiwa na madhara WHO watapitisha kwa mikono miwili na nchi zote zitakiwa kutumia hiyo chanjo.

Ndio hapo najiuliza nchi zetu za Afrika kuna umuhimu wa kupambana na hili janga bila msaada wa umoja wa mataifa au tukubali kua bila wao hatuwezi kupamba na huu ugonjwa hivyo tufate kila mashariti wanayotuagiza?
 
Afrika kupambana Na ugonjwa huu inawezekana endapo viongoz Wa afrika watakapo kuwa Na msimamo mmoja Na kuziondoa fikla za kusema kwamb paspo msaada Wa umoja Wa mataifa hatuwezi.

Endapo wataelewa hlo hakika afrika tutaweza kumshinda adui huyu, Namalzia kusema kwamba Eeeee mungu ibariki afrika Na uijalie ushind dhidi ya janga hili mbariki rais wetu JPM aendelee kuwa na moyo wa ujasiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaweza Kama tutaamua kuwa na fikra huru ya kufanya kile tunachokiamini.Huo Umoja wa Mataifa ni kitengo Cha kulinda maslahi ya watu.Historia iko wazi walivyoazisha kizengwe mwaka 1919 (the League of Nation) Mabeberu Kama German aliukataa kabla ya kuvunjika na kuletwa huu wa Sasa 1945.Africa tunaweza kabisa.
 
Afrika kupambana Na ugonjwa huu inawezekana endapo viongoz Wa afrika watakapo kuwa Na msimamo mmoja Na kuziondoa fikla za kusema kwamb paspo msaada Wa umoja Wa mataifa hatuwezi.

Endapo wataelewa hlo hakika afrika tutaweza kumshinda adui huyu, Namalzia kusema kwamba Eeeee mungu ibariki afrika Na uijalie ushind dhidi ya janga hili mbariki rais wetu JPM aendelee kuwa Na moyo w ujasir.

Sent using Jamii Forums mobile app
tatizo wanatumia umasikini wetu kutugawa kupitia misaada yao na sisi tumehaminishwa bila misaada yao hatuwezi kupambana na huu ugonjwa
 
Inawezekana kwa 100% tatizo lililopo ambalo litasababisha kushindwa ni kwa sababu nchi nyingi ni mwanachama wa WHO so linapokuja janga la kimataifa hao ndiyo wenye jukumu la kutoa hadhari nini kila nchi ifanye kuepa mbali na kinga, dawa itakayoletwa nao.

Hebu fikilia issue ya malaria, ni dawa ngapi tumebadirishiwa mpaka sasa, hapo ndipo utagundua hao mabeberu hawapo na waafrika, wapo kimaslahi tu.
 
Tunaweza Kama tutaamua kuwa na fikra huru ya kufanya kile tunachokiamini.Huo Umoja wa Mataifa ni kitengo Cha kulinda maslahi ya watu.Historia iko wazi walivyoazisha kizengwe mwaka 1919 (the League of Nation) Mabeberu Kama German aliukataa kabla ya kuvunjika na kuletwa huu wa Sasa 1945.Africa tunaweza kabisa.
Tunaweza kama tutakua na umoja na kushirikiana kikamilifu kwa pamoja katika hili jambo ni muda umefika na sisi kuwaonesha kua tunaweza kua na mchango katika maendeleo ya dunia, kwani nimeona nchi nyingi za Africa ikiwemo Tanzania wamegundua dawa zinazosadikika kutibu huu ugonjwa, cha ajabu hawa wenzetu hawatusaidii katika hili ila wanatuponda tu, halafu wako bize kutafuta chanjo ambazo majaribio ya chanjo zao wanataka kufanyia kwetu
 
Inawezekana kwa 100% tatizo lililopo ambalo litasababisha kushindwa ni kwa sababu nchi nyingi ni mwanachama wa WHO so linapokuja janga la kimataifa hao ndiyo wenye jukumu la kutoa hadhari nini kila nchi ifanye kuepa mbali na kinga, dawa itakayoletwa nao.

Hebu fikilia issue ya malaria, ni dawa ngapi tumebadirishiwa mpaka sasa, hapo ndipo utagundua hao mabeberu hawapo na waafrika, wapo kimaslahi tu.
Brother mimi nahami hakuna ugonjwa usio kua na tiba mwenyezi mungu hajawai kua katili kiasi hicho kutuletea majanga yasio kua na majibu hawa jamaa wanachofanya ni biashara na sisi ndio wateja wao, yahani wanaweza kutengeneza dawa ya kurefusha maisha kwa wagonjwa wa ukimwi lakini sio kuja na tiba kamili lengo lao ni kufanya uendele kuishi kwa kutegemea mdawa yao na hapo ndio ushakua mteja
 
H
Hatuwezi, tuko limited sana kwenye masuala ya sayansi, uchumi na afya kwa ujumla.
Vipi kama dunia nzima ingekua ni Africa tu inamahana wote tungekosa majawabu juu ya matatizo yanayotusumbua au ni uvivu wa kutumia akili zetu kukabiliana na changamoto tunazozipitia ndio tatizo?
 
Back
Top Bottom