Je, Adolf Hitler alikuwa katili tu hakuwa na Mema ktk Maisha yake?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,443
ADOLF HITLER NI NANI KTK HISTORIA YA DUNIA?

Wanahistoria Na Watu wengi Duniani wamekuwa wakisimulia kuhusu Maisha ya Dikteta Adolf Hitler Wa Ujerumani .Leo Ninamuelezea kwa kifupi Hitler kuwa ni nani ktk Historia ya Dunia Hii. Je ,Adolf Hitler alikuwa katili tu hakuwa na Mema ktk Maisha yake ? Fuatilia Historia hii .

Adolf Hitler alizaliwa Aprili 20, Mwaka 1889 ktk mji mdogo Wa Austria ujulikanao kama Braunau .Baba yake alikuwa anajulikana kwa jina la Alois Hitler ambaye baadaye alikuja kuwa Afisa Forodha Mkuu .Mama yake Adolf Hitler aliitwa Klara ambaye ni mtu aliyetokea katika familia masikini kabisa ya Kikulima .

Adolf Hitler hakufanikiwa kusoma kwani aliamua kutoroka na kuacha shule mnamo mwaka 1905.Baadaye alitamani sana kusoma chuo cha Sanaa cha Vienna lakini alikataliwa . Historia inaonyesha kwamba Adolf Hitler akiwa shule ya Msingi alikuwa na uwezo mkubwa darasani na alikuwa mtu maarufu sana miongoni mwa wanafunzi wenzake huku sifa za kuwa kuwa kiongozi bora zikimbeba .

Ktk Elimu ya Serikali kulikuwa na ushindani mkubwa sana na hivyo Hitler aliamua kusimama kimasomo .Alisimama kimasomo akiwa na Umri mdogo sana Wa miaka 15 hivyo Elimu rasmi ikawa imemshinda .

Akiwa na Umri Wa takribani miaka 18 aliamua kwenda hadi mjini Vienna huku akiwa na fedha alizokuwa amerithi baada ya baba yake kufariki Dunia mnamo mwaka 1903,Alikwenda huko ili atafute nafasi ya masomo ktk chuo cha Sanaa cha Vienna na Chuo cha Ujenzi lakini kwa bahati alikataliwa kutokana na kukosa Sifa .Baada ya kushindwa kujiunga na vyuo hivyo Alipenda sana Siasa na kuanza kuzifuatilia kwa karibu ndipo ndoto za kuwa Kiongozi Wa Taifa la Ujerumani zilianza kumjia .

Historia inaonyesha Adolf Hitler ktk vita Ya kwanza ya Dunia alikuwa ni mpiganaji Wa kujitolea ktk jeshi la Ujerumani na hatimaye alipata nafasi ya UKopuro na baadaye alibahatika kupata zawadi ya mkimbiaji bora vitani na akapewa nafasi ya mjumbe wa mawasiliano jeshini .Hapo ndipo ilianza safari yake ya kupelekea uzoefu kamili jeshini na kuanza kuibukia ktk majukwaa na mikutano ya Kisiasa .Endelea kufuatilia bila kuchoka Historia hii fupi ya Dikteta huyu maarufu Duniani.

Adolf Hitler Aliibuka na kuwa miongoni mwa Madikteta wenye nguvu na umaarufu mkubwa sana Duniani ktk karne ya 20.Baada ya vita vya kwanza vya Dunia Adolf Hitler aliibuka na kuwa kiongozi mkuu Wa Serikali Ya Ujerumani kupitia chama cha National Socialist German Workers Party mnamo mwaka 1933.Kupitia kuanzisha kwake kwa makambi ya Mauaji pamoja na mateso dhidi ya watu wasiokuwa Wajerumani hasahasa akiwalenga na kuwaua Wayahudi Takribani 6000000(Milioni sita) kulimfanya aonekane kuwa ni mbaguzi Wa Rangi .Haya yalikuwa ni Mauaji ya Halaiki yasiyoweza kusahaulika ktk Historia ya Dunia.

Jitihada na chokochoko zake zilisabanisha kuivamia kijeshi nchi ya Poland mnamo 1939 na Hatimaye vita ya pili ya Dunia ilitokea .Hadi mwaka 1941 Ujerumani ilikuwa inashikilia sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Afrika .

Kabla ya kuwa Kiongozi Wa Taifa la Ujerumani Historia inaoonyesha alikuwa ni mwanajeshi Wa kawaida kabisa jeshini .Kuna muda Aliwahi Toroka mafunzo ya kijeshi jeshini huko Austria -Hungary mnamo mwaka 1913 lakini alirudishwa kwa nguvu.Baada ya muda alianza tena kujitolea ktk jeshi la Balvaria na hatimaye mwaka 1914 alingia vitani huku akiwa askari Wa Kikosi kilichokuwa mstari Wa mbele upande Wa magharibi mwa nchi.Mwaka 1918 Hitler alipata ulemavu wa macho baada ya Gesi kumpata usoni .Wakati majeshi ya Ujerumani ikisalimu Amri Hitler alikuwa yupo Hospitalini na Aliporudi Nchini Ujerumani alikuta Uchumi umeyumba vibaya huku Wajerumani wakikosa matumaini kabisa .Uzoefu alioupata ktk mapigano ulimuathiri sana vibaya kiwango cha muda mwingi ktk maisha yake alikuwa akiwaza na kupenda vita .

Mwaka 1919 Adolf Hitler aliudhuria mkutano Wa kwanza Wa chama cha kijamaa cha Wafanyakazi na mkutano wa Kundi la wazarendo Wa Ujerumani ,Ktk mikutano hii Hitler aliudhuria kama jasusi Wa Jeshi.Baadaye alijikuta akikubaliana na Mawazo ya Anton Dlexler ambayo yalikuwa yakisisitiza Utaifa na Kupinga maonevu lakini hakukubaliana kwa namna ambavyo walikuwa wamejipanga kuyatekeleza Mawazo yao.Katika mkutano huo Adolf Hitler aliinuka na kupewa nafasi kisha kuanza kutoka hotuba iliyokuwa imejaa Upole na ukali ndani yake .Ktk Hotuba yake Hitler alieleza jinsi gani mkataba Wa Versailles ulivyokuwa unaiumiza nchi ya Ujerumani .

Ilifahamika wazi kuwa watu Wengi walianza kujiunga na chama hicho ili kumfuata Hitler na kusikiliza hotuba zake ambazo zilijaa ushawishi ,Elimu na Hamasa kubwa kwa Wajerumani wengi .Wajerumani baada ya kusikiliza hotuba zake walikuwa wapo Tayari kufanya jambo lolote ikiwa wangeamriwa.

Ikumbukwe Adolf Hitler baada ya vita vya kwanza vya Dunia alibaki hana kazi yeyote .Huu ndio ulikuwa muda wake Muafaka Wa kutekeleza ndoto na Malengo yake kwa Taifa la Ujerumani.Akiwa Mitaani na wanajeshi wenzake waliokuwa wamerejea kutoka vitani lakinihawana kazi waliendelea na harakati zao za mapambano kwenye mitaa ya Ujerumani.Mwaka 1919 alibahatika kupata ajira mjini Munich inasadikika alikuwa na mahusiano mazuri na Ofisa mmoja Wa Kijeshi ajulikanaye kwa Jina la Ernst Roehm .Baadaye Hitler akawa mwanapropaganda mzuri jeshini na kuanza kwa nguvu kujihusisha na chama cha Wafanyakazi cha kijerumani .

Mnamo Septemba 1919 Adolf Hitler alianza kushiriki mikutano kibao ya Chama cha Wafanyakazi .Ktk mikutano hiyo alikuwa ni mzungumzaji Mwenye ushawishi mkubwa kutokana na propaganda zake .Hitler alikuwa ni bingwa Wa kujenga hoja ktk chama cha KiNAZI.Hoja za Hitler zilijikita zaidi ktk kuupigania Utaifa na kuchochea zaidi Ubaguzi Wa Rangi .Aliongeza sana ushawishi kwa watu na maelfu ya wanachama walijiunga na chama cha National Socialist German Workers Party (NSDAP) jina rasmi chama cha NAZI .
Kutokana na Hali ngumu ya Uchumi miaka iliyofuata ilichangia kwa Kiwango kikubwa kukua kwa chama hicho .Hadi Mwishoni mwa mwaka 1923 idadi ya wanachama Wa chama cha NAZI walikuwa wamefikia 56000 hao ni yeye tu aliokuwa amewaongeza Ktk chama chake akawa maarufu sana ktk jeshi la Balvaria na Siasa za Ujerumani.Hitler alitumaini kuwa angetumia Udhaifu Wa Hali ngumu ya Kiuchumi kuipindua Serikali ya Mjini Berlin.Kwa dhamira ya dhati kabisa ya Kuipindua Serikali alianzisha maandamano na Fujo mnamo Novemba 8-9 1923 huku akitumaini kabisa kuwa Serikali ya Ushirika ya Balvaria ingeshirikiana naye kuipindua Serikali ya Berlin .Jaribio hili la kuipindua Serikali Ya Berlin lilishindikana.Najua una shauku kubwa kujua nini Kilifuata ,,Usichoke kufuatilia.

Baada ya jaribio hili la mapinduzi Adolf Hitler alishitakiwa kwa Makosa ya Uhaini dhidi ya Serikali ya Ujerumani kisha akahukumiwa kifungo Cha Kwenda Gerezani ktk Mji Wa Ngome Ya Zamani ya Landsberg .Kipindi ambacho Adolf Hitler yupo Gerezani Mawazo yake Ya mikakati na mbinu yalikua kwa kiwango kikubwa sana Nchini Ujerumani.Adolf Hitler alifanikiwa kuandika kitabu chake kijulikanacho kama MEIN KAMPF ktk kitabu hicho aliorezesha Mipango na Imani.

Adolf Hitler alifanikisha kuandikwa kwa kitabu chake hicho kwa kumtajia maneno na kisha kuandika mwandishi mmoja aliyemuamini sana ajulikanaye kwa jina la RUDOF HESS ambaye aliishi kati ya mwaka 1894 -1987 . Mipango na Imani hizo zililenga hasa ktk Kukiunda upya chama cha Kijamaa na Wafanyakazi .Mara kadhaa Akiwa Gerezani alifanya jitihada nyingi zilizolenga kukata rufaa dhidi ya Hukumu ya kifungo Gerezani.

Baadaye Hitler aliachiwa Huru ,Mara baada ya kuachiwa huru alizirejea Siasa zake kisha kuanza kurejesha ushawishi wake ktk chama cha NAZI .

Baada ya mapinduzi ya Serikali kushindwa mnamo mwaka 1923 alikamatwa na kutiwa jela ambapo baada ya Kutoka jela aliendelea kukijenga chama chake ili kije kishike madaraka kwa njia ya Kisheria (Legal means) .

Aliamini kuna majira yangekuja angeanza kuijenga ujerumani mpya kwa misingi ya Rangi (Ubaguzi Wa rangi) ambapo angeongeza ukubwa Wa Ujerumani kwa kuvamia na kutawala maeneo mbalimbali Ya Dunia.

Aliamini Kwamba Ujerumani ni lazima ipigane vita vingi ili ikalie Eneo kubwa la Ardhi na Wajerumani waendeshe shughuli mbalimbali za Kilimo na viwanda .Vita ndogo na rahisi ilipiganwa dhidi ya nchi ya Czechoslovakia ,ikifuatiwa na vita kubwa dhidi ya Ufaransa na Uingereza na vita ya Tatu ambayo ingefuata ambayo ilitegemewa ingekuwa rahisi na haraka ni zidi ya Muungano Wa Jumuiya ya Kisovieti (Urusi) ambapo Ujerumani ingepata malighafi nyingi Hususani mafuta na Vita ya Nne na ya mwisho iliyopangwa na Adolf Hitler ilikuwa ni dhidi ya Taifa la Marekani.

Mipango hii ya vita ingeweza kufanikiwa ikiwa Ujerumani ungekuwa na Ndege vita na Meli za kivita zenye Uwezo Wa kushambulia kwa masafa.
Safari yake ya kuingia Serikalini na kutimiza azima na mipango ya Kuiteka Dunia iliendelea kubaki kichwani mwake .Miaka ya 1930 Dunia ikiwa katika Mvurugiko Wa Kiuchumi Adolf Hitler alianza kushamiri na kuwa mtu maarufu Sana ktk Siasa Za Ujerumani kama ambavyo awali nimeelezea .Katika Uchaguzi Wa Septemba 1930 Chama cha NAZI kilipata takribani Kura 6500000

Hatimaye kuwa na Umaarufu usio na shaka ktk Siasa za Ujerumani.Mwezi Novemba 1932 Rais Wa Ujerumani mh.Paul Von Hindenburg aliyeishi kuanzia mwaka 1847-1934 alimuita Adolf Hitler kisha kumfanya Awe Kansela ili kuiongoza Serikali Ya Muungano ya KiNAZI ,Watu wazalendo na watu mbalimbali huru na maarufu .

Kwa miaka miwili ya Mwanzo Adolf Hitler alionyesha heshima kubwa ktk kutoingilia mihimili mingine Yaani Mahakama na Bunge .Kutokana na wadhifa muhimu ktk Serikali ya Kijeshi ya chama cha NAZI ,Hitler alianza kumtumia aliyekuwa Rafiki yake na waziri wa Ulinzi ambaye alijulikana kwa Jina la Werner Von Blomberg ,Taratibu Hitler alianza kuiongoza Wizara hiyo .Adolf Hitler alianza kuwaondoa mahasimu wake Wa Kisiasa huku Akihakikisha Ngazi zote za kiserikali na Taasisi kuu Za Kisiasa zipo chini ya Udhibiti wake .Kufuatia kifo cha Rais Hindenburg Mwezi Oktoba 1934 basi ikawa ndio Yake rahisi ya Kufuta cheo cha Urais ,Hatimaye rasmi Adolf Hitler akawa Kiongozi Mkuu Wa Serikali ya Ujerumani na Amiri Jeshi Mkuu Wa Majeshi ya Ujerumani .

Baada ya Muda alimteua Joseph Goebells kuwa Mkuu Wa kitengo cha propaganda aliyezaliwa mwaka 1887 na kufariki Dunia mwaka 1945 pia alimteua Heinrich Himmler kuwa Mkuu Wa Polisi Wa Ujerumani .Utawala Wa Adolf Hitler ulionekana kuwa na mvuto mkubwa baada ya mamilioni ya Watu Wa Ujerumani kuandamana huku wakimshangilia mnamo mwaka 1934 .

Baada ya kuhakikisha nchi ya Ujerumani imedhibitiwa vilivyo alianza kuhamasisha maliasili za Wajerumani zitumike kwa ajili ya uvamizi ktk mataifa jirani na Kuhakikisha Ubaguzi Wa Rangi unatawala Upande wa katikati na Mashariki mwa Ulaya .Aliwaandaa watu waliokuwa hawana kazi takribani 6000000 ili wafanye kazi kwa ajili ya maandalizi ya Vita .Kutokana na propaganda za kikatili Hitler aliwaua wayahudi wengi ambapo alidai wao ni sababu ya matatizo ya Ndani na nje ya Ujerumani.Kitu kinachoogopesha na kutisha ni kwamba Hitler alitoa amri wayahudi waliokuwa watoto ,wanaume na wanawake wachomwe moto kwenye matanuri yaliyokuwa yameandaliwa kwenye makambi maalumu yaliyokuwa chini ya udhibiti Wa Himmler .Mahusiano ya kigeni zaidi yalijikita ktk maandalizi ya vita .Kutokana na Jeshi la Ujerumani kuboreshwa na kuwa na nguvu pia kupata washirika Wa mataifa mengine ndio Ikawa hatua muhimu sana ya maandalizi ya vita kama vilivyokuwa ndoto zake tangu mwanzo yaani kuiteka Ulaya na Dunia yote .Hitler alivamia na kudhibiti Czechoslovakia ,Austria mnamo mwaka 1939 .

Hatimaye ,kupitia ahadi na vitisho chake alianza kujipenyeza na kutaka kuvamia Uliokuwa Muungano Wa Kisovieti ambao ulikuwa ukiundwa na Urusi na vinchi vidogovidogo .

Ujerumani ilipata Muungano Wa Kijeshi Wa Taifa la Japan na Italia .Muungano huu ulikuwa muhimu sana kuelekea maandalizi ya Vita.
Mnamo Septemba 1,1939 Adolf Hitler alianzisha vita Ya Pili ya Dunia kwa kuivamia kijeshi nchi ya Poland lengo lake hasa aitawale Ulaya Yote .Uvamizi huu Wa ghafla dhidi ya Poland ulienda sambamba na maangamizi makubwa ya Wayahudi wakati huo na wasomi wengi Wa Poland waliuawa vibaya na hatimaye Eneo la Poland Likawa chini ya Utawala Wa Kikoloni Wa Kijerumani.

Baada ya Uvamizi huo Wa Adolf Hitler Uingereza na Ufaransa walitangaza vita zidi ya Ujerumani. Mara tu baada ya tangazo hili la Vita majeshi ya Hitler yaligeuzia Silaha za kivita upande Wa magharibi mwa Ulaya na Hatimaye kuvamia na kuua vibaya pamoja na kuleta athari mbalimbali.Baada ya mashambulizi makali mnamo Aprili 1940 Nchi ya Denmark ilijisalimisha kwa Ujerumani na baadaye nchi ya Norway ilifuatia .Mwezi Mei na Juni Majeshi ya Hitler yalisonga mbele huku yakiwa yamejihami vilivyo kwa Vifaru na Ndege za kivita hatimaye nchi ya Ufaransa na nchi nyingine ndogondogo zilizopo karibu Zilipigwa Vibaya .

Kutokana na Uimara Wa jeshi la Anga la Uingereza na Ufaransa, majeshi ya Ujerumani yaliondolewa kwa nguvu na Hatimaye Hitler aliamuru kurudishwa nyuma jeshi lake ili lijipange vizuri zaidi .
Mengi kubwa la Hitler lilikuwa ni Kuvamia Eneo lote la Mashariki ili kurahisisha harakati zake za Kuiteka Ulaya .Mnamo Juni 22,1941 jeshi la Ujerumani lilisonga mbele zaidi ktk Operesheni yake ijulikanayo kama BARBARROSSA ,Ambayo Hitler alidai kwamba hii Ni Opesheni ya Harakati za Mwisho za Kuendelea kuishi na Kuwepo ktk Dunia .Ingawaje majeshi ya Adolf Hitler yalisonga mbele kwa haraka sana lakini hayakufanikiwa kutimiza malengo makuu Matatu kwani Majeshi ya Urusi yaliwazuia kusonga mbele zaidi .Malengo makuu matatu ya majeshi ya Hitler yalikuwa ni kufikia Miji mikubwa mitatu ambayo ni :MOSCOW,LENINGRAD na STALINGRA.

Miaka iliyofuata Nguvu ya jeshi la Adolf Hitler ilizidi kushuka Tofauti na matarajio na kikwazo kikubwa ilikuwa ni namna ya Kuvamia na kuchukua mji Wa STALINGRAD mwaka 1943 .Mwaka uliofuata majeshi ya Muungano Wa Uingereza, Marekani, Ufaransa na Urusi yaliendelea kusonga mbele mpaka ndani ya Makao Makuu Ya Serikali ya chama cha NAZI iliyokuwa chini ya Dikteta Adolf Hitler.
.
SABABU ZA KWANINI ADOLF HITLER ALIIBUKA NA KUWA DIKTETA WA UJERUMANI
(1)Vita vya kwanza vya Dunia
Sababu kubwa kabisa iliyomuibua Adolf Hitler ni vita vya kwanza vya Dunia ambapo yeye binafsi alishiriki kama mpiganaji Wa kawaida .Vita hivi vilisababisha Ujerumani ikaharibiwa vibaya sana kwani madaraja ,Viwanda, Barabara ,Mashamba ,majengo ,viwanja vya Ndege vilibomolewa vibaya sana .Ujerumani kwa sehemu kubwa ilibaki kuwa magofu na mamilioni ya wajerumani waliuawa huku mamilioni wakiwa wakimbizi kwenye mataifa ya Ulaya .Hali hii limkasirisha sana Hitler baada ya Vita na kuanza mipango na mikakati ya kuwa Kiongozi Wa Taifa hilo ambapo mnamo mwaka 1933 alichaguliwa kama kansela (Kiongozi Mkuu ) na Hatimaye kuigeuza katiba na kujitangazia kuwa yeye ni Kiongozi Wa kudumu na milele Wa Ujerumani .Hii ina maana Hitler alipochaguliwa Kidemokrasia baadaye allibukia kuwa Dikteta au mtawala Wa Kiimla .

(2)Kuporomoka kwa uchumi Wa Dunia mnamo mwaka 1929-1933
Baada ya vita vya kwanza vya Dunia Uchumi Wa Dunia uliyumba sana kiwango chakutishia maisha ya watu wengi .Uchumi uliporomoka kutokana na Vita kuchukua muda mrefu mpaka kuisha hivyo uzalishaji viwandani na mashambani ulisimama .Ujerumani ni moja ya mataifa ya Ulaya yaliyoathirika vibaya kutokana na mdororo huu Wa uchumi .Ikumbukwe Ujerumani ilikuwa Ina deni kubwa sana la kulipa mataifa mbalimbali kama fidia kutokana na Uharibifu Wa kivita uliojitokeza .Katika mkataba Wa VERSAILLES Ujerumani ilipaswa ilipe Takribani Paundi 650,000000 .


Hili lilikuwa deni kubwa sana na Serikali ya Ujerumani chini ya Kansela Kurt Von Schleicher ilikuwa imekwishaanza kulipa .Adolf Hitler wakati Wa kampeni za uchaguzi mwaka 1933 aliwaambia wajerumani kwamba akichaguliwa kuwa Kansela angevunja mkataba huo na hatimaye Alichaguliwa kuwa Kansela na kuanza kufuta mipango yote ya kulipa fidia .Wajerumani walimtazama Adolf Hitler kama Mkombozi wao .
(3)Mkataba Wa Versailles mwaka 1919

Kama nilivyoeleza awali kwamba mkataba huu Wa VERSAILLES ulichukuliwa na Adolf Hitler pamoja na Wajerumani wengi kuwa ni mkataba uliokuwa umejikita zaidi kulinyanyapaa Taifa la Ujerumani kama muanzilishi Wa vita vya kwabza vya Dunia .Kwa mujibu Wa mkataba huu Ujerumani ilipaswa kulipa Takribani Paundi 650,000000 kama fidia Kutokana na Uharibifu uliotokana na vita vya kwanza vya Dunia vilivyodumu kuanzia mwaka 1914 -1918, pili ,Tatu,Ujerumani ilinyang'anywa makoloni yake yote Barani Afrika ikiwemo Tanganyika ,Namibia n.k , Nne,Ujerumani ilipaswa ipunguze ukubwa Wa jeshi lake hadi kufikia Takribani wanajeshi 100000,Tano ,Ujerumani ilipaswa kumiliki manowari Sita tu za kivita siyo zaidi ya hapo n.k .Makubaliano haya ktk mkataba huu Wa VERSAILLES yaliumiza sana Ujerumani kiwango cha kuanza kufurukuta ili ijinusuru na mkataba huu .Wajerumani walipoona Adolf Hitler anatamaa na Shauku ya kutaka Ujerumani iondokane na Mkataba huu walinuia na kumchagua rasmi kuwa Kansela Wa Ujerumani .

(4)Udhaifu Wa Katiba na Serikali ya Ujerumani iliyokuwepo madarakani .
Katiba na Serikali ya Ujerumani ilikuwa dhaifu sana kiwango hata kutoa upenyo na Adolf Hitler kuingia madarakani na kuibuka kuwa Dikteta Wa Kutisha .
(5)Akili na ushawishi Wa Hitler kwa Wajerumani.

Adolf Hitler alikuwa ni mtu Mwenye akili kubwa sana na kitu kilichombeba sana alikuwa ni mzungumzaji Mwenye mvuto na ushawishi mkubwa pindi anapopanda jukwaani .Hitler anapojieleza au kulielezea jambo Fulani alijawa hisia sana huku akiuvaa uhusika kamili Wa jambo hilo au akionyesha kuguswa sana na jambo hilo ndio maana wataalamu Wa Historia wanaona hii ni moja ya sababu iliyomfanya Achaguliwa na kuibuka rasmi kuwa Kansela Wa Ujerumani .Baada ya kuwa Kansela aliibuka na kuwa mtawala Wa Kidikteta.

MATOKEO YA UTAWALA WA HITLER NCHINI UJERUMANI ,ULAYA NA DUNIANI KOTE
Kutokana na utawala Wa kiimla Wa Dikteta Adolf Hitler yapo mambo Hasi na chanya ambayo yalitokea Nchini ujerumani ,Ulaya na Duniani kote .Yafuatayo ni mambo chanya au yafaida yaliyotokana na utawala Wa Adolf Hitler nchini Ujerumani ,,
(1)Ujerumani ilipata Maendeleo makubwa ya kijeshi .

Kwanza kabisa azima na Lengo la Adolf Hitler lilikuwa ni Kuvamia na kuchukua Udhibiti wa Maeneo mbalimbali ya Dunia na kuyafanya kuwa makoloni yake.Mkataba Wa Versailles 1919 ulitamka kwamba Ujerumani inapaswa kuwa na idadi ya wanajeshi wasiozidi 100000 lakini Mara baada ya Kuingia madarakani Dikteta Adolf Hitler hadi mwaka 1934 kulikuwa na wanajeshi 4,500,000.Mwaka 1935 jeshi lilipata idhini ya kutoa mafunzo kwa vijana takribani 300,000.Hadi mwaka 1939 wakati Ujerumani inaivamia Kijeshi nchi ya Poland ilikuwa na Wanajeshi 1500000 ambao walikuwa wapo Tayari kwa vita ukiachana na waliokuwepo akiba.

(2)Ujerumani ilipata Maendeleo makubwa Ya Viwanda .
Ukiachana na Sera za Kijeshi za Hitler pia alijikita ktk Sera ya Viwanda.Wakati Wa Utawala Wa Adolf Hitler Viwanda vingi vilijengwa ili kuharakisha azima na Mengi la Hitler kuifanya Ujerumaniinayoongoza kiuchumi na Kijeshi Barani Ulaya na Duniani kote.

(2)Utawala Wa Adolf Hitler Ulitatua tatizo la mdororo Wa uchumi
Uchumi Wa Ujerumani alianza kukua kwa kasi ya ajabu .Kusinyaa kwa uchumi kulikotokana na vita vya kwanza vya Dunia kulianza kuwa historia kutokana na Maono makubwa ya Adolf Hitler kuifanya Ujerumani yenye nguvu kiuchumi na Kijeshi .Viwanda vilifanya kazi ya uzalishaji usiku kucha na mchana .Wakulima walifanya kazi kubwa ya uzalishaji ili kuilisha idadi kubwa ya Wajerumani ambao walikuwa wakiongezeka kwa kasi ya ajabu ingawaje watu wengi walikufa ikiwa ni matokeo ya vita vya kwanza vya Dunia vilivyodumu kuanzia 1914-1918.

(3)Maendeleo makubwa Ya Sayansi na Teknolojia .
Wakati Wa Utawala Wa Adolf Hitler Ujerumani iliendelea sana ktk Sayansi na Teknolojia mfano Sayansi na Teknolojia ktk Uvumbuzi Wa madawa ya Tiba na Kilimo ,Uvumbuzi na Ujenzi Wa Magari aina ya Volkswagen ,Ujenzi wa makombora ya kuvuka Bara kwenye miaka ya 1940 n.k
(4)Tatizo la Ajira lilitatuliwa kwa Kiwango Kikubwa kwani Miradi mikubwa ya Maendeleo ilianzishwa.Mara baada ya kuingia madarakani na kuwa Mtawala Mwenye madaraka kamili Hitler alihamasisha Ujenzi Wa Miradi mikubwa ya Barabara ,Reli ,Viwanja vya Ndege ,Ujenzi Wa viwanda ,Nafasi nyingi za kazi jeshini zilitengenezwa n.k.Vijana wengi walipata ajira kupitia miradi hiyo na Nafasi za jeshi .Tatizo la Ukosefu Wa ajira lilipungua Kwa kiasi kikubwa Tofauti na awali baada ya vita vya kwanza vya Dunia .

Mfano Kabla ya Ufunguzi na Ubunifu Wa miradi mbalimbali ya Maendeleo tatizo la ajira nchini Ujerumani lilikuwa ni 8.5% mwaka 1929, 14% Mwaka 1930, 21.9% mwaka 1931 hadi kilele cha 29.9% mwaka 1932 .Kati ya mwaka 1933-1937 Adolf Hitler aliajiri vijana takribani milioni 5 kwenye miradi mbalimbali likiwemo jeshi hii ilipunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la Ajira.Awali vijana takribani Milioni 6 walikuwa hawana Ajira hii maana ake vijana waliokosa ajira hadi mwaka 1937 walikuwa takribani milioni 1 Tofauti na hapo awali .

(5)Maendeleo makubwa ktk Sekta Ya Elimu.Shule na vyuo vingi vilijengwa wakati Wa Utawala Wa Dikteta Adolf Hitler. wanafunzi Wa ngazi zote walifundishwa itikadi ya chama cha NAZI na Utaifa .Mitaala ilikuwa ikielezea ujenzi Wa Ujerumani mpya yenye nguvu Kijeshi na kiuchumi bila kusahau Itikadi ya chama cha NAZI.

(6)Ujerumani iliendelea kwa Kasi kubwa ktk Sekta Ya Miundo mbinu Kama Viwanja vya Ndege,Barabara ,Reli ,Madaraja makubwa .Kwa kiwango kikubwa Miundo mbinu hii ilijengwa kwa kutumia jeshi .Adolf Hitler alikuwa akitoa amri na muda Wa kukamilisha miradi ambayo aliona ingekuwa na manufaa kwa Taifa lake.

(7)Wafanyakazi waliboreshewa Hali zao .Hakukuwa na migomo ya Wafanyakazi kama ilivyokuwa awali .Hitler alikuwa akiwajali sana Wafanyakazi Wa Ujerumani ambao walikuwa wapo tayari kulijenga Taifa ili liwe na nguvu kubwa kiuchumi ,Kisiasa na Kijeshi.

(8)Maendeleo makubwa ktk Ujenzi wa Silaha .Adolf Hitler alijikita sana kwenye utengenezaji Wa Silaha kama Mabomu ,Bunduki ,Vifaru ,Mizinga ,Ujenzi Wa Meli za Kivita ,Utengenezaji wa Ndege Vita n.k .mfano hadi mwaka 1940 Ujerumani ilikuwa na Vifaru vya Kijeshi Takribani 2500
Nje ya kuwepo matokeo chanya ya Utawala Wa Adolf Hitler pia upande Wa pili Wa shilingi ulibeba mambo yafuatayo ,

(1)Wayahudi wengi waliuawa kutokana na Amri za Adolf Hitler.
Kabla ya kuibuka kwa Utawala Wa Adolf Hitler mnamo mwaka 1933 nchini Ujerumani wayahudi waliishi maisha mazuri sana ingawaje changamoto ndogondogo zilikuwepo .Baada ya kuingia mamlakani Kwa Hitler wayahudi walianza kuishi maisha ya mashaka kutokana na ubaguzi Wa wazi uliokuwa unafanywa na Utawala Wa Adolf Hitler. Katika Utawala Wa Adolf Hitler wayahudi walichukuliwa kuwa ni wasaliti na ndio maana Ujerumani ilishindwa ktk vita vya kwanza vya Dunia. Hitler aliwachukia sana wayahudi na kuanza kuandaa mipango ya Kutengeneza makambi rasmi kwa ajili ya kutekeleza Mauaji ya wayahudi .Inasadikika Wayahudi wapatao 6000000(Milioni 6) waliuawa kwenye matanuri ya moto na makambi rasmi yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya Mauaji ya wayahudi .Kiujumla yalikuwa ni Mauaji ya Halaiki ya Wayahudi (Watu kutoka Nchini Israel).

(2)Utawala Wa Adolf Hitler uliitumbukiza Dunia Kwenye vita vya pili vya Dunia.
Pamoja na Jitihada zote za kimataifa kuinusuru Dunia kuingia kwenye vita vingine vya Dunia ktk mkataba Wa Versailles mwaka 1919 kuibuka kwa utawala Wa Kiimla Nchini Ujerumani chini ya Adolf Hitler kuliitumbukiza Dunia ktk vita vingine vya pili. Utawala Wa Adolf Hitler ulikuwa ni wachokochoko ,kibabe ,Kishari na Fujo Barani ndani ya Ujerumani, Ulaya na Duniani kote .Hitler aliamini sana ktk Matumizi makubwa ya jeshi na Silaha nzito Kiujumla .Alipenda na kiu yake kubwa ilikuwa ni kuiweka Dunia yote chini ya Himaya yake .Mwaka 1939 alipanga mipango na mikakati kisha akaivamia kijeshi nchi ya Poland ndipo vita vya pili vya Dunia vilipozuka na kuenea kwa kasi kwani washirika Wa Poland ambao ni Uingereza ,Ufaransa ,ubelgiji n.k
hawakuridhishwa na kitendo hicho .
(3)Hitler alikuwa akitoa amri za kuuawa kwa Mashoga ,Wezi ,wauaji ,vibaka ,Walawiti ,majambazi n.k .Hitler aliwachukia sana watu Wa namna hiyo .

(4)Ktk Utawala Wa Adolf Hitler watoto walipewa jukumu na kazi ya kuripoti au kutoa Taarifa za wazazi wao ambao walikuwa wanauchukia na kuukosoa Utawala wake .Wazazi Wengi waliteswa,waliwekwa vizuizini na hata kuuawa kinyama .Jukumu la kuwaua ,kuwatesa wazazi hao walipewa watoto wao na kama wakigoma kutekeleza Adhabu hizo watoto ndio walibeba Adhabu hizo kwa niaba ya wazazi wao.Kiujumla ulikuwa ni Utawala mbaya Kwa wajerumani na watu wengine.

(5)Watu wenye magonjwa ya akili wapatao 72000 waliuliwa kati ya mwaka 1939-1941 huku Viwete wapatao 300000 wanawake na wanaume walipewa ugumba na Utasa ili wasibebe ujauzito au kutia wanawake ujauzito ilikuwa ni kati ya Mwaka 1934-1945.Adolf Hitler hakuwapenda na kuwajali watu wenye ulemavu Wa aina yeyote binafsi aliamini watu hao ni laana na mzigo kwa Taifa la Ujerumani .
(5)Vyama Vyote vya Wafanyakazi kwenye Utawala Wa Adolf Hitler vilifutiliwa mbali .

Mara baada ya Adolf Hitler kuingia rasmi mamlakani alianza zoezi la kuvifutilia mbali vyama vya kutetea masirahi ya Wafanyakazi. Hitler alitangaza vyama hivyo kuwa ni Haramu na kuwa havitakiwi kujihusisha na shughuli zozote mnamo Mei 2 ,1933. Kufuatia tangazo hilo Ofisi za vyama hivyo zilifungwa huku Akaunti za Benki zikifilisiwa .Viongozi Wa vyama vya Wafanyakazi wengi waliuawa ,waliteswa na hata kutiwa jela bila kufunguliwa mashitaka .Kutokana na hatua hiyo Wafanyakazi walikosa sauti ya kusemea mahitaji na matatizo yao .Hitler alifuta vyama vya Wafanyakazi akihofia kupinduliwa na vyama hivyo.Mfano Wa viongozi Wa vyama vya Wafanyakazi waliouawa ni Max Haberman

(6)Katika Utawala Wa Adolf Hitler wanawake walikuwa Wakibaguliwa kwenye nafasi za ajira .
Baada ya kuingia rasmi madarakani Dikteta Adolf Hitler aliamuru madaktari ,Mainjinia ,walimu ,Wahadhiri na watumishi Wa umma waliokuwa Wa jinsia ya kike kuacha kazi Mara moja na kujikita ktk kazi za malezi majumbani .Wanaharakati Wa wanawake waliojitokeza na kuanza kupigania haki za wanawake waliuawa na wengine walifungwa jela bila kufunguliwa mashitaka .Mfano Wa wanaharakati Wa kijinsia waliouawa ni Rosa Manus ,n.k.

(7)Vyama vya kisiasa vilifutwa huku wapinzani Wa utawala wake wakiuliwa ,wakiteswa ,wakiwekwa magerezani n.k .Wanasiasa wengi walikimbilia nchi za Nje wakihofia kuchinjwa .Vyama vya Siasa vilitangazwa kuwa ni adui mkubwa Wa Serikali yake ya chini ya chama cha KiNAZI. Mifano ya wanasiasa waliouawa Fritz Elsas ,Wilhelm Leuschner,Ludwig Landmann,Ernst Schneller,Joseph Roth n.k .

(8)Shughuli zote za kidini zilitangazwa kuwa ni Haramu nchini Ujerumani. ilikuwa ni Marufuku kufanya ibada kwenye Makanisa na Misikiti wala popote .Ukikamatwa unaeneza Dini popote Adhabu yake ilikuwa ni kifo au kifungo gerezani .Wachungaji wengi Wa Kiprotestanti (Kilokole) waliuawa kikatili .Mfano Wa wachungaji na viongozi wa Dini wengine alikuwa anaitwa Dietrich Bonhoffer ,Edith Stein ,Friedrich Lorenz ,Regina Jonas ,Paul Schneider,Joachen Kepper ,Yitzchak Shimon Gottlieb,Stefan Wincenty Frelichowski,Maximilian Kolbe ,Maria Skobtisova n.k

(9)Ukoministi ulikuwa ni Haramu ktk Utawala Wa Adolf Hitler.
Ukoministi /ujamaa ktk Kipindi cha Utawala Wa Dikteta Adolf Hitler ulikuwa ni Haramu .Hitler aliuchukia sana Ukoministi na yeyote aliyekuwa ni mfuasi Wa Ukoministi aliuawa kwa kunyongwa au Kutiwa gerezani bila kufunguliwa mashitaka yeyote .Wakati anaingia mamlakani mwaka 1933 alionekana kuuchukia sana ukoministi binafsi alikuwa ni mfuasi Wa Sera ya Kibepari .Hitler pia aliwachukia sana warusi na aliona kuwa ni maadui makubwa Wa Taifa la Ujerumani.mifano ya Wakoministi waliouawa huku wakitetea Ukoministi nchini Ujerumani ni kama Franz Jacob,Walter Kramer ,Albert Kuntz ,Walter Moller ,August Lutgens ,Judith Auer ,Friedrich Aue,Edgar Andre ,Hans coppi ,Hilde Coppi n.k

(10)Utawala Wa Kidikteta Wa Adolf Hitler ulipelekea kuibuka kwa Madikteta Barani Afrika .
Utawala Wa kiimla Wa Adolf Hitler ulisababisha baadhi ya Viongozi Wa Kiafrika kuibuka na Kuiga Udikteta na kufanya matendo yaliyokosa Ubinadamu kwani kulikuwa na Ukiukaji mkubwa Wa Haki za Binadamu. Mfano Wa Madikteta Wa Afrika walioibuka na Kuiga Utawala Wa Adolf Hitler ni Dikteta Iddi Amin Dada Wa Uganda (1971-1979).

MWISHO WA UTAWALA WA HITLER NCHINI UJERUMANI
Unaweza ukajawa na maswali mengi sana moja wapo ni hili ,Je ,Utawala Wa Dikteta Adolf Hitler Uliishieje?
Utawala Wa Adolf Hitler ulijiondoa wenyewe kwa kujichimbia kaburi lake kwa kuwa siku zote Sera za Kidikteta za Hitler zilikuwa zikiandaa kifo cha Serikali yake .Harakati za kuangusha Utawala Wa Adolf Hitler Zilianza kwa kasi ya ajabu ktk vita vya pili vya Dunia Kama nilivyoeleza awali .Hapo Awali ktk utangulizi nilielezea namna ambavyo vikosi vya Majeshi Ya Muungano Wa Uingereza ,Ufaransa,Marekani na Urusi vilivyoingia Mjini Berlin na kuuteka mji huo.

Vikosi vya Majeshi ya Urusi,Marekani, Ufaransa na Uingereza Vilipouzingira mji Wa Berlin Hitler Alisalia kutoa Amri zisizotekelezeka Wakati huo washauri wake walikuwa wakimashauri ajisalimishe Mara Moja lakini alikataa.Kutokana na ndoto ya Hitler ya kuangamiza vikosi vya Maadui ,Watoto kwa wazee walihamasishwa kupigana vita ktk mstari Wa Mbele .Vikosi vya Jeshi lake vilipoona vinazidiwa na vikosi vya maadui baadhi ya wanasiasa na makamanda wake Wa jeshi walijaribu kumuua mnamo Julai 20,1944 lakini ilishindikana.Utawala Wa Adolf Hitler ulizidi kubanwa na kuwa matatani zaidi .

Katika siku za mwisho za Utawala Wa chama cha NAZI ,Majeshi ya Urusi yakiwa ktk Viunga vya mji Wa Berlin ,Hitler aliingia kwenye handaki na kutoa Amri kwa vikosi vyake ili viharibu handaki hilo kwani alikuwa ktk mfadhaiko mkubwa sana na mwisho Wa maisha yake alikuwa amekwishaanza kuuona.
Adolf Hitler aliamua kujiua mwenyewe Mnamo Aprili 30,1945 baada ya kuona Vikosi vya mahasimu wake vinakaribia kumtia nguvuni .Hitler Aliacha Historia ya kutisha Duniani ambayo haiwezi sahaulika ktk nchi ya Ujerumani, Barani Ulaya na Duniani kote .Hitler aliacha makovu Mioyoni mwa Wayahudi na kamwe hawawezi kumsahau mpaka Miisho ya Dunia.

MAREJEO
Browning ,Christopher R.(2004) The Origins of Final Solutions:The Evolution of NAZI Jewish policy ,September 1939-March 1942 .Comprehensive History of the Holocaust .Lincoln:University of Nebraska Press.
ISBN.0-8032-1327-1
Evans ,Richard J.(2003).The Coming of third Reich .New York:penguin Group .
ISBN.978-0-14-303469-8.
Evans,Richard J.(2005).The third Reich in power.New York : Penguin Group.
ISBN.978-0-14-303790-3.
Goblin,James Cross .The Life and death of Adolf Hitler .New York : Clarion Books 2002.
Kershaw,Ian.(2008).Hitler :Anb Biography .W.W.Norton and Company .
ISBN.978-0-393-05767-6.
Martin,Albert .Hitler .New York .Viking Kestrel ,1987.
Toland,John .Adolf Hitler .Garden City ,NY: Doubleday ,1976.
Zitelmann,Rainier.Hitler :The Policies of Seduction .London. London House



Credit: The Society States
 
Who winn, who write the history.....Mim mpaka izo vita zao za kwanza na pili siamni zile sabbu walizotuandikia ktk vitabu vya history kuwa ndzo ziliwafanya wadundane na kuita world war, kwahiyo hata hizo stori zao kwenye media kumuhusu Adolf ni uzushi na uongo mkubwa, mybe angekuwepo uyo itra angeweza jitetea kuwa hakuwa hiv wanavyomshutumu, or otherwise kama mtu mwenye akiki timamu, huwez kumjudge mtuhumiwa bila yeye kupata nafasi ya kujitetea.

achen kuamin uongo na ujinga, hayo mataifa yanayosema yalishinda izo vita hayo siku zote yamejawa hila na propagandas za kijinga kabisa, kwakuwa wale mabwana wayahudi feki waliadhibiwa vikari, na huyo bwana hitra kwenda kinyume na mipango ya awa beberu wenzie basi ndio kma hivyo tena, alichofanyiwa ndcho alifanyiwa idi amini kwa kusambaza taharifa za uzushi kumuhusu
 
Who winn, who write the history.....Mim mpaka izo vita zao za kwanza na pili siamni zile sabbu walizotuandikia ktk vitabu vya history kuwa ndzo ziliwafanya wadundane na kuita world war, kwahiyo hata hizo stori zao kwenye media kumuhusu Adolf ni uzushi na uongo mkubwa, mybe angekuwepo uyo itra angeweza jitetea kuwa hakuwa hiv wanavyomshutumu, or otherwise kama mtu mwenye akiki timamu, huwez kumjudge mtuhumiwa bila yeye kupata nafasi ya kujitetea.

achen kuamin uongo na ujinga, hayo mataifa yanayosema yalishinda izo vita hayo siku zote yamejawa hila na propagandas za kijinga kabisa, kwakuwa wale mabwana wayahudi feki waliadhibiwa vikari, na huyo bwana hitra kwenda kinyume na mipango ya awa beberu wenzie basi ndio kma hivyo tena, alichofanyiwa ndcho alifanyiwa idi amini kwa kusambaza taharifa za uzushi kumuhusu
Wanachokisema wamarekani kuhusu ubaya wa Hitler ndicho hicho wanachokisema wajerumani wenyewe. The guy devil and a half
 
Napenda akivyovaa, viatu virefu hadi magotini, kombati imechomekwa kwenye buti na jinsi ile mifuko ya pembeni ikivyotuna.
 
Je 'Wayahudi' waliofanyiwa mauaji ya kimbari katika simulizi yako, walikuwa ni wayahudi wa kimadhehebu ama walikuwa wayahudi wa kiutaifa?

Nimeuliza swali hili utupe ufafanuzi juu ya utata huu wa kihistoria.

Ukiangalia picha za wahanga wa mauaji hayo ni wazungu tena 'blonde' walionaswa nchi za Poland pamoja na nchi zingine jirani zilizovamiwa na kutekwa na Ujerumani.

Embu weka nyama kidogo kuiboresha simulizi yako mkuu.
 
Huu ndio ukweli wenyewe...... Stalin aliua warusi wengi kuliko hata majeshi ya Hitler !!! Ila kwakuwa alikua upande wa ushindi tumeaminishwa Hitler ndio ibilisi na mabeberu wengine wote ni malaika!!
Sio kweli ndugu mbona unatuongopea.yani Stalin auwe Warusi wengi kuliko Hitler?.ni uwongo uliopitiliza,hao watu alikuwa anawauwaje mpaka afanane na Hitler.Vita ya Germany na Urusi iliondoka na Warusi zaidi ya milion 8.stalin ajawahi kuuwa hata warusi laki 1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli ndugu mbona unatuongopea.yani Stalin auwe Warusi wengi kuliko Hitler?.ni uwongo uliopitiliza,hao watu alikuwa anawauwaje mpaka afanane na Hitler.Vita ya Germany na Urusi iliondoka na Warusi zaidi ya milion 8.stalin ajawahi kuuwa hata warusi laki 1

Sent using Jamii Forums mobile app
Unazijua Gulags? Au ulisikia kitu kinaitwa purge?? Stalin aliua warusi (ukigusia Soviet nzima basi mpaka Ukranians n.k) wengi kuliko hata Hitler.

Embu soma walau article hii ya NewYork Times (Credible Newspaper) inayorejea research za scholars wa Russia wenyewe

Hata wachina walikufa wengi wakati wa utawala wa Mao kuliko hata walivyovamiwa na Majeshi ya japana world war 2!! Ila haya huwa hayasemwi sababu tu Mao alishirikiana na majeshi ya Marekani kwenye WW II.

Kama ile Vita angeshinda Hitler basi leo hii Stalin,Churchill, na Mao wangeitwa mashetani wa karne ya 20. Hiyo ndio siasa ya mshindi akiandika historia
 
Je 'Wayahudi' waliofanyiwa mauaji ya kimbari katika simulizi yako, walikuwa ni wayahudi wa kimadhehebu ama walikuwa wayahudi wa kiutaifa?

Nimeuliza swali hili utupe ufafanuzi juu ya utata huu wa kihistoria.

Ukiangalia picha za wahanga wa mauaji hayo ni wazungu tena 'blonde' walionaswa nchi za Poland pamoja na nchi zingine jirani zilizovamiwa na kutekwa na Ujerumani.

Embu weka nyama kidogo kuiboresha simulizi yako mkuu.
[/QUOTE


Wayahudi simply ndio Waisraeli
 
Kaka yote unayodai kuwa matokeo bora ya Hitler – sehemu kubwa si kweli na kinyume ya historia. Hasa huwezi kuelewa kwa nini Wajerumani leo wanamchukia na kuona aibu juu ya utawala wake.

Unajua alifaulu kuharibu Ujerumani kushinda watawala wote? Robo moja ya nchi ilipotea – leo ni sehemu ya Poland na Urusi. Pamoja na mamilioni waliokufa vitani na katika makambi ya mauti, milioni 10 Wajerumani walipaswa kukimbia kutoka nyumbani kwao na kuhama sehemu nyingine za Ujerumani.

Hebu tuangalie yale unayodai yalikuwa mafanikio:

(1)Ujerumani ilipata Maendeleo makubwa ya kijeshi .

Faida yake nini?
(2)Ujerumani ilipata Maendeleo makubwa Ya Viwanda .
Si kweli. Ujerumani ilikuwa nchi ya viwanda vingi tayari. Kabla ya Hitler kutawala, asilimia zaidi ya 40 walikuwa tayari wafanyakazi viwandani, asilimia haikuongezeka chini yake.
(2)Utawala Wa Adolf Hitler Ulitatua tatizo la mdororo Wa uchumi
Si vile. Idadi ya Wajerumani haikuongezeka ajabu. Kinyume Hitler alikuwa na ndoto ya kuongeza idadi ya Wakulima na hapo alipanga kuvamia Urusi, kuifanya koloni na kutoa ardhi yake kwa wakulima Wajerumani. Hakuweza kuwaza kwamba maendeleo ya tekonolojia yataleta tokeo ambako asilimia 1-2 wakulima wanatosha kulisha taifa lote jinsi ilivyotokea baada yake

(3)Maendeleo makubwa Ya Sayansi na Teknolojia .
Si kweli. Ujerumani kabla ya Hitler ilikuwa nchi kiongozi kisayansi duniani. Kwa siasa yake alifukuza wengi wa wanasayansi bora (Einstein alifukuzwa kazi ya uprofesa..). Hadi Hitler Kijerumani ilikuwa lugha ya sayansi kimtaifa. Hitler alikimbiza wanasayansi wengi waliopokewa Marekani, sasa lugha kuu ya kisayansi ni Kiingereza

(4)Tatizo la Ajira
Tatizo la ajira lilitokana na Mdodoro Mkuu wa Uchumi wa 1929-1931 kote duniani, na kote duniani serikali zilifuata siasa ya kurudisha watu kwenye ajira – Ujerumani sawa na Marekani na Uingereza, Ufaransa
(5)Maendeleo makubwa ktk Sekta Ya Elimu.
Wapi? Idadi ya shule haikuongezeka chini ya Hitler. Kinyume chake: tazama juu, wanasayansi wengi waliondoka.

(6)Ujerumani iliendelea kwa Kasi kubwa ktk Sekta Ya Miundo mbinu
Alichofanya Hitler alijenga mtandao wa barabara kuu akitumia mipango iliyokuwa tayari; alifanya vile kwa sababu aliandaa vita akaona ni muhimu kuwa na barabara bora.

(7)Wafanyakazi waliboreshewa Hali zao .Hakukuwa na migomo
Wafanyakazi walikufa maana aliwafanya kuwa wanajeshi na kuwatuma katika vita pumbavu. Migomo ilipigwa marufuku.

(8)Maendeleo makubwa ktk Ujenzi wa Silaha .
Alitaka vita akaagiza silaha nyingi. Maendeleo? Mara Warusi walianza kutoa kifaru T34 vifaru vya Kijerumani vilishindwa. Vifaru vyake vyote vilikuwa na matatizo ya injini, maana Hitler mwenyewe alikataa matumizi ya injini za dizeli. Mahandisi wake walikuwa wa kwanza kutengeneza ndege za jeti na roketi (si ya kuvuka mabara unavyodai), lakini mpangilio ulikuwa kiholela na hivyo haikuwasaidia kitu.

Historia yake inakushinda, pole sana.
 
Je 'Wayahudi' waliofanyiwa mauaji ya kimbari katika simulizi yako, walikuwa ni wayahudi wa kimadhehebu ama walikuwa wayahudi wa kiutaifa?

Nimeuliza swali hili utupe ufafanuzi juu ya utata huu wa kihistoria.

Ukiangalia picha za wahanga wa mauaji hayo ni wazungu tena 'blonde' walionaswa nchi za Poland pamoja na nchi zingine jirani zilizovamiwa na kutekwa na Ujerumani.

Embu weka nyama kidogo kuiboresha simulizi yako mkuu.
Kukung'utwa na kuuwawa Kwa wayahudi ndio kumepelekea uwepo was taifa la Israel.

Big up Hitler
 
Back
Top Bottom