Je, adhabu hii dhidi ya Yanga itadumu?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Mniwie radhi kwa herufi makubwa, nimeichukua hii toka kwa Michuzi kama ilivyo.

SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI A.K.A TFF LEO IMEIFUNGIA TIMU YA YANGA KUTOSHIRIKI MICHEZO YOYOTE YA KIRAFIKI NA KIMASHINDANO YA KIMATAIFA NDANI NA NJE YA NCHI KWA KIPINDI CHA MIAKA 2 KUANZIA LEO.
KATIBU MKUU WA TFF FREDERICK MWAKALEBELA AMESEMA MCHANA HUU KWAMBA KAMATI YA UTENDAJI, IKITUMIA MAMLAKA YA KIKATIBA YALIYOMO KATIKA IBARA YA 34 (1Q) INAYOELEZEA MAENEO YA MAMLAKA YA KAMATI YA UTENDAJI, IMEAMUA KUTOA ADHABU KALI KWA YANGA ILI IWE FUNDISHO KWA YANGA YENYEWE NA TIMU ZINGINE ZENYE MAWAZO YA KUGOMEA MICHEZO.
KWA MUJIBU WA KAMATI HIYO YA UTENDAJI, YANGA WALIFANYA MAKOSA YAFUATAYO:
1. KUAIBISHA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU, TFF NA NCHI KWA JUMLA
2. KWENDA KINYUME NA TABIA YA UANAMICHEZO
3. KUHUJHUMU KWA KUSABABISHA MAPATO YA MCHEZO KUPUNGUA
4. KUSABABISHA TFF KUKOROFISHANA NA WADHAMINI WALIOWEKEZA PESA NYINGI KUDHAMINI MASHINDANO
5. KUIDHALILISHA TFF KAMA CHAMA MWENYEJI WA MASHINDANO YA UKANDA WOTE WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI NA WAANDAJI CECAFA
6. KUHATARISHA USALAMA WA WATU NA MALI ZAO
7. KURUDISHA NYUMA HATUA NA HARAKATI ZA KULETA MAENDELEO YA KWELI KATIKA SOKA
AIDHA, PAMOJA NA ADHABU HIYO, MWENYEKITI WA YANGA MH. IMNI MADEGA NA KATIBU MWENEZI WA KLABU HICHO FRANCIS LUCAS WAMEPEWA SIKU SABA KUANZIA LEO WATOE MAELEZO NA KUTHIBITISHA MADAI YA KUWEPO KWA MAKUBALIANO YA KULIPWA SH. MILIONI 50 KABLA YA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA.
 
Hii ni adhabu au kukomoa?Wanajenga au wanabomoa?
TFF hakuna viongozi ni uchwala tu.
 
Musonye anaendesha CECAFA kama kampuni yake hana kazi nyingine nini?, na ule mpango wa FIFA wa kuajiri makatibu wakuu katika vyama va mpira wa miguu unafuatwa na CECAFA? wanajua ajira ya Musonye ikoje?

Haiwezekani Mkenya mmoja awaendeshe watanzania anavyotaka, Tenga na Magoli bure kabisa. Jamaa ana emotions za ajabu analalamika yeye anachukua hatua yeye na anawatuma TFF nao wachukue hatua nao wanachukua hatua. hii kali kuliko ya yanga kuingia mitini, kesi moja mahakama mbili hukumu mbili watoa hukumu watu hao hao, mshtakiwa huyo huyo. siku mbili zimetosha kuendesha kesi, kuchunguza, kutoa hukumu. Only in Afrika.

Musonye anatukana mbele ya media na media ya kibongo iko kimya kwa sababu ya unazi dhidi ya Yanga.

Yanga msipapalike waacheni wachukue hatua zao, na nyinyi kusanyeni ushahidi tu, wataingia tu! Hakuna maamuzi magumu yaliyopita kiulaini, na Pareto ana 80/20 rule,si lazima wanachosema wengi kikawa sahihi.
 
...hiyo adhabu naipa wiki tu itatenguliwa,

Simba na Yanga ina mizizi mikubwa,...ukiwagusa Yanga ujue pia umemgusa Jakaya Kikwete, nk... Muungwana huyu mpaka mwembe yanga alikuwa anaegesha kijiweni.

Ukiwagusa Simba ujue umemgusa mpaka spika Mzee Sitta, nk...

atayedhania michezo haiingiliani na siasa ajue anajidanganya, ...wataziua hizo timu za kwao kina Gor Mahia, AFC leopards, etc, sio Yanga na Simba!
 
Nikumbushe timu gani ilisha ngoma kupeleka timu uwanjani dkk za mwisho kwenye michezo ya kimataifa, hizi tabia huwa tunaziona kwenye makombe ya Mbuzi..Mimi naona ni sawa kabisa yanga kufungiwa, hivi wale w2 waliotoa viingilio waliumia kiasi gani, watu walisafiri kwenda kuona hiyo mechi hlf wakazinguliwa kwa sababu zisizo za msingi au yanga hawakupewa kanuni za mashindano hayo na kama hawakupewa walishiriki vipi bila kanuni nakama walipewa ziliandikwa yanga na simba wapewe mil 50@ na bingwa $35000, lazima tukubali kitendo cha kutopeleka timu uwanjani ni chakipuuzi, tuache unazi. watu wangeamua kudai pesa zao nini kingetokea pale taifa..unataka Tenga afanye nini kwanza Tenga anamapenzi makubwa kuliko unavyo zania ila limewakera ndiyo maana wanatoa azabu kali vile.....na kwa taarifa yako bado CUF wakishusha rungu lao daaah mbona mtakoma...Musonye ni mtendaji wa CECAFA na hutoa hukumu kama yeye kamati ilikaa ikatoa maamuzi hayo kama angekuwa ni yeye angetoa baadaa ya dkk 45 bila yanga kutia timu....
 
...hiyo adhabu naipa wiki tu itatenguliwa,

Simba na Yanga ina mizizi mikubwa,...ukiwagusa Yanga ujue pia umemgusa Jakaya Kikwete, nk... Muungwana huyu mpaka mwembe yanga alikuwa anaegesha kijiweni.

Ukiwagusa Simba ujue umemgusa mpaka spika Mzee Sitta, nk...

atayedhania michezo haiingiliani na siasa ajue anajidanganya, ...wataziua hizo timu za kwao kina Gor Mahia, AFC leopards, etc, sio Yanga na Simba!

Mkuu Mchongoma,

Adhabu hii haina uhai mrefu.

1. Kimewekwa kipengele cha viongozi wa Yanga kutoa maelezo. Hii ni njia nyeupee wamepewa Yanga kutokea. Maelezo machache na kuomba radhi kwa kutoa faini.

2. Kikosi cha wachezaji 15 wa Taifa Stars kimefungiwa - ina maana Maximo ama hana kazi au ana kazi ya ziada ya kuanza upya na kikosi kipya.

3. Simba itacheza na nani? Kudorora kwa Ligi Kuu kwa miaka miwili? Mmmh!

4. Mashabiki wa Yanga kutokuhudhuria mechi yoyote kwa muda wote huo. Limishatokea hilo. TFF itafilisika upesi sana.

5. Mchezo wa soka utadorora ile mbaya yake.

Nahisi hata August 2008 haitakwisha Mabingwa watakuwa uwanjani. TFF haina ubavu wa kujitia kitanzi yenyewe. Ghadhabu ya mkizi.
 
Mchongoma,
Umenikumbusha yula Alhaji alikuwa katibu wa FAT jina limenitoka alikuwa anawaandama saana Yanga, unajua kilichotokea ? kumbe jamaa hakuwa mtanzania basi iliibuliwa kesi na kuvuliwa uraia, sasa tusubiri mambo. Tenga anasahau kuwa harakati za kuuondoa ukoloni zilifanyika Yanga sasa mambo yaanza.
 
Hiki ni kichekesho sana.
Hili kweli ni fundisho ama kuua soka. Hivi hawa TFF hawafahamu soka la Tanzania ama wanataka sifa tu eti watu waseme kuwa wanchukua hatua. Wanatakiwa kujua kuwa kitendo chao hicho kitafadhaisha watanzania wangapi.

Jambo ambalo silielewi ni kuwa adhabu imetolewa kisha viongozi wanaambiwa walete ushahidi. Mimi si mtaalamu wa mambo ya sheria, nilifikiri kabla ya kutoa maamuzi ilikuwa kwanza ushahidi uletwe, washitakiwa wajieleze kisha adhabu itolewe. Labda mtanisaidia wana JF namna ya kuendesha mambo. Je hao viongozi wa Yanga wakileta ushahidi na kujieleza na ikafahamika kuwa kuna sababu za msingi watabadilishaje maamuzi yao? Labda kutenda haki ni kuwaruhusu tu Yanga wakate rufaa katika chombo cha juu na ushahidi wao waupeleke huko na sio TFF tena kwani wao tayari walisha toa adhabu.
 
Haya ndio matatizo ya kuwa na viongozi wakurupukaji wanao toa maamuzi bila kufikiri
 
Kuna mambo manne hapa ya kuyaangalia. Kwanza, ni kweli kwa standards zozote viongozi narudia viongozi wa Yanga walikosea kutoipeleka timu uwanjani. Naamini viongozi wa Yanga walipewa kanuni za mashindano mapema kabla mashindano hayajaanza, wakazisoma, wakazielewa wakakubali kuingia mashindanoni kwa kuongozwa na kanuni hizo. Wanapogomea kundelea na mashindano kinyume cha kanuni hizo ni makosa na wanastahili kuadhibiwa.
Jambo la pili tunaambiwa Simba na Yanga (hapa hatuelezwi kuhusu Miembeni ambao pia ni timu ya Tanzania kama nayo ilikuwa ikipewa fedha) walikuwa wakipewa fedha (nasikia TZS 3m hadi 4m) kwa kila mechi walizocheza. Sijui zilikuwa ni fedha za nini, je timu zingine hasa Miembeni nazo zilipewa malipo haya? kama hazikupewa ni kwa nini hazikupewa? Je malipo waliyokuwa wanapewa Simba na Yanga yapo kwenye kanuni zilizokuwa zinaendesha mashindano hayo? Hivi fedha za viingilio nani alikuwa na mamlaka nayo? Ni nani alikuwa mwaandaaji wa mashindano hayo, ni CECAFA au TFF ambayo ilikuwa mwenyeji? Kama ni CECAFA, vipi TFF ipange kugawa mapato ya viingilio tena kwa timu chache tu za Simba na Yanga? Nadhani tunahitaji kupata majibu ya maswali haya kutoka kwa viongozi wetu wa TFF na CECAFA na ikiwezekana Yanga na Simba pia.
Tatu, mazingira yanaonyesha CECAFA nayo ilishiriki katika mazungumzo ya kupanga/kufafanua suala la kuwagawia Simba na Yanga fedha hizo (kwa mujibu wa maelezo ya Musonye kupitia kipindi cha michezo cha Redio moja hapa jijini), kama ndivyo kwa nini CECAFA ilikubadili kujadili jambo ambalo haliko ndani ya kanuni zake? Magori kaeleza walikubaliana wawape Simba na Yanga 10% ya mapato kwa mechi ya mwisho, ni kwa nini jambo hili lilifanyika usoni mwa CECAFA nayo imekaa kimya! Katika mazingira haya Yanga wakisema hapa kuna upendeleo watakuwa wanaongopa?
Jambo la nne, ni kuhusu taratibu na adhabu iliyopewa Timu ya Yanga kutokana na kugomea mchezo. Nilisema hapo juu kwamba kwa kitendo walichofanya viongozi wa Yanga kutopeleka timu uwanjani, hakika ni kibaya na wanastahili adhabu. Jambo la kujiuliza hapa ni kuwa KANUNI za CECAFA zinasema nini kuhusu jambo hili? Najua kama kuna utata wowote wanaweza ku-refer Kanuni za CAF au FIFA, lakini nazo zinasemaje? Musonye na wenzake wametumia kanuni ipi kuwafungia Yanga mashindano matatu na faini $35m. Hivi hii faini ya $ 35m ni kwa mujibu wa kanuni au kwa kuwa wanajua Yanga sasa wana fedha na hivyo wanaweza kulipa na wao kupata fedha hizo bila matatizo?
Tano, liko suala la haki ya mtuhumiwa kusikilizwa na kupewa haki ya kukata rufaa. Ni kwa nini Yanga na viongozi wake hawakupewa haki ya mambo hayo mawili ili haki ionekane imetendeka? Nimemsikia Musonye akisema kupitia kituo kimoja cha redio kuwa hakuna rufaa, tena akisema rufaa ya nini. Musonye vilivile ametoa matusi kwa viongozi wa Yanga, hivi kweli viongozi hawa kwa matendo haya tunawaamini kuendesha na kuendeleza mpira katika ukanda huu? TFF wamewataka Madega na Francis kutoa maelezo ndani ya siku saba kwa nini nao wasiadhibiwe, je haingekuwa vema na haki pia kabla ya kuwafungia Yanga mashindano/michezo ya kirafiki ya nje na ndani kuwapa kwanza nafasi ya kujitetea?
Adhabu waliyopewa Yangu inakusudia kutoa fundisho kwa timu zingine na Yanga yenyewe au kuikomoa? Pengine kwa timu zingine ndio, lakini kwa timu ya Yanga napata wasiwasi kidogo.
Natoa rai waungwana kuwa ni vema kuweka mwelekeo imara wa kule tuendako tunapojaribu kutatua matatizo tuliyonayo
 
Kuna mambo matano hapa ya kuyaangalia. Kwanza, ni kweli kwa standards zozote viongozi narudia viongozi wa Yanga walikosea kutoipeleka timu uwanjani. Naamini viongozi wa Yanga walipewa kanuni za mashindano mapema kabla mashindano hayajaanza, wakazisoma, wakazielewa wakakubali kuingia mashindanoni kwa kuongozwa na kanuni hizo. Wanapogomea kundelea na mashindano kinyume cha kanuni hizo ni makosa na wanastahili kuadhibiwa.
Jambo la pili tunaambiwa Simba na Yanga (hapa hatuelezwi kuhusu Miembeni ambao pia ni timu ya Tanzania kama nayo ilikuwa ikipewa fedha) walikuwa wakipewa fedha (nasikia TZS 3m hadi 4m) kwa kila mechi walizocheza. Sijui zilikuwa ni fedha za nini, je timu zingine hasa Miembeni nazo zilipewa malipo haya? kama hazikupewa ni kwa nini hazikupewa? Je malipo waliyokuwa wanapewa Simba na Yanga yapo kwenye kanuni zilizokuwa zinaendesha mashindano hayo? Hivi fedha za viingilio nani alikuwa na mamlaka nayo? Ni nani alikuwa mwaandaaji wa mashindano hayo, ni CECAFA au TFF ambayo ilikuwa mwenyeji? Kama ni CECAFA, vipi TFF ipange kugawa mapato ya viingilio tena kwa timu chache tu za Simba na Yanga? Nadhani tunahitaji kupata majibu ya maswali haya kutoka kwa viongozi wetu wa TFF na CECAFA na ikiwezekana Yanga na Simba pia.
Tatu, mazingira yanaonyesha CECAFA nayo ilishiriki katika mazungumzo ya kupanga/kufafanua suala la kuwagawia Simba na Yanga fedha hizo (kwa mujibu wa maelezo ya Musonye kupitia kipindi cha michezo cha Redio moja hapa jijini), kama ndivyo kwa nini CECAFA ilikubadili kujadili jambo ambalo haliko ndani ya kanuni zake? Magori kaeleza walikubaliana wawape Simba na Yanga 10% ya mapato kwa mechi ya mwisho, ni kwa nini jambo hili lilifanyika usoni mwa CECAFA nayo imekaa kimya! Katika mazingira haya Yanga wakisema hapa kuna upendeleo watakuwa wanaongopa?
Jambo la nne, ni kuhusu taratibu na adhabu iliyopewa Timu ya Yanga kutokana na kugomea mchezo. Nilisema hapo juu kwamba kwa kitendo walichofanya viongozi wa Yanga kutopeleka timu uwanjani, hakika ni kibaya na wanastahili adhabu. Jambo la kujiuliza hapa ni kuwa KANUNI za CECAFA zinasema nini kuhusu jambo hili? Najua kama kuna utata wowote wanaweza ku-refer Kanuni za CAF au FIFA, lakini nazo zinasemaje? Musonye na wenzake wametumia kanuni ipi kuwafungia Yanga mashindano matatu na faini $35m. Hivi hii faini ya $ 35m ni kwa mujibu wa kanuni au kwa kuwa wanajua Yanga sasa wana fedha na hivyo wanaweza kulipa na wao kupata fedha hizo bila matatizo?
Tano, liko suala la haki ya mtuhumiwa kusikilizwa na kupewa haki ya kukata rufaa. Ni kwa nini Yanga na viongozi wake hawakupewa haki ya mambo hayo mawili ili haki ionekane imetendeka? Nimemsikia Musonye akisema kupitia kituo kimoja cha redio kuwa hakuna rufaa, tena akisema rufaa ya nini. Musonye vilivile ametoa matusi kwa viongozi wa Yanga, hivi kweli viongozi hawa kwa matendo haya tunawaamini kuendesha na kuendeleza mpira katika ukanda huu? TFF wamewataka Madega na Francis kutoa maelezo ndani ya siku saba kwa nini nao wasiadhibiwe, je haingekuwa vema na haki pia kabla ya kuwafungia Yanga mashindano/michezo ya kirafiki ya nje na ndani kuwapa kwanza nafasi ya kujitetea?
Adhabu waliyopewa Yangu inakusudia kutoa fundisho kwa timu zingine na Yanga yenyewe au kuikomoa? Pengine kwa timu zingine ndio, lakini kwa timu ya Yanga napata wasiwasi kidogo.
Natoa rai waungwana kuwa ni vema kuweka mwelekeo imara wa kule tuendako tunapojaribu kutatua matatizo tuliyonayo
 
mimi nashabikia yanga, sikufurahia yanga kukacha ile mechi. Ila, kwa watz wapenda maendeleo ya mpira, sioni kama ni solution kutoa adhabu kama ile. TFF hawakutakiwa kutoa adhabu ile, kwasababu Yanga sasa itakufa kabisa, wachezaji wake ndo kipaji chao kitaishia pale hivyo tutakuwa tumewakomoa na kulikomoa taifa pia, sio solution hii. sidhani kama walikuwa na individual thinking capacity na diligence kabla ya kufanya uamuzi huu. ilitosha kwa Cecafa kutoa adhabu, sio iongeze na TFF, haiwahusu. kina kaseja watacheza wapi mpira sana, na vipaji vyote hivyo ndo vimeisha wanarudi kuvuta bangi mtaani. hivi mtoto wako akikosa, unaweza kutoa adhabu ya kuuua na kumkomoa kabisa au kumvunja miguu awe kilema, au utatoa adhabu ya busara ili imsaidie aendelee mbele asijekuwa kilema ukawa na mtoto kilema?, TFF hawana akili, nao sio wafaifa kabisa.

wameendeshwa na yule mkenya? kumbe ni mkenya, hata sikujua hilo,ndo najua sasahivi. mimi nilifikiri ni mnyarwanda, ndo maana nilishangaa hata wanyarwanda wanakuwa na negative attitude kwa watz?, nilishangaa kwasababu yule jamaa alivyohojiwa alionyesha kama likuwa na kinyongona timu za tz toka mda mrefu sasa ulifika muda wa kuwakomesha vile, manake alisisitiza sana kuwa yanga, timu ya dsm nakadhalika. halafu alionyesha kama haipendi sana nk. ni muda mrefu, wakenya na watz hua hawapendani, sijui hii itakuja iishe lini. hata tukionyesha kuwa tunapendana, huwa kuna ka element ka ushindani na uadui ndani yetu, kama tunataka kuendeleza eas africa inabidi wakenya wabadilike na sisi pia.

kwa kufanya hivyo, soka kenya itaendelea na nchi zingine, na tz itabakia hivihivyo. yangana ndo kuna wachezaji wengi wa taifa stars, sasa wote hawana kazi. nasema hawana kazi kwasababu yanga isipocheza, itapata wapi hela za kuendesha shuguli na kuwalipa wachezaji? si ndo itawaruhusu tu waende kussajiliwa kwingine?, hivi tunaendeleza soka au tunaua,kweli tuue yanga leo, wenzetu wanajitahidi kuimarisha na kuanzisha timu mpya sisi tunaua. hahahaha. wendawazimu kweli....hahaha.
 
kuna mkuu mmoja hapa ameongea kitu chamaana sana. hivi mtu unaweza ukahukumiwa bila kujitetea, au hivi yanga wanaweza wakawa na sehemu wanayotakiwa kukata rufaa ili hukumu hii ivujwe?, kikwete, wewe si unanisikia, au hujaona, si nasikia na wewe pia ni mshabiki mwenzangu wa yanga, pamoja na ccm wote....hebu fanyeni utaratibu wa kurekebisha mambo haraka iwezekanavyo. hapa tunaua soka, na litakufa kweli nawambieni.
 
Ukiangalia kwa makini Soka la Tanzania lilikuwa linapaa sasa angalia usajili wa Yanga watu wamesajiliwa kwa mamilioni wengine saizi wameuaga umaskini.Kitendo cha kuifungia Yanga miaka yote hiyo nikuua ajira pamoja na vipaji vya wachezaji.Kosa sawa tunakubali wamefanya lakini mazingira ya adhabu zinavyo tolewa inaonyesha wazi wazi ni kukomoana tu hakuna kingine.Adhabu juu ya adhabu hivi kanuni za michezo zinatumika pande zote?Namaanisha kanuni za Ligi kuu ya Voda zinawiana na zile za CECAFA?au CECAFA na CAF zinawiana?
TFF pale hakuna viongozi huyo Tenga tulikuwa tunamtegemea kama msomi kumbe naye hakuna kitu kwenye bongo yake maamuzi gani kama haya ya kutofikiria.
Na kwa nini huyo mkenya aliye tukana mnamwacha anapeta tu?Au matusi yapo kwenye kanuni zenu za CECAFA?Tunaomba waziri aingilie kati swala hili lasivyo tunawazibia hata RUZUKU ile mnayo gombania na ZFA kutoka FIFA.
 
Hawa Yanga Kawaponza Gabacholi Wao Yulee...huyu Jamaa Amekuwa Na Tabia Ya Kuchonganisha Na Kuwaaribia Watu Kutokana Na Jeuri Yake Ya Pesa ,najua Wazo La Kutopeleka Timu Uwanjani Kisasa Na Madega Kama Madega Wasingekubaliana Nalo Lakini Kilichowaponza Ni Tamaa Ya Hela Za Gabacholi Huyo.sasa Angalia Walivyoiponza Klabu .....na Wao Adhabu Yao Inakuja.huyu Mdosi Aliznza Siku Nyingi.kashawagombanisha Viongozi Wengi Wa Serikali Wa Juu Kwa Ajili Ya Matakwa Yake Mpaka Wengi Hadi Leo Hawasalimiani.juzi Juzi Katoka Kuwagombansha Kikundi Kimoja Cha Vichekesho Na Bosi Wao Wa Zamani...tumuangalie Sana Kwanza Yeye Si Mtu Wa Mpira Kusema Ukweli
 
ni kweli, yawezekana ni gabacholi manji, lakini hatuna uhakika, pamoja na kwamba yeye ndo kazi yake kuchonganisha na kuwatelekeza watu. angalia hata zecomedy, wamechonganishwa na wameisha.sasahivi watu wameshaanzakuwasahau, wakija wataanza upyaaa, kwasababu ya huyo gabacholi.

Tatizo litaweza kuwa solved,kama kutakuwa na mabadiliko kule TFF. kuanzia Tenga hadi kaijage wanatakiwa wawe nje, kwasababu sio wataifa kabisa. Tumeweka watu kule hawana akiili ujue. juzi tu hapa walikuwa wametoa kauli ya kumlipisha mtu kwasababu ya jezi, wakajigonga wenyewe wakaonyesha kuwa kumbe huwa hawafikirii kwanza kabla ya kufanya jambo. Tenga pale hala lolote zaidi ya kujidai yeye kuwa ni msomi, kuishia kulambalamba midomo yake pale wakati wa kuongea, kumbe hana lolote. na mimi huwa ananikera, hivi kwanini anatabia ya kulamba midomo yake vile...hahaha. futilia mbali watu wasio na mtazamo wa mbele kisoka hawa.

ajira ngapi zitayoyoma hapa, watu wangapi watafilisika hapa, they din't foresee before deciding this, hawakuona kabisa madhara yake, kumbe walikuwa wanajikata wenyewe na kuzikata juhudi za taifa lao kujikkwamua na ukichwa cha mwendawazimu. lol!.
 
Yanga yafungiwa CAF

na Khadija Kalili
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SIKU moja baada ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuifungia Yanga katika mashindano yake, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), nalo limeipiga ‘stop' kucheza mashindano ya kimataifa kwa miaka miwili.

Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, alisema jana kuwa huo ni uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo, iliyoketi juzi na kutoa adhabu hiyo kwa kitendo kilichofanywa na Yanga.

Mbali ya adhabu hiyo kwa Yanga, pia Mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega na Katibu Mwenezi wake, Francis Lucas, wamepewa siku saba kuthibitisha madai kuwa kulikuwa na makubaliano ya Simba na Yanga kupewa sh mil 50 kila moja.

Mwakalebela, alisema Mwakalebela alisema Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Jumatatu na Rais wa Shirikisho hilo, Leodegar Tenga, imetoa adhabu hiyo ili kuwa funzo kutokana na timu hiyo kuwakacha Simba katika mechi ya Jumapili.

Hiyo ilikuwa mechi ya kusaka nafasi ya mshindi wa tatu wa michuano ya Kombe la Kagame, iliyoanza Julai 12 na kufikia tamati Julai 27.

Alisema kuanzia jana ni marufuku Yanga kucheza mechi za kimataifa - iwe za kirafiki au za ushindani - hali inayoifanya Yanga kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ilipata nafasi hiyo baada ya kumaliza nafasi ya kwanza katika Ligi Kuu iliyofikia tamati Aprili 27, huku Prisons ikimaliza ya pili na Simba nafasi ya tatu.

Alisema kuwa adhabu hiyo imetolewa na Kamati hiyo kwa mujibu wa mamlaka ya kikatiba iliyopewa kutokana na makosa yaliyofanywa na Yanga yaliyoitia nchi aibu.

"Ni kinyume kabisa cha dhana ya ‘fair play' (uungwana wa michezo). Zaidi ya hapo, kitendo cha Yanga kimeiweka katika nafasi mbaya TFF na wadhamini waliowekeza mamilioni ya shilingi katika mashindano hayo," alisema Mwakalebela.

Mwakalebela alisema kitendo cha Yanga kimeidhalilisha TFF kama mwenyeji wa mshindano ya Cecafa, kwani kingeweza kuhatarisha usalama wa watu na mali zao na kurudisha nyuma jitihada za maendeleo ya soka nchini.

Mbali ya adhabu hiyo, Kamati ya Utendaji, ikitumia ibara ya 34 kifungu 1(q), Madega na Lucas wametakiwa kuwasilisha utetezi wao kuhusu kila klabu kupewa sh mil 50.

Alisema hiyo ni kutokana na kauli ya Katibu Mwenezi wa klabu hiyo, Lucas, aliyotoa muda mfupi baada ya kufutwa kwa mechi ya Simba na Yanga, kwamba Yanga ilifanya hivyo baada ya TFF na Cecafa kukiuka makubaliano ya kila klabu kupewa mil 50.

Mwakalebela alisema Jumapili jioni Julai 27, Mwenyekiti wa Yanga, Madega, alikutana na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Lamada na kusisitiza madai yaliyokuwa yametolewa na katibu mwenezi wake, kwamba walizuia timu baada ya kubaini unafiki na ubabaishaji katika uendeshaji wa soka.

Mwakalebela alisema kilichotokea ni viongozi wa klabu hizo kuomba kupewa fedha za kulipia gharama za kambi, hivyo kila timu kupatiwa sh mil 5.

Katika kuleta ufanisi zaidi, TFF ilifanya mazungumzo na wadhamini wa michuano hiyo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), waliotoa sh mil 3 kwa Yanga, Simba na Miembeni.

Alisema baada ya kutekelezwa hayo, suala la fedha lilikuwa limekwisha, hivyo kupisha taratibu nyingine za mechi ya Jumapili ambako saa nne subuhi ya siku ya mechi, kulikuwa na mkutano na kuhudhuriwa na viongozi wa klabu zote mbili.

Kwa mantiki hiyo, hakukua na makubaliano yoyote kuhusu Simba na Yanga kupewa fedha kiasi cha sh mil 50 kabla ya mechi.

Katika hatua nyingine, Rais wa Cecafa, Leodegar Tenga, amesema hana budi kuwaangukia kwa maandishi wadhamini wote na mlezi wa Kombe hilo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kwa kitendo kilichotokea.

Wadhamini wa Kombe hilo, TBL kupitia bia yake ya Castle na Shiririka la Utangazaji Tanzania (TBC) na mashabiki wote wa soka wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
 
tafadhari aliyekariri maneno machafu aliyotoa musonye wa cecafa kwa yanga naomba ayakakariri hapa niyaone
 
Adhabu wanazotoa TFF na CECAFA sidhani kama zipo kisheria (kwenye katiba). haiwezekani CECAFA watoe zawadi ya dola 30,000 kwa mshindi. na kwa yanga hata kama wangeshinda wangeambulia dola 10,000. halafu kwenye adhabu zaidi ya kufungiwa waambiwe walipe dola 35,000, inaingia akilini kweli? Na TFF wanakurupuka kuwafungia Yanga katika mechi za kimataifa na kuruhusu wacheze hizi za ndani, jamani si maajabu hayo? kama kuna mtu mwenye hizo katiba hasa vipengele vya adhabu atutumie humu. Hivi hawa TFF huwa wanafocus yoyote ya kuendeleza michezo hasa kwenye virabu? au wanapata uraji tu na hasa wanakula sana pale wakitumia uwanja mpya wa Taifa.
Jamani watanzania tubadilike. Michezo inaleta ajira na kunyanyua uchumi wa nchi lakini hapa wabongo longolongo nyingi sana hasa kwa viongozi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom