Je, Acacia waanza kufungasha kiaina? Wauza 51% ya shares mgodi mmoja!, wajipanga kuuza shares zote 100%

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,988
2,000
Wanabodi,

Leo naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" hili ni bandiko la swali "Jee Acacia Waanza Kufungasha Kiaina?!. Wauza 51% ya Shares Mgodi -wa Nyanzaga, huku Wakijipanga Kuuza shares zote asilimia 100%!", hawa jamaa hawatatuacha solemba ?!.

Huku mazungumzo kati ya serikali yetu na kampuni ya Barrick, yakiendelea ambapo yamefikia hatua nzuri, mgodi wa Acacia ambao tunaudai matrilioni ya fedha kutokana na kutuibia kwenye makinikia, wameanza kufungasha mdogo mdogo kwa kuanza kuuza shares zake kidogo kidogo.

Katika website yao, leo wametangaza kuuza asilimia 51% umiliki wa mgodi wa Nyanzaga kwa kampuni ya OneCorp Tanzania Limited. Ukisikia kampuni imeuza asilimia zaidi ya 51% kwa kampuni nyingine, hiyo kibiashara ni kuachia bodi kiaina, aliyeuziwa anamiliki majority shares na imeeleza wazi ina mpango wa kuiuzia OreCorp Tanzania, shares zote zilizobakia, hivyo Acacia kujitoa kabisa katika umiliki wa mgodi huo!.

Wasiona mbali, wanaweza kuona uamuzi huu kama ni uamuzi tuu wa kawaida wa kibiashara kwenye, mergers and acquisitions lakini kwa sisi waona mbali, hizo ndizo dalili za awali za watu kutaka kuachwa solemba!. Nawaombeni sana msije kushangaa, kabla Acacia haijaunda ile kampuni mpya ya kumilikiwa kwa ubia na Tanzania ambayo tutamiliki asilimia 16% ya shares, mnaweza kukuta kila kitu kimeishauzwa kwa Wachina!.

Taarifa yenyewe rasmi ni hii

PRESS RELEASES
Nyanzaga Project Update
06 Sep 2018
Further to the announcements made on 20 July 2018, the Tanzanian Fair Competition Commission (FCC) has now granted its approval for OreCorp Tanzania Limited (OreCorp Tanzania) to increase its interest in Nyanzaga Mining Company Limited (NMCL) to 51%. This move remains subject to: (i) the approval of the newly established Mining Commission, the application for which was lodged at the same time as the application for FCC approval; and (ii) the future payment of US$3 million to the Acacia Group.
In addition, members of the OreCorp Group have now entered into a completion agreement with Acacia and other members of the Acacia Group to allow OreCorp Tanzania to move to 100% ownership of NMCL, and thereby 100% ownership of the Nyanzaga Gold Project (Project). This move remains subject to: (i) the Tanzanian regulatory approvals referred to above; (ii) the grant of the Special Mining Licence (SML) in respect of the Project; and (iii) the making of a future payment of US$7 million. Following completion Acacia will retain a net smelter return production royalty over the Project, capped at US$15 million.
Both OreCorp and Acacia believe that a simplified ownership structure of NMCL is beneficial to the future development of the Project and would enable it to be best placed to provide significant benefits to Tanzania and all stakeholders.

Nyanzaga Project Update

© Copyright 2018 Acacia Mining plc. All rights reserved

Kama hawa jamaa hawajatulipa hata senti tano na sasa ndio wanaanza kuuza mali zao kwa asilimia 100%, hawa jamaa hawatakuja kweli kutuacha solemba?.

Msingi mkuu wa majadiliano kati ya Barrick na serikali yetu ni trust and transparency, yaani uwazi na kuaminiana, tayari kuna minong'ono, yale makontena ya makinikia, yamehamishwa mahali yalipokuwepo, isije ikawa yameondoka!.

Hitimisho.
Kwa vile Acacia ndio the determinant ya kila kitakachoamuliwa na mazungumzo yetu na Barrick, then serikali yetu iangazie kwa makini, kila kinachofanywa na Acacia, kukiangazia kina maanisha nini, what is the motive behind his mergers and acquisitions wakati tunapaswa kuunda kampuni mpya ya kugawana 50/50 ya faida. My sixth sense tells me kuwa kabla hatujafika huko, huku tutakuwa tumebakiwa na skeletons!.

Mungu Ibariki Tanzania!.
Paskali
Update
briefly walikuwa na kitu kinaitwa earn-in agreement na acacia, nadhani mkataba ulisainiwa september 2015, at first walipata 5% ya shares baada ya kutumia $1m, baadae waliendelea to perform earn-in obligations (pre-feasibility study)zilizowafanya kutumia jumla ya $14m na kupata 25% ya ownership, wamelipa $3m kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba na ku-qualify kumiliki mgodi kwa asilimia 51. wanategemea kulipa another $7m zitakazowaleta kwenye 100%
kwa ufupi.
Hii ni taarifa muhimu sana, kumbe mkataba wa kuuziana shares ulianza toka mwaka 2015 kabla hata ya sakata la makinikia!. Sisi tumejua kuwa baada ya kushukiwa kuwa walikuwa wanatuibia, ndia kaamua kuuza kila kitu na kusepa, kumbe sio hivyo!.

Hata hivyo, baada ya Tanzania kuwa na sheria mpya ya madini kuwa serikali lazima imiliki 16% percent ya migodi yote na gesi yote, na hawa Acacia wamekubali tutagawana faida 50/50, nilidhani as of now, Acacia walipaswa kusimamisha all mergers na acquisitions mpaka the regulations za sheria mpya are in place. Kitendo cha kuuza 100% stake, wakati sisi tayari tuna 16% stake yetu, nadhani hakijakaa vizuri. Barrick nao wako kwenye mazungumzo na Wachina ku off load shares zao zote za Acacia, by the time tunakuja kushtuka, tunakutana na mifupa, nyama yote imeliwa!.

Mazungumzo yetu haya ndio ya kwanza mimi kusikia wazungu hawana haraka!. Extractive Industries ni diminishing resources, zinakwenda zikipungua!, take it from me, by the time tunakuja kugawana hiyo 50/50, it might be ni 50/50 ya hasara!.
P.
 
successor

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
3,085
2,000
Wanaondoka kwa kujidai, hawana haraka, wanauza shares taratiiibu, hawatulipi hata senti mbovu, wamefungua kesi, na hakuna cha kuwafanya, uhakika wa kushinda kesi ni mkubwa, hapo ndio tutajua madhara ya kukurupuka ili kujipatia sifa zisizostahili.

Tusubiri maumivu.
 
LUCKDUBE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,183
2,000
Wanaondoka kwa kujidai, hawana haraka, wanauza shares taratiiibu, hawatulipi hata senti mbovu, na wamefungua kesi, hakuna kuwafanya, na uhakika wa kushinda ni mkubwa, hapo ndio tutajua madhara ya kukurupuka ili kujipatia sifa zisizostahili.

Tusubiri maumivu.
Ukute hata hao wanaouziwa share ni watu wao yaani wanakuja kivingine,

Pesa tunapigwa na wanaendelea kuchimba kwa kivuli cha wachina
 
Dr.Godbless

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
828
1,000
Kosa la msingi lilianzia kwenye setting ya kikao cha majadiliano. GoT inamtuhumu Acacia kama ndio mkwepa kodi na ndio anastahili kutulipa trilioni 400 . Majadiliano hayajahusisha Acacia kwa sababu kwamba GoT haiitambui kwa kuwa haina usajili na Brela. Majadiliano na Makubaliano ni kati ya Barrick na GoT ambapo tuliahidiwa kishika uchumba cha Bilioni 300, japo Acacia waliweka wazi kuwa hawana fedha za kulipa. Kwa kifupi tumejiingiza mkenge wenyewe kwa kujifanya tunajua. Na wao Barrick na Acacia wakatupumbaza kana kwamba Barrick hawakubaliani na kinachofanywa na Acacia kumbe wao kwa wao wana jinsi yao ya kuelewana.
 
CHLOVEK

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
534
1,000
Wanabodi,

Leo naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" hili ni bandiko la swali "Jee Acacia Waanza Kufungasha Kiaina?!. Wauza 51% ya Shares Mgodi -wa Nyanzaga, huku Wakijipanga Kuuza shares zote asilimia 100%!", hawa jamaa hawatatuacha solemba ?!.

Huku mazungumzo kati ya serikali yetu na kampuni ya Barrick, yakiendelea ambapo yamefikia hatua nzuri, mgodi wa Acacia ambao tunaudai matrilioni ya fedha kutokana na kutuibia kwenye makinikia, wameanza kufungasha mdogo mdogo kwa kuanza kuuza shares zake kidogo kidogo.

Katika website yao, leo wametangaza kuuza asilimia 51% umiliki wa mgodi wa Nyanzaga kwa kampuni ya OneCorp Tanzania Limited. Ukisikia kampuni imeuza asilimia zaidi ya 51% kwa kampuni nyingine, hiyo kibiashara ni kuachia bodi kiaina, aliyeuziwa anamiliki majority shares na imeeleza wazi ina mpango wa kuiuzia OreCorp Tanzania, shares zote zilizobakia, hivyo Acacia kujitoa kabisa katika umiliki wa mgodi huo!.

Wasiona mbali, wanaweza kuona uamuzi huu kama ni uamuzi tuu wa kawaida wa kibiashara kwenye, mergers and acquisitions lakini kwa sisi waona mbali, hizo ndizo dalili za awali za watu kutaka kuachwa solemba!. Nawaombeni sana msije kushangaa, kabla Acacia haijaunda ile kampuni mpya ya kumilikiwa kwa ubia na Tanzania ambayo tutamiliki asilimia 16% ya shares, mnaweza kukuta kila kitu kimeishauzwa kwa Wachina!.

Taarifa yenyewe rasmi ni hii

PRESS RELEASES
Nyanzaga Project Update
06 Sep 2018
Further to the announcements made on 20 July 2018, the Tanzanian Fair Competition Commission (FCC) has now granted its approval for OreCorp Tanzania Limited (OreCorp Tanzania) to increase its interest in Nyanzaga Mining Company Limited (NMCL) to 51%. This move remains subject to: (i) the approval of the newly established Mining Commission, the application for which was lodged at the same time as the application for FCC approval; and (ii) the future payment of US$3 million to the Acacia Group.
In addition, members of the OreCorp Group have now entered into a completion agreement with Acacia and other members of the Acacia Group to allow OreCorp Tanzania to move to 100% ownership of NMCL, and thereby 100% ownership of the Nyanzaga Gold Project (Project). This move remains subject to: (i) the Tanzanian regulatory approvals referred to above; (ii) the grant of the Special Mining Licence (SML) in respect of the Project; and (iii) the making of a future payment of US$7 million. Following completion Acacia will retain a net smelter return production royalty over the Project, capped at US$15 million.
Both OreCorp and Acacia believe that a simplified ownership structure of NMCL is beneficial to the future development of the Project and would enable it to be best placed to provide significant benefits to Tanzania and all stakeholders.

Nyanzaga Project Update

© Copyright 2018 Acacia Mining plc. All rights reserved

Kama hawa jamaa hawajatulipa hata senti tano na sasa ndio wanaanza kuuza mali zao kwa asilimia 100%, hawa jamaa hawatakuja kweli kutuacha solemba?.

Msingi mkuu wa majadiliano kati ya Barrick na serikali yetu ni trust and transparency, yaani uwazi na kuaminiana, tayari kuna minong'ono, yale makontena ya makinikia, yamehamishwa mahali yalipokuwepo, isije ikawa yameondoka!.

Hitimisho.
Kwa vile Acacia ndio the determinant ya kila kitakachoamuliwa na mazungumzo yetu na Barrick, then serikali yetu iangazie kwa makini, kila kinachofanywa na Acacia, kukiangazia kina maanisha nini, what is the motive behind his mergers and acquisitions wakati tunapaswa kuunda kampuni mpya ya kugawana 50/50 ya faida. My sixth sense tells me kuwa kabla hatujafika huko, huku tutakuwa tumebakiwa na skeletons!.

Mungu Ibariki Tanzania!.
Paskali
Mungu hawezi Ibariki tanzania tunayoiharibu sisi wenyewe, hilo la kwanza, la pili ni kwamba kama gesi na uranium Rais wetu amekiri tumeshanyang'anywa kwa mikataba waliyoingia wabunge wetu na hili tukubali tu wajichukulie tu kama mikataba waliyosaini viongozi wetu inavyosema. Yakiisha madini tutajishughulisha na kilimo zaidi.
 
MKANDAHARI

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
4,354
2,000
Matrilioni tumekosa, kodi tumekosa, ajira tumekosa, kesi tumefunguliwa, fidia ya matrilioni tutawalipa na makinikia yataondoka. Sasa si ni bora wangeachwa waendelee huku tukijipanga kurekebisha mikataba yetu?

Jiwe alijitafutia umaarufu wa kisiasa bila kujua madhara yake. Ona hasara tutakayoipata kwa kukurupuka kwake.

Jiwe analia lia tena kuhusu gesi, wakati mikataba hiyo ilipitishwa kwa hati ya dharura na yeye alishiriki kuipitisha huku wapinzani wakiipinga mwisho wa siku wakaishia kuonekana wapinga maendeleo

Mimi kiukweli nikiona mtu anaeisapoti CCM kwa hali yeyote ile huwa namshangaa sana.

Tumefika hapa kwa sababu ya CCM so tusitarajie mapya kwa CCM na wengi watamlaumu JK ila kiukweli hata akija mwingine Jiwe nae ataonekana ni Rais dhaifu kuwahi kutokea

CCM ni ile ile
 
Jorojik

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
3,396
2,000
Kosa la msingi lilianzia kwenye setting ya kikao cha majadiliano. GoT inamtuhumu Acacia kama ndio mkwepa kodi na ndio anastahili kutulipa trilioni 400 . Majadiliano hayajahusisha Acacia kwa sababu kwamba GoT haiitambui kwa kuwa haina usajili na Brela. Majadiliano na Makubaliano ni kati ya Barrick na GoT ambapo tuliahidiwa kishika uchumba cha Bilioni 300, japo Acacia waliweka wazi kuwa hawana fedha za kulipa. Kwa kifupi tumejiingiza mkenge wenyewe kwa kujifanya tunajua. Na wao Barrick na Acacia wakatupumbaza kana kwamba Barrick hawakubaliani na kinachofanywa na Acacia kumbe wao kwa wao wana jinsi yao ya kuelewana.
Hahahaha......Dunia ni utata mtupu, hii kitu kinachoitwa acacia haipo na kinaeleaelea tu hewani. Awali kulikuwa na kampuni mama inayoitwa Barrick Gold ya Canada iliyokuwa ikichimba dhahabu Tanzania, Chile na Papua New Guinea. Kwa Tanzania migodi ya Barrick Gold ndo hayo ya Tulawaka, Bulyanhulu, Buzwagi na Northmara.

Barrick Gold wakageuza gia angani wakidai wanataka kuimarisha portfolio yao ya uchimbaji Chile na Papua na kwamba migodi yake ya Tanzania yataundiwa kampuni tanzu itakayoitwa Barrick Africa. Barrick africa ikaundwa. Kwa hiyo Barrick africa ilioperate hadi ilipofunga mgodi wa Tulawaka kwa madai kwamba gold reserve imeisha. Mgodi ukapewa Stamico chini ya wizara ya madini.

Ghafla tena Barrick Africa ikabadili jina na kujiita Acacia bila ya jina hilo kusajiliwa nchini ikiwemo Brela. Maajabu haya. Wakati Barrick Africa ilipokuwa inadecommision mgodi wa Tulawaka ilisema inataka kutanua shughuli zake za uchimbaji ktk miradi yake mipya ya Nyanzaga na Kabanga. Wakati huo nyanzaga ni just mradi uliokuwa under survey. Uchimbaji ulikuwa haujaanza. Sasa leo acacia ambayo haitambuliki nchini inauza nyanzaga baada ya kukamilisha survey.
 
Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,605
2,000
Wanabodi,

Leo naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" hili ni bandiko la swali "Jee Acacia Waanza Kufungasha Kiaina?!. Wauza 51% ya Shares Mgodi -wa Nyanzaga, huku Wakijipanga Kuuza shares zote asilimia 100%!", hawa jamaa hawatatuacha solemba ?!.

Huku mazungumzo kati ya serikali yetu na kampuni ya Barrick, yakiendelea ambapo yamefikia hatua nzuri, mgodi wa Acacia ambao tunaudai matrilioni ya fedha kutokana na kutuibia kwenye makinikia, wameanza kufungasha mdogo mdogo kwa kuanza kuuza shares zake kidogo kidogo.

Katika website yao, leo wametangaza kuuza asilimia 51% umiliki wa mgodi wa Nyanzaga kwa kampuni ya OneCorp Tanzania Limited. Ukisikia kampuni imeuza asilimia zaidi ya 51% kwa kampuni nyingine, hiyo kibiashara ni kuachia bodi kiaina, aliyeuziwa anamiliki majority shares na imeeleza wazi ina mpango wa kuiuzia OreCorp Tanzania, shares zote zilizobakia, hivyo Acacia kujitoa kabisa katika umiliki wa mgodi huo!.

Wasiona mbali, wanaweza kuona uamuzi huu kama ni uamuzi tuu wa kawaida wa kibiashara kwenye, mergers and acquisitions lakini kwa sisi waona mbali, hizo ndizo dalili za awali za watu kutaka kuachwa solemba!. Nawaombeni sana msije kushangaa, kabla Acacia haijaunda ile kampuni mpya ya kumilikiwa kwa ubia na Tanzania ambayo tutamiliki asilimia 16% ya shares, mnaweza kukuta kila kitu kimeishauzwa kwa Wachina!.

Taarifa yenyewe rasmi ni hii

PRESS RELEASES
Nyanzaga Project Update
06 Sep 2018
Further to the announcements made on 20 July 2018, the Tanzanian Fair Competition Commission (FCC) has now granted its approval for OreCorp Tanzania Limited (OreCorp Tanzania) to increase its interest in Nyanzaga Mining Company Limited (NMCL) to 51%. This move remains subject to: (i) the approval of the newly established Mining Commission, the application for which was lodged at the same time as the application for FCC approval; and (ii) the future payment of US$3 million to the Acacia Group.
In addition, members of the OreCorp Group have now entered into a completion agreement with Acacia and other members of the Acacia Group to allow OreCorp Tanzania to move to 100% ownership of NMCL, and thereby 100% ownership of the Nyanzaga Gold Project (Project). This move remains subject to: (i) the Tanzanian regulatory approvals referred to above; (ii) the grant of the Special Mining Licence (SML) in respect of the Project; and (iii) the making of a future payment of US$7 million. Following completion Acacia will retain a net smelter return production royalty over the Project, capped at US$15 million.
Both OreCorp and Acacia believe that a simplified ownership structure of NMCL is beneficial to the future development of the Project and would enable it to be best placed to provide significant benefits to Tanzania and all stakeholders.

Nyanzaga Project Update

© Copyright 2018 Acacia Mining plc. All rights reserved

Kama hawa jamaa hawajatulipa hata senti tano na sasa ndio wanaanza kuuza mali zao kwa asilimia 100%, hawa jamaa hawatakuja kweli kutuacha solemba?.

Msingi mkuu wa majadiliano kati ya Barrick na serikali yetu ni trust and transparency, yaani uwazi na kuaminiana, tayari kuna minong'ono, yale makontena ya makinikia, yamehamishwa mahali yalipokuwepo, isije ikawa yameondoka!.

Hitimisho.
Kwa vile Acacia ndio the determinant ya kila kitakachoamuliwa na mazungumzo yetu na Barrick, then serikali yetu iangazie kwa makini, kila kinachofanywa na Acacia, kukiangazia kina maanisha nini, what is the motive behind his mergers and acquisitions wakati tunapaswa kuunda kampuni mpya ya kugawana 50/50 ya faida. My sixth sense tells me kuwa kabla hatujafika huko, huku tutakuwa tumebakiwa na skeletons!.

Mungu Ibariki Tanzania!.
Paskali
Tutapata shida sana! Kishika uchumba hakuna, Noah hakuna na zaidi ya yote nasikia kuna kesi wametufungulia ambayo huenda tunakwenda kuwalipa zaidi ya T4. Mbwembwe za tume za maprofesa hazijatusaidia kitu. Tuliambiwa awali kuwa wale ni wezi lakini baadaye tukaambiwa wale ni wanaume wamekubali kutulipa! Tufwileee malafyale!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom