Je, ‘’15 minutes of fame’’ za Fatma Karume zimegharimu biashara za IMMMA Advocates na TLS?

Kwenye nchi zetu zinazoendelea huwezi kuepuka ukweli kuwa serikali ndio taasisi pekee ambayo matumizi yake ya pesa ndio kipato kikubwa kwa makampuni makubwa ya huduma na kwa mantiki hii huwezi kufanya kazi za uwakili ambazo zinahusu makampuni makubwa ya ndani na kimataifa ambayo mdawi wake mkubwa ni serikali halafu ukaanza kuishambulia serikali kisiasa ukitegemea mafanikio kibiashara. Ni lazima utapoteza moja au yote. Huu ni ukweli ambao wenye kujua umuhimu wa biashara zao za huduma wanaujua na huufanyia kazi.

IMMMA Advocates ni kampuni kubwa ambayo niya vigogo ndani ya CCM ambao mizizi yao iko pia serikalini na kwenye taasisi ya mahakama. Kwa mantiki hii hawawezi kukubali kampuni yao kugonganishwa kisiasa na serikali waziwazi.

Alichokuwa anafanya Fatma Karume hakina tofauti na kujipiga risasi mguuni bila kujua huku akishangiliwa na watu wanaodhani anachofanya ni kuwaburudisha kwenye mitandao huku kampuni ya IMMMA Advocates ikipata matatizo kibiashara.

Badala ya kutumia Urais wa TLS kama daraja la kuiunganisha IMMMA Advocates kibiashara badala yake ametumia kama uzio wa kuitenganisha na serikali. Hata Urais wake wa TLS umeifanya TLS kuwa mbali na taasisi ya mahakama badala ya kuwa karibu zaidi.

Washirika wenzake wamemuomba achague moja kati ya mawili kama anataka aendelee kuwa mshirika wa IMMMA Advocates. Kama anataka aendelee na uanaharakati kama Rais wa TLS au aachane na uanaharakati ndani ya TLS.

Kauli ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ilipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Urais wa Fatma Karume aliposema, ‘’Chama Cha Wanasheria Nchini (TLS) kuacha kujishirikisha na masuala ya kisiasa na uanaharakati na iwapo watakiuka hilo Mahakama haitowapa ushirikiano’’.

Kauli ya Jaji Mkuu ilihitimishwa pale ambapo kwa mara ya kwanza TLS hawakupewa nafasi ya kutoa hotuba kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Hiki kilikuwa ni kitendo cha kuwafungua macho wanachama wa TLS kuhusu mstakabali wake nchini kama mdau wa sheria. Hii ilipelekea hata jina lake kutopendekezwa na wanachama wa TLS kuwa mgombea Urais.

Yaliyomkuta Fatma Karume yanatoa angalizo kuwa huwezi kuukata mti alioukalia mwenyewe maana ukianguka unaanguka na wewe! Fatma alikuwa anakata mti wa IMMMA Advocates na TLS kwa kujua au bila kujua!

Kuna wengine watasema, ''hakuna mkate mgumu mbele ya chai'' hasa kama kuna mlaji!
Kuna watu wataanza kutokwa na povu hapa.
 
wekeni masihara pembeni;

Kuna muda hiyo kampuni ya uwakili ilishiriki kutunyonya sisi watanzania. .

Ila kwakua kwa sasa mirija imekatwa...

eti nao ghafla wanafahamu anuani zetu sisi wanyonge..

na kwa bahati mbaya sana ;

wapinzani wetu hawajitambui...

wanazoa kila uchafu
 
Kuna wana TLS hawapendi chama chao kinavyoendeshwa tangu Lissu awe Rais na sasa Fatma.

Kwa maana, TLS ya sasa imebeba taswira ya kisiasa na kiharakati kuliko kuwa huduma muhimu ya msaada wa kisheria kama ilivyokuwa awali.

Ndio maana hata zile kauli za Fatma kuhusu sakata la Ushoga, chama kiliingilia kati na kusema ni mawazo yake binafsi na sio msimamo wa TLS.

TLS ya sasa unaweza kudhani ni mpya yaani kumbe imekuwepo muda mrefu na kazi zilikuwa zinaenda kabla hakijatekwa na hawa kick masters..

Nisiwe adui kwa kutoa maoni yangu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom