JB: Mganda huyu ni nani na anafanya nini Tanzania?

very interesting ..... hapa kuna sintofahamu nyingi na za ajabu
 
Kinachonishangaza nijinsi Watanzania tulivyojaliwa kuficha siri hata za wageni wanaopiga "magumashi".........duuhh!!
 
Kuna jina limekuwa likirushwa rushwa kwenye mazungumzo juu ya raia mmoja wa Kiganda ambaye anakwenda kwa kutumia initials za "JB". Does anybody know who is he and what is he doing in Tanzania na kama in anyway shape or form anaweza kuwa ni tatizo kwa Tanzania?

Mwanakijiji habari yako haijakamilika kwa uwa inaacha maswali mengi kuliko majibu, na umeiandika katika lugha ya kijiweni kwa mimi nasikitika kuiita habari hiyo ni majungu na siko tayari kuchangia upuuzi huo zaidi ya kukuambia tumia lugha fasaha kuwasilisha usemacho kama hujui kiswahili andika hicho kiingereza chako na kama hujui kiingereza fasaha andika kiswahili fasaha.
 
Mzee Mwanakijiji,

Kwa ufupi huyu bwana ni mganda na alikuwa mwanajeshi wakatofautiana na Museveni akaja hapa Tanzania na kuishi kwa muda na badaye alikwenda Ulaya akafanya biashara zake mambo hayakwenda sawa na akarudi tena Tanzania na ndipo akapata mwanamke wa kihaya akamuoa na ndiye wanaye mpaka sasa.

Ana pesa nyingi sana ni mfanya biashara, hizi hbr ni kutoka kwa mtu wa ndani ya familia, na huo ndo ukweli
 
Last edited by a moderator:
Kwa mujibu wa mganda mmoja ni kwamba hizi investment za JB zipo nyuma ya wakubwa flani na kwamba hata jina si halisi ila huyu JB anatumika kuuficha ukweli, kwa mujibu wa huyu mganda ni kwamba herufi J ni ya jina la mke wa mkulu mmoja uganda na kwamba anawatumia ndugu hao ili kujificha.

Hizi ni rumours na si lazima ziwe na ukweli
 
Mwanakijiji habari yako haijakamilika kwa uwa inaacha maswali mengi kuliko majibu, na umeiandika katika lugha ya kijiweni kwa mimi nasikitika kuiita habari hiyo ni majungu na siko tayari kuchangia upuuzi huo zaidi ya kukuambia tumia lugha fasaha kuwasilisha usemacho kama hujui kiswahili andika hicho kiingereza chako na kama hujui kiingereza fasaha andika kiswahili fasaha.
Hapa ndipo ninapoukumbuka ule mfano maarufu wa Baba wa Taifa kuhusu mashoka na Misitu. Miti midogo ilipoingiwa hofu kwa kuyaona mashoka yakija, ile mikubwa ikauliza "Wenzetu" wapo? Bila "Wenzetu" kama wewe mnaotupiwa makombo wageni wasingeifanya hii nchi shamba la bibi.
 
Mwanakijiji habari yako haijakamilika kwa uwa inaacha maswali mengi kuliko majibu, na umeiandika katika lugha ya kijiweni kwa mimi nasikitika kuiita habari hiyo ni majungu na siko tayari kuchangia upuuzi huo zaidi ya kukuambia tumia lugha fasaha kuwasilisha usemacho kama hujui kiswahili andika hicho kiingereza chako na kama hujui kiingereza fasaha andika kiswahili fasaha.

Umechangia lakini!
 
Mimi simfahamu huyu. Bali napenda kukumbusha Mwanakijiji kuwa baada ya kukusanya taarifa uwe unatupa hitimisho. Nadhani unakumbuka juu swali kama hili juu ya yule Mfanyabiashara Maarufu wa Morogoro.

Tupe hitimisho lako kuhusu huyo mtu kama ni hatari kwa Taifa au la na pendekeza tufanye nini.

Pia kuna siku ulituonya juu ya kutumia aina fulani ya mtandao wa simu (provider) nchini (nadhani Voda?) lakini hutueleza shida ni nini. Kama great thinker naomba niwe naelezwa hitimisho ya mada kama hizo vinginevyo basi hatuna haja ya kukuna vichwa kumpa mtu taarifa halafu hatuelewi mwisho hizo taarifa ni za utafiti wa nini kwa ajili ya nani na sisi kubaki katika suspense!

Chonde chonde mwishoni nataka kuona setenso kama vile:

JB ni mnyonya damu watu hivyo kaeni kwa umakini au muepukeni au
JB ni mgeni mfanyabiashara asiye na mawaa kama tulivyofikiri n.k :smash:
 
Kwenye records za BRELA kuna makampuni kadhaa yenye majina yanayoanza na JB na makampuni hayo yamesajiliwa kuanzia mwaka 2007 ila sina uhakika kama yana uhusiano na huyo Mganda

60146JB VENTURE SOLUTIONS LIMITED27/04/2007
60259JB FLORA LIMITED08/05/2007
62598JB LAB MAINTENANCE LTD18/10/2007
66328JB TRANSPORTES AND TOURS OPERATORS CO LIMITED02/07/2008incorporation
66875JB FINANCIAL SUPPORT LIMITED04/08/2008
67500JB ELECTRONICS & GENERAL TRADERS CO. LIMITED16/09/2008incorporation
67801JB NTIRUGELEGWA CO. LIMITED07/10/2008incorporation
114918JB INDEPENDENT24/09/1997incorporation
115248JB MODERN ENTERPRISES27/10/1997incorporation
73419JB HOSPITALITY LIMITED28-Oct-09incorporation
78202JB ADVERTISE & PROMOTION CO. LIMITED26/08/2010incorporation
 
Mzee Mwanakijiji,

Kwa ufupi huyu bwana ni mganda na alikuwa mwanajeshi wakatofautiana na Museveni akaja hapa Tanzania na kuishi kwa muda na badaye alikwenda Ulaya akafanya biashara zake mambo hayakwenda sawa na akarudi tena Tanzania na ndipo akapata mwanamke wa kihaya akamuoa na ndiye wanaye mpaka sasa.

Ana pesa nyingi sana ni mfanya biashara, hizi hbr ni kutoka kwa mtu wa ndani ya familia, na huo ndo ukweli

Hapo penye red....Mhhhh
 
Hapa nilikuwa namtofautisha JB na wale Wafanyakazi lukuki waliopo nchini kinyume cha sheria!
Kuhusu Magumashi sina uhakika ila ukiangalia kasi ya kumiliki Chain stores na ile hotel iliyokuwa Paradise... lazima kutakuwa na namna!
shida yako ni kasi ya kumiliki ama uhalali wa umiliki?Inaonekana umeathiriwa na snail-pace attitude ya Kitanzania,ile ya mtanzania kununua kiwanja then anakaa miaka kumi ndio anaweka msingi.Waganda wanafanya kazi na wame-embrace ujasiriamali kwa moyo wa ujasiri na bidii.
 
JB ni janga kwa taifa hili....mpeni muda kidogo tu you will prove this..... mbali na hayo mambo ya down to earth ni mzinzi sana na anaharibu sana mabinti pale Quality Centre
Ujinga kama huu wako ndio janga halisi la kitaifa-watu kupenda uzushi au ku-conclude mambo bila hoja au ushahidi wowote!JB(ingawa simjui) ni janga la taifa kivipi?Halipi kodi?Yeye ndie anayefanya sisi tusifanye kazi na kuishia kuimba nyimbo za ufisadi na freemason?Kuna mtanzania amezuiliwa kufanya biashara Uganda?Tatizo letu ni elimu ya kukariri na kujibu mitihani ya darasani tu.Huu ndio utandawazi uliokariri darasani,watu wanazunguka dunia nzima kutafuta business opportunities.Acha JB afanye kazi huku sisi tukiendeleza porojo zetu za kuogopa kujiunga na EAC kwa sababu ya uvivu wetu.Unamwita JB malaya na kusahau kuwa kama ni umalaya si anaufanya na Watanzania wenzetu,kwa nini tusiwalaume hao watanzania wenzetu,let's deal with our own failures first.
 
Tatizo sisi Watanzania ni masikini sana halafu wengi wetu ni watumwa wa kiakili wamezoea lazima tajiri awe Mzungu au Muarabu.

Bob Justus Baguma ni tajiri mkumbwa sio Tanzania tu mpaka UK kwao Uganda pia ana hotel nyingi tu za kitalii, Bob Justus Baguma ni Mkurugenzi wa JB Beltont.

Uingereza kuna kampuni zake pia kuna ARMSTONE LIMITED, EORO-AFRO CONSUMERS LIMITED.

JB saizi ni mwenyekiti wa jumuiya ya waganda wanaoishi Tanzania, JB ni kichwa kaenda shule ana Masters Degree in business kasoma UK.

Huyu jamaa ni mtu makini sana.
 
Unaposoma comments za wachangiaji wa hii Thread unazidi kupata picha halisi ya elimu yetu na uwezo wa kufikiri.Mtu anaandika kuwa JB ni janga la taifa(huu nao umekuwa msemo ambao kila asiye na hoja anautumia kuficha utupu wake) bila kutoa sababu yoyote.Wengine wanadai Kasi ya JB inatisha,haya ni madhara ya watu kuzoea kasi ya kobe,kila kitu foleni,mipango kuchukua miaka mingi kuliko utendaji.Uvivu wetu unazidi kukua kwa kasi kwa hio wakija wageni wakaona nafasi za kukua kwa biashara zao hapa Tanzania tunaishia kwenye porojo zetu za kila siku ilhali ripoti zote za kimataifa zinaonesha kuwa tunaongoza kwa uzembe kwenye EAC.
 
Mzee Mwanakijiji,

Mr Justus Baguma, a Ugandan entrepreneur in Tanzania, owns the JB Belmont, Savannah and some shops at Quality Centre and has also been elected the chairman of the Ugandan Community in Tanzania.

He is a self-proclaimed self made man and attributes his success to hard work... Whether "hard work" means "trouble for Tanzania" I don't know....

Be careful! Sio kila utajiri ni safe made...wengine wako kwenye mission tofauti under the guise of being entrepreneurs.
 
Tatizo sisi Watanzania ni masikini sana halafu wengi wetu ni watumwa wa kiakili wamezoea lazima tajiri hawe Mzungu au Muarabu.

Bob Justus Baguma ni tajiri mkumbwa sio Tanzania tu mpaka UK kwao Uganda pia ana hotel nyingi tu za kitalii, Bob Justus Baguma ni Mkurugenzi wa JB Beltont.

Uingereza kuna kampuni zake pia kuna ARMSTONE LIMITED, EORO-AFRO CONSUMERS LIMITED.

JB saizi ni mwenyekiti wa jumuiya ya waganda wanaoishi Tanzania, JB ni kichwa kaenda shule ana Masters Degree in business kasoma UK.

Huyu jamaa ni mtu makini sana
.

Story za aina hii nzuri kweli kama watasimuliwa kina Obama kwenye mkutano wao wa G8. Kuwa tajiri sio tatizo na kwa kweli tunahitaji watu wenye uwezo wa kufanya biashara na kutengeneza mitaji na ajira. Lakini Tanzania ina watu wendawazimu sana. Mtu akishakuwa na hela basi asisemwe wala kuguswa hata kama hela zake zinapatikana pasipo uhalali. Sio busara kumuonea wala kumsingizia mtu. Ila penye ukweli lazima pia usemwe....nyinyi mliozoea kuimba sifa za matajiri na wenye hela endeleeni tu maana hata Akudo, Twanga pepeta, diamondo soundo wanaifanya kwa uastadi mkubwa kazi hiyo ya kuimbia wenye pesa mjini, kama kina Papaa Msofe na Ndama mtoto wa ng'ombe.
 
Back
Top Bottom