JayDee na Chuki Party | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JayDee na Chuki Party

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Silvano, Apr 1, 2010.

 1. Silvano

  Silvano Member

  #1
  Apr 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ndugu zangu mnaongeleaje kuhusu part hii kali nimeipata kupitia http://ladyjaydee.blogspot.com/ . Nadhani ni kali na haijawahi kutokea hebu someni:  Habari gani wapendwa.

  Nimepata wazo moja hivi ambalo ningependa kuwashirikisha, mara nyingi tumekuwa tukifanya party za kukusanyika marafiki, fans na watu wengine wa karibu.
  Lakini nimepata wazo tofauti, kuliko kukutana na watu wanaokupenda tu kila siku nimeona niwape nafasi na wengine pia ambao hawanipendi.

  Nataka kufanya Chuki Party nitagharamia kila kitu, kuanzia vinywaji, chakula mpaka usafiri wa kuwaleta na kuwarudisha watakaopenda kuhudhuria...na chochote wanachopenda kuvuta kasoro Bangi na vilevi visivyo halalishwa
  Venue pia mchague nyinyi, na mpendekeze pia ni nini mnahitaji kiwepo kwenye party hiyo.

  Pia ningependa mpendekeze tarehe na muda ambao mngependa party hiyo ifanyike kati ya Jumatatu, Jumanne au Jumatano.
  Maana kuanzia Alhamisi Sanya Sanya inaanza kwahiyo hakuna muda.

  Nimeona watu wanapata tabu sana kutuma msg na comments za matusi na kejeli, ambazo siwezi kuzi post kwakuwa hazina maana na wala haziwahusu wapenzi wengine wa blog hii...badala yake basi nimeamua kuwakutanisha na mimi live ili kila mtu atoe donge na dukuduku lake linalomsumbua juu yangu.... Nadhani pengine itawasaidia kufahamu yale wasioyafahamu na itawasaidia kupunguza maumivu na chuki waliyonayo dhidi yangu.


  Maanake kila siku ukikaa una mkasirikia mtu unakosa amani ya moyoni, nataka kukutana na nyinyi jamani/? Je!! Mko tayari kwa CHUKI PARTY??

  Wanaonipenda na fans, na ndugu hawaruhusiwi kwenye party hii.
  Hii ni kwa wale wasiopendezwa na mimi kuanzia, mavazi, sura yangu, swaga zangu na chochote nilicho nacho.


  Kushiriki party hii ni rahisi sana, niandikie sms kwenye 255 773 212 000 au nitumie e-mail: judyjaydee@yahoo.com

  Shughuli ni watu na watu ndio nyinyi, nawategemea sana

  with lots of love and respect to you all


  BintiMachozi a.k.a Comandoooooo
   
Loading...