Jay Moe atamba kusoma na Rais wa DRC Joseph Kabila

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
Jay.jpeg

Msanii wa Bongo Fleva, Jay Moe ameeleza changamoto alizokumbana nazo shule hadi kupelekea kutoa albamu ya Ulimwengu Ndio Mama, licha ya hiyo kuna vitu ambavyo anajivunia ikiwemo kusoma shule moja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila.

Rapper huyo amesema kutokana na kukulia katika maisha ya kishua hadi unafika wakati ambao anaenda boarding school alikuwa hajui kama kuna nyumba za udongo nchini zaidi ya kuziona kwenye movie za Vietnam.

Ameeleza kuwa wakati anaenda Mbeya kuanza form one mwaka 1993 ndipo alianza kuona nyumba za udongo kitu kilichomfanya kuanza kulia lakini baba yake na ndugu zake walipomueleza kuwa amekua hivyo hana budi kuachana na mambo ya kitoto na kupambana.

“Siku ya kwanza nilipofika Irambo (secondary) jamaa wameniibia begi la mamisosi, kwa hiyo kule ndipo nilipojifunza maisha kiasi kwamba nilipofika form three mzee wangu alitaka anihamishie Dar es Salaam lakini nikamwambi hapana mimi nabaki, nimeshazoea ingawa maisha ni magumu,” Jay Moe amekiambia kipindi cha The Play List cha Times FM.

“Kingine kinacho-inspire image mimi nimesoma na Joseph Kabila ambaye ni Rais wa Congo, nimesoma na Cesi, nimesoma na Clara ambao wote ni watoto wa mzee Kabila. Mimi nikiwa form two Jose ndio anamaliza form six na alikuwa kaka mkuu wa shule, kwa hiyo nilijifunza kama huna mama basi, kuna ulimwengu ambao utakufunza kama mama,” amesema Jay Moe.

By Peter Akaro
 
Shule gani?
 
Alikua hajui kama kuna nyumba za udongo..?uyu mmakonde kazaliwa na kukulia wapi aiseeee?
 
Joseph kabila amekulia mwananyamala maeneo ya garden pale so nikawaida katika maisha sababu hujui kesho ya mtu itakuwaje
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom