Jay Mo na Mwana FA walimpotosha Dj Nelly wakazima wimbo wangu Masqo wa "Nimepata Demu"

Tunapoongelea suala la kina joti kufanya comedy bila kuvaa nguo za kike au manguo na mandala ya ajabu ndo inabidi wajifunze kwa mtemi deo kisandu
Huyu jamaa ni level za kina dave chapelle anakuchekesha huku kavaa suti ya gucci na kunukia expensive perfume
aisee mtemi kisandu wewe ni comedian asilia,embu tutafutane weekend hii tukutane hata villa park kirumba tupate moja mbili tatu za baridi na samaki wa kuchoma
ha haha hahaha"" lakini namna ambavyo ameiunda hiyo story daaah lazima uamini aisee.. kitakachokufanya utilize walakini "!nikwakuwa muandishi wa habari yenyewe ni deo kisandu "... ila nikweli kwamba backyard rec.ilikuwa chini ya usimamizi wa mtoto wa mengi .. " etc
 
JAY MO na MWANA FA WALIMPOTOSHA DJ NELLY WA CLOUDS FM MWAKA 2003/2004 AKAGOMA KUNIPA PROMO WIMBO WANGU WA "NIMEPATA DEMU" LAKINI ROZI CHITARA(Radio One),SHEIZA (Eastafrica radio) NA NIKO TRACK(Times fm) WALIUPA PROMO WIMBO HUO.

Mimi Deogratius Kisandu ambaye jina langu la Kisanii ni "Masqo" Wimbo wangu wa "NIMEPATA DEMU" ambao nilimshirikisha BRATON(samwel Mbwana) nilifanyia Studio za Backyard Record zilizokuwa Namanga kona, Dar es Salaam wakati huo Studio ilikuwa chini ya mtoto wa Dkt.Reginald Mengi(Abel), Aliyenitengenezea BITI na Kuingiza VOKO alikuwa Prodyuza MARIJANI lakini aliyemalizia mixing alikuwa Prodyuza HINGI.

Baada ya wimbo huu kukamilika Mtangazaji wa Clouds fm Madam Vivian Ntilya wakati huo alinisisitiza sana kuupeleka Radioni lakini ilionekana alitaka kuupeleka Cloudfm lakini tukapewa taarifa kuwa Jay Mo analalamika kuwa wimbo huo wa MASQO unafanana na wimbo wake wa "KAMA UNATAKA DEMU" na pia unafanana na wimbo wa MWANA FA wa "MABINTI" hivyo kama wimbo wa Masqo ukitoka nyimbo zao zitaporomoka, hivyo kila mtangazaji aliyefika na kuusikiliza aliupenda sana lakini walipotaka kuuchukua walizuiwa.

Hata hivyo niliukomboa na kumpelekea Dj Nelly pale Cloud fm nikampa, aliposoma tu kasha akanambia "Wimbo wako ni mzuri tutausikiliza lakini wasiliana vizuri na Prodyuza wako" alivyosema tu hivyo nikajua nimegonga mwamba na wimbo huo ukawekwa kapuni. Nilibadili gia angani na kukwenda Radio One na kuonana na Mtangazaji Rozi Chitara na akanipokea na kuanza kuupa Promo wimbo wangu wa "NIMEPATA DEMU", baada ya hapo nilionana na Mtangazaji Sheiza wa East Africa Radio naye akaanza kunipa Promo kwa nguvu, ndipo nilipoingia Urafiki wa karibu na Dj Niko Track wa Times Fm radio ambaye naye alinisaidia kupata Promo kituoni kwake.

Wimbo huu ulizuwa gumzo kwa baadhi ya wasanii wakilalamika kuwa Jay Mo na MWana FA wamemuwekea Vikwazo Masqo(Deogratius Kisandu) ili asiinuke maana wimbo wake utafunika kama utasambaa vituo vingi vya radio, kimsingi mimi nilikuwa na puuza tu kila kitu na kuendelea kupambana ili kuinuka kimziki. Najua kama hayo yalikuwa ya kweli basi ulikuwa ni utoto ambao sasa tumekuwa watu wazima sana hakuna uhasama. PIa kuna gazeti kati ya Nipashe au Lete Raha waliwahi kuandika"Masqo Pungo" badala ya "Masqo" ilikuwa tu nimakosa madogo ya kiuchapaji, naomba kuweka sawa.

Ndimi: Deogratius nalimi Kisandu a.k.a MASQO
6 Desemba 2017
Duh..! Maskini huyu mwalimu namfananisha na nabii Tito

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom