JAWS OF THE FORMIDABLE DRAGON BRIDGE: Daraja muhimu la North Vietnam lililosumbua ndege vita (Fighter Jets) za Marekani kuvunja kwa miaka saba (7)

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
FORMIDABLE JAWS OF THE DRAGON BRIDGE: Daraja muhimu la North Vietnam lililosumbua ndege vita (Fighter Jets) za Marekani kuvunja kwa miaka saba (7).

images (18).jpeg


DRAGON'S JAW ni jina la utani la watu wa Vietname kwa daraja la Thanh Hóa. Wakati wa Vita vya Vietnam, wachambuzi wa masuala ya ujasusi wa CIA waliigundua kama moja ya malengo muhimu ya miundombinu yaliyoteuliwa kwa kushambuliwa kwa nguvu ya ndege vita (Air Force) ili kulivuruga kwani ilitoa msaada wa kusafirisha vifaa muhimu (logistical support) vya Vietnam ya Kaskazini kwenye juhudi zake za vita huko Vietnam ya Kusini.

Iliyoundwa kwa ustadi wa juu zaidi wakati wa kujengwa kabla ya vita, na ikizungukwa na mifumo madhubuti ya usalama wa anga (Air Defense Systems), jeshi la Vietnam ilifanikiwa kutetea na kulilinda daraja hili dhidi ya kupigwa kwa ndege vita kadhaa za Marekani kwa kutumia mabomu ya ufundi wa hali ya juu, na hivyo kuishinda nguvu ya anga ya Marekani na kuinyima mafanikio ambayo iliyapata katika mashambulizi mengine kwenye miundombinu muhimu wakati wa vita ile.

Waasi wa Viet Minh walikuwa wameharibu daraja la mwanzoni katika eneo hili mnamo mwaka wa 1945 wakati wa Vita vya Indochina kipindi cha utawala wa kikoloni wa Ufaransa. Wakati daraja la mbadala lilikamilishwa mnamo mwaka wa 1964, lilikuwa na urefu wa futi 540 na futi 50 juu ya mto.

images (10).jpeg


Katika futi 56 za upana, liliweza kubeba reli kuu ya kati pamoja na barabara mbili. Daraja hilo lilisimamishwa kwa nguvu na uimara sana ndani ya vilima vya juu ambavyo viliinuka kila upande wa mto, ambao uliongezea ugumu wa kufanya shambulio hapo darajani. Daraja lenyewe lilikuwa la chuma na zege tupu, na kati ya 1965 na 1968 Serikali ya Vietnam ya Kaskazini iliongeza zege zaidi pamoja na nguzo ngumu.

Matokeo yake sasa, jeshi la anga la Marekani lilihitajika kubuni na kutafuta njia mpya ya kupata ushindi wa vita. Majaribio na mbinu mpya za kupambana na silaha hatimaye yalisababisha kutengenezwa kwa bomu lililoongozwa na miale (Laser Guided Bombs). Miale hiyo ingeweza kupunguza stress na usumbufu kwa baadhi ya askari wa anga juu ya kupatikana kwa lengo (Target Acquisition), urushaji wa silaha, na kunusurika wakati wa mapambano kuwa muundo wa kipekee wa nguvu za kisasa za anga.

Kwa sababu ya umuhimu wake na hali yake ya kimkakati kwenye njia za usambazaji kwenye uwanja wa mapigano kando ya DMZ (Demilitarized Zone) na kwa Viet Cong huko Vietnam Kusini, Daraja la Dragon Jaw lilikuwa lengo kuu na lilitambuliwa kama hivyo na askari wa North Vietnam ambao walilinda eneo hilo kwa ulinzi wa mizinga ya kutungulia ndege ambayo haijawahi kuwekwa nje ya miji ya Hanoi na Haiphong.

images (11).jpeg


Licha ya mashambulio ya awali ya ndege vita aina ya F-105s kutoka ngome moja wapo ya jeshi la Marekani nchini Thailand, daraja ambalo lilikuwa limeundwa kwa ufundi wa hali ya juu zaidi, lilikataa kuvunjika. Shambulio moja la USAF (United States Air Force) lilikuwa na ndege takriban 79 nyakati tofauti zilizotumika wakati mmoja na bado daraja lilisimama imara.

Mwishowe mwaka huo huo Maabara ya Ugunduzi wa Silaha huko walikuwa wakifanya utafiti juu ya kutumia silaha zilizolipuka sana (Highly Explosive Devices) ambazo zililenga nguvu zao katika eneo la mashambulizi. Wakuu wa jeshi la Kikosi cha anga cha Pasific kinachoendesha kampeni ya mashambulizi ya anga ya ndege za Marekani huko Vietnam waliarifiwa juu ya nguvu inayowezekana ya uharibifu wa silaha hizi mpya, lakini zinaweza kubebwa tu ndege za kubebea mizigo aina ya Lockheed C-130 Hercules.

Kwa kuwa Anti Aircraft Defense Systems kwenye daraja la Dragon Jaw ilikuwa kubwa sana na imara sana, mpango uliandaliwa wa ndege aina ya C-130s kuangusha silaha kwenye mto na kuzifanya zielee chini ya daraja kisha kulipuka.

images (19).jpeg


Marubani kadhaa wenye uzoefu walichaguliwa kutoka 314th Troop Carrier. Kikosi kimoja kiliongozwa na Major Richard Remers na wafanyakazi wengine wakiongozwa na Major Thomas Case, wafanyakazi wote kutoka Kikosi cha 61st Troop Carrier Squadron.

Mnamo mwezi Mei 30, mwaka wa 1966, kikosi cha Remer waliondoka wa kwanza na ndege ya C-130E kutoka Da Nang AB mara tu baada ya saa sita usiku. Wakiwa na kikundi cha watu saba tu, walipaa na ndege kwa umbali wa futi 100 juu ya Bahari ya china ya kusini na kisha wakageuka kuelekea eneo la lililolengwa, huku wakiendelea kubaki umbali wa futi 100 juu. Kulikuwa na "navigators" wawili ndani ya ndege ya kikosi cha major Remers na kulikuwa na maeneo mawili yaliyochaguliwa ya kudondoshea mabomu kutoka kwenye Daraja la Dragon Jaw.

Eneo la kwanza ilikuwa umbali wa miles 2 na ya pili ilikuwa umbali wa kama mile moja tu kutoka mtoni. Baada ya kufikia eneo la kwanza na kutokutana na upinzani wowote wa mizinga ya ndege, Remer akaelekea kwenye eneo linalofuata ya kuangushia bomu. Ghafla mizinga ya kutungulia ndege vita ikaanza kushambulia kwenye bonde la mto lakini walifanikiwa kuangusha silaha zao tano kwenye mto na wakaruka haraka sana kurudi Da Nang, mara hii wakiruka chini ya mita 100.

images (20).jpeg


Picha za upelelezi za siku iliyofuata zilionyesha daraja bado lilisimama imara sana hivyo usiku huo, misheni ya pili iliyoongozwa na Meja Case iliondoka zaidi ya saa moja baada ya saa sita usiku kutoka Da Nang. Kama ilivyokuwa kwa mission ya usiku uliopita na Major Remer, ndege aina ya F-4s zilifanya mashambulizi kwa ubadilishaji na kukwepakwepa katika eneo hilo na mmoja wa marubani aliripoti kuona mashambulizi mazito ya mizinga ya ndege na vimulimuli vikubwa karibu dakika 2 kabla ya eneo la kudondoshea mabomu.

images (17).jpeg


Kikosi cha Major Case hakikuwahi kusikika tena na haikuwa hivyo hata baada ya vita kumalizika hadi siku ambapo eneo la ajali ya Hercules hatimaye iligundulika na uchimbaji ukafanyika.

Iligundulika baadaye kwamba mabomu maalum yalilipuka chini ya daraja kama yalivyoundwa, lakini walipungukiwa na nguvu ya kutosha kuangushadaraja Dragon Jaw. Mission haikufanikiwa hadi hapo mwaka wa 1972 ndege vita aina ya F-4 Phantoms ikiangusha mabomu mapya - yanayoongozwa na miale - Laser Guided Bombs - (LGBs) ilifanikiwa hatimaye kuangusha daraja la DRAGON JAW.

images (9).jpeg


OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hakuna shirika liitwalo Gazprom Neft ila kuna mashirika haya, Gazprom ambalo ni shirika la uchakataji na usambazaji gas Urusi na Ulaya pia Roseneft ni shirika la mafuta, haya yote yanamilikiwa na Serikali ya Urusi
 
Hakuna shirika liitwalo Gazprom Neft ila kuna mashirika haya, Gazprom ambalo ni shirika la uchakataji na usambazaji gas Urusi na Ulaya pia Roseneft ni shirika la mafuta, haya yote yanamilikiwa na Serikali ya Urusi
kweli
 
Back
Top Bottom