Jasusi la Trump liliishi Tanzania/Raia Mwema, Februari 12-18, 2020

Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
2,055
3,239
BARAZANI

Jasusi la Trump liliishi Tanzania

Na Ahmed Rajab

Mwishoni mwa mwezi uliopita kulizuka msisimko mkubwa katika duru za kijasusi za mataifa kadhaa, hasa ya Mashariki ya Kati na Urusi.

Msisimko huo ulizivaa ghafla duru hizo baada ya wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan kutangaza kwamba waliitungua na kuiangusha ndege ya kivita ya Marekani aina ya Bombadier/Northrop Grumman E-11A.

Ndege hiyo, iliyokuwa ikitumiwa na shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), ilikuwa ikifanya kazi kama jukwaa la mawasiliano na upelelezi. Ikiwa angani ndege hiyo ilikuwa na uwezo wa kuyanasa mawasiliano ya aina tofauti toka ya simu, baruapepe na mengineyo.

Kwa hivyo ilipoangushwa wapiganaji wa Taliban walidai kwamba walizitia mikononi nyaraka kadhaa za siri zilizonusurika na moto pamoja na zana za kijasusi za Wamarekani.

Picha zilizosambazwa na Taliban kwenye mitandao ya kijamii zilionesha ndege ya aina hiyo ya Bombadier iliyokuwa ikiteketea. Pia zilionesha maiti walioteketea pamoja na hizo nyaraka zilizonusurika na moto.

Wapiganaji hao wa Taliban wanasema waliitungua ndege hiyo katika eneo la mji wa Ghazni nchini Afghanistan mnamo Januari 27. Hakuna aliyebisha kwamba ndege hiyo ilianguka.

Swali ni kuwa jee, ni kweli ilipopolewa ikiwa angani na wapiganaji wa Taliban au kulikuwa jengine lililosababisha ikaanguka?

Baada ya kimya cha saa kadhaa hatimaye jeshi la Marekani lilikiri na kuthibitisha kwamba kweli ndege yake ilianguka Afghanistan.

Lakini papo hapo Marekani ikakanusha kwamba ndege hiyo iliangushwa, ikidai kwamba ilianguka kwa sababu mtambo wake mmoja uliharibika.

Wataalamu wa ajali za ndege wanakubaliana na Wizara ya Ulinzi ya Marekani kwamba ndege hiyo haikutunguliwa ikiwa angani lakini ilianza kuwaka moto na kuteketea ilipotua ardhini. Inavyoonekana ni kwamba kulitokea hitilafu Fulani katika mitambo ya ndege na rubani akalazimika kutua kwa dharura.

Swali jingine nyeti lililoibuka hapo ni idadi ya abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo na walikuwa ni akina nani. Swali hilo limezusha utata mkubwa.

Wapiganaji wa Taliban wanasema kwamba walikuta maiti sita kwenye eneo lililotokea ajali hiyo. Marekani, kwa upande wake, inakanusha kwamba ndege hiyo ilikuwa na idadi hiyo ya abiria.

Zilipopindukia saa 48 baada ya kuanguka ndege hiyo wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema kwamba abiria wa ndege hiyo walikuwa wawili tu, wote wakiwa wanajeshi wa Kimarekani.

Hata hivyo, si watu wengi walioyaamini maelezo yote hayo yaliyotolewa na serikali ya Marekani kwa vile serikali hiyo haiaminiki. Imezoea ama kusema uongo au kuyaficha yaliyo ya kweli, hususan yanapohusu mambo ya kijeshi au njama zake Marekani katika nchi za nje.

Badala yake watu wamekuwa wakiyakimbilia kwa kasi maelezo yaliyotolewa na Irani pamoja na vyombo vya habari vya Urusi.

Maelezo hayo ndiyo yaliyokuwa yakiwasisimua wenye kufuatilia mchuano baina ya Marekani na Irani katika medani za kijasusi na za kivita za Mashariki ya Kati.

Irani imekuwa ikidai kwamba mmoja wa waliofariki katika ajali hiyo ya ndege lilikuwa jasusi kubwa sana la Marekani lenye kuhusudiwa na mijasusi mingine mikubwa ya kimataifa.

Jasusi anayetajwa ni Michael D’Andrea wa CIA. Kama ni kweli jasusi huyo alifariki katika ajali hiyo basi kifo chake ni pigo kubwa kwa Rais Donald Trump wa Marekani.

D’Andrea ni mtu muhimu kwa siasa za Trump za Mashariki ya Kati. Juni 2, 2017 Trump alimteua aongoze na kusimamia njama za Marekani dhidi ya Irani.

Ndani ya shirika la ujasusi la CIA D’Andrea anajulikana kwa lakabu ya “Ayatollah Mike”. Wengine humuita “Undertaker”, yaani mtayarishaji mazishi.

Jasusi huyo ni Mwislamu. Mkewe Faridah Currimjeeh ni mzawa wa Mauritius, aliyemzidi mumewe kwa umri kwa miaka kumi. Ukoo wa mkewe ni wa kitajiri na una asili ya Gujarat, India.

D’Andrea alianza kazi zake za ujasusi nje ya Marekani mwaka 1979 alipoteuliwa kuwa mwanadiplomasia. katika ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Kutokana na shughuli zake za kijasusi D’Andrea amekuwa akiwafahamu vizuri baadhi ya wanasiasa wa Tanzania na alifanya ujasusi mkubwa alipokuwa akiishi Dar es Salaam, akiwa karibu na Watanzania kadhaa wenye ushawishi nchini.

Alipokuwa anafanya kazi Tanzania ndipo alipopata fursa ya kukutana na Faridah.

D’Andrea alisilimu ili aweze kumuoa. Kwa sababu alikuwa Mwislamu ndipo wenzake kazini walipoanza kumtania na kumwita ‘Ayatollah’ Mike, lakabu ambayo imemselelea.

D’Andrea aliwahi pia kuwa mkuu wa kituo cha CIA, jijini Cairo, Misri. Baadaye alipelekwa Baghdad, Iraq.

Ingawa ni Mwislamu alipanga mauaji ya maelfu Waislamu wenzake waliokuwa wanaharakati wa Kiislamu alioamini kuwa ni magaidi.

Dhamana zake zimemfanya atambe kama mwewe juu ya anga za Irani, Iraqi, Syria, Pakistani na Afghanistani. Ni muuaji mwenye kutafahari kwa kazi yake. Mikono yake imejaa damu za wengi. Kwake kuua ni kama mchezo.

Hivi sasa tunajua kwamba yeye ndiye aliyemuua Luteni-Jenerali Qassem Solaimani, kamanda mkuu wa Irani, aliyeuliwa katika shambulio la droni jijini Baghdad Januari 3, mwaka huu.

Pamoja naye pia aliuawa Abu Mahdi al Muhandis, kaimu mkuu wa majeshi ya mgambo ya Hashd al Shaabi ambayo ni sehemu ya majeshi ya serikali ya Iraq.

Mnamo mwaka 2008, D’Andrea alimuua Imad al Mughniyeh, aliyekuwa wa pili katika uongozi wa jeshi la wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon. Mughniyeh pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa kundi la Islamic Jihad la Lebanon.

Akishirikiana na Idara ya ujasusi ya Israel, Mossad, D’Andrea alimuua Mughniyeh kwa bomu lililotegwa ndani ya gari wakati Mughney alipokuwa akirudi nyumbani kwa miguu jijini Damascus, Syria. Wapiganaji wa Hezbollah wanayasaidia majeshi ya serikali ya Bashar al Assad huko Syria.

Inasemekana kwamba D’Andrade karibuni alihusika na mauaji ya watu 300 waliokuwa wakiandamana Baghdad.

Watu waliofanya kazi naye, wanasema kwamba yeye D’Andrea ndiye aliongoza msako wa Osama bin Laden nchini Pakistani.

Na, akiwa Washington, ni yeye aliyeongoza mauaji ya bin Laden, aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa magaidi wa kimataifa wa al Qa‘eda.

Mashambulizi mengi ya Marekani nje ya nchi hiyo yanayotumia droni, yaani zile ndege zisizo na rubani, yamekuwa yakiongozwa na kusimamia na D’Andrea.

Kwa hivyo, ni yeye aliyekuwa akiongoza mauaji ya wanaoshukiwa kuwa magaidi nchini Afghanistani na katika nchi za Kiarabu zikiwa pamoja na Iraq, Syria na Yemen.

Wenye kumjua wanasema D’Andrea ana macho makali, ni tipwatipwa, kishtobeshtobe hivi, ingawa amekonda kidogo katika miaka ya karibuni.

Wanaongeza kusema kwamba anavuta sigara kama Giriki, moja baada ya moja. Anasifika pia kwamba ni mchapakazi ambaye siku nyingine hulala ofisini mwake anakoweka kitanda.

Juu ya hayo, inavyoonyesha ni kwamba “Ayatollah” Mike si mtu mwenye kupendwa na wenzake wengi. Baadhi yao wanalalamika kwamba heshi kununa na kuvimbisha mashavu.

Tunavyoyaandika makala haya Wamarekani hawakuthibitisha iwapo D’Andrea amefariki au la ingawa habari za kifo chake zimekuwa zikizunguka kwa kasi katika duru za kijasusi za Irani na Urusi.

Ikiwa ripoti hizo si za kweli basi huenda zikawa sehemu ya mkakati wa Irani wa kupambana na Marekani kisaikolojia.

Baruapepe: aamahmedrajab@icloud.com; Twitter: @ahmedrajab

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo alikuwa afisa wa ubalozi wa Marekani tanzania haina shida hata sisi mbona tunao waambata wa kijeshi kwenye balozi zetu na inaruhusiwa kimataifa sababu ubalozi ni nchi hivyo kuwa na maafisa Usalama was wa ubalozi ruksa

Si tu aliishi Tanzania huyo jasusi lakini alioa Tanzania mtanzania mwenzetu mtoto wa Karimjee aliyetupa ukumbi wa Karimjee hivyo huyo jasusi aliyeuawa Ni shemeji yetu watanzania .

Watanzania tuwaombe wamarekani watupe silaha tukawatwange Taliban kulipa kisasi kwa kitendo chao Cha kutuulia shemeji yetu
 
Mnapenda kuomba omba sana alafu hao hao wakiwakosoa kwa maovu yenu mnawaita mabeberu.

Ammed Rajab Je umebakiza viporo vya kande iliyochacha uliyoiparamia na kushindilia?
 
Lakini baada ya ndege kupigw,Kuna watu wawili walitoka humo wazima na Taliban walikuwa wakiwasaka,hatima yao yaweza kuwa walitekwa,marekani waliokoa maiti mbili,,maiti mbili hazijulikani ziko mikononi mwa talebani ama lah,
Je jasusi Mike Ni miongoni mwa hizo maiti ama alitekwa mzima baada ya ajali,
Baada ya tukio Hilo,Trump na Taleban wamefanya mazungumzo ya amani na nasikia wameelewana,Sasa Hapo utajaza mwenyewe kichwani Nini hasa kimejiri
 
Afisa wa ubalozi mwaka 1979 hawezi kuwa leo hii miaka 40 kazini bado ye combat soldier anatungua, anatunguliwa, anapigana ngumi kavu, mabomu ya mkono, kujificha, kuhama hama from one vita to the next...

kwanza hakunaga Mjeshi wa USA anaenda theater zaidi ya moja mbili....
 
Hv sasa Taleban na Warusi ni dugu moja. Sasa ameingia na muirani ndio kunazidi kunoga..wazayuni na merekani inabidi wajizatiti zaidi.
 
Back
Top Bottom