Rusumo one
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 3,020
- 3,504
Imetulia
Riwaya : Mpango wa Congo
Sehemu ya tatu
Alitamani kukisoma kile kikaratasi,ila akajionya kutokufanya kosa lolote katika wakati kama ule ambao hajui wapi anapelekwa.
*****
Gari ilizidi kuacha mji wa Ivuba na haikufuata barabara kuu ya Julius Nyerere kuelekea katikati ya Mji wa Kinshasa au barabara ya Nailogi kuelekea kituo kikuu cha polisi Ivuba,badala yake ikawa inaelekea katikati ya mji unaokaliwa na waasi wa ADF(Allied Democratic Forces) hiki ni kikosi cha waasi kinachoshambulia mara kwa mara nchi ya Congo japo hujipambanua kama kikosi kinachompinga Rais wa Uganda.
Karandinga lilizidi kuiacha Ivuba na Kinshasa na sasa uelekeo wake ulikuwa ni kaskazini mwa Congo katika Jimbo la Kivu.
Safari ilikuwa ni ya mwendo kasi sana na muda wote watu wale walikuwa kimya kabisa.
Wakiwa wameanza kutoka kwenye makazi ya watu mara gari ikasimama gafla na haraka Sajini Kebu akateremka kisha akaja nyuma ya karandinga lile,hakusema kitu akatoa ishara fulani na mmoja kati ya askari akashuka chini na kwenda kumsikiliza Sajini.
Honda alikuwa akiwatizama kwa makini sana na aliona wakiteta jambo huku wakimtizama kwa macho ya wizi wizi.
Macho yao na maongezi yao yakamtia shaka ila akajipa muda wa maamuzi kwa sababu hadi muda huo hakujua nini alitakiwa afanye na pia hakujua kwa nini mauaji yamewaandama katika ofisi yao,hivyo alihitaji kujua zaidi ila alikwamishwa na aina ya watu waliomzunguka.
Sajini Kebu aliendelea kuteta na yule askari aliemuita huku kila mara wakiendelea kumtazama Honda.
Baada ya mazungumzo yao kuisha ndani ya dakika tano,Sajini Kebu na yule askari wajongea kwenye lile karandinga na walipolifikia,tofauti na matarajio ya Honda kuwa Sajini arudi kuvunja kishoka kule mbele na safari iendelee,ilikuwa tofauti badala yake wote wawili wakaja hadi nyuma ya karandinga na kisha wakapeana ishara na wale waliokuwa ndani ya karandinga lile kisha wakateremka wote wanne waliokuwa wamesalia na hapo ndipo Honda akachezesha akili yake kuona lipi rahisi kulifanya kwa wakati huo na akapata wazo moja tu,kukisoma kikaratasi alichokichukua kwa marehemu Bulembo.
Akakisoma ila hakuelewa kilichoandikwa kwa uharaka ule,akakariri kilichoandikwa mana hakutaka kuamini kilikuwa kimeandikwa bahati mbaya,na kama ni bahati mbaya inamaana gani kufichwa kwenye unyayo wa miguu na kufunikwa na soksi?
Mana ipo!!
Akarudia tena kukisoma.
“142BOULEVARD DU JUIN
B. P. 1612
KINSHASA CONGO (81).”
Alipohakikisha kilichokuwa kimeandikwa kimemkaa kichwani,akakitafuna haraka sana kile kikaratasi na kukimeza.
Kitendo hiki kilifanyika ndani ya nusu dakika tu kiasi kwamba hata wale askari licha ya kuendelea kumtazama hawakufanikiwa kuona uharaka wa kitendo kile.
Wajanja walikutana na mjanja!!.
Dakika mbili badae askari watatu walipanda kwenye karandinga na bila kumsemesha wawili wakamfuata na kunyanyua juu kimabavu,nusura wambwage chini kisha kwa mbwembwe wakamsukuma nje ya karandinga nae akatua chini kwa mbwembwe zile zile bila kuumia na ilikuwa rahisi kwake mana walikuwa hawajafanya jitihada zozote kumfunga.
Kitendo chake cha kutoanguka kikawa kama kimewatia hasira,wale wawili waliokuwa wamebaki chini wakampokea kwa kipigo kizito bila kujali anakwepa au la.
Kipigo alichopewa Honda ndani ya dakika tano kilitosha kumuacha bila nguvu za kusimama na hapo ndipo akagundua alikuwa anapigwa na askari wote watano isipokuwa Sajini Kebu,ambae muda wote alikuwa kimya akishuhudia vijana wake wakimsulubu mfanyakazi yule wa ubalozi wa Tanzania nchini Congo.
Sajini Kebu alipiga hatua moja na kufika pale alipokuwa Honda akitweta kwa maumivu,akamwinamia na kumshika ukosi wa shati lake kisha akamvuta kwa nguvu na kufanya nyuso zao zitazamane kwa karibu zaidi na bila kusema kitu Sajini Kebu akamshushia kichwa kizito Honda na kumuacha akiwa na nundu kwenye paji la uso huku akijibwaga chini kama mzigo ulioozesha matunda.
Honda alipoanguka akafanya jitihada za kunyanyuka na hapo akaona Sajini Kebu anamfuata tena kwa gadhabu na bila kusema kitu akawahi kuushika mkoba uliokuwa ukininginia shingoni Honda.
Honda hakutaka kukubali kizembe,nae akajitutumua kumdhibiti Sajini Kebu asichukue ule mkoba.
Dhamira yake ya kuulinda ule mkoba ukagonga mwamba bada ya mmoja wa askari wale kumchapa teke la kifua na kumyanyua juu kisha kubwagwa chini kwa uzito wa teke lile na hapo askari mwingine akaudaka ule mkoba na kuutoa shingoni kwa Honda.
Honda hakuwa na la kufanya akabaki akitweta kwa maumivu huku akipanga namna ya kuwadhibiti watu wale ambao tayari walionekana si wema kabisa.
Baada ya Sajini Kebu na wenzie kuona wamemdhibiti Honda; akauchukua mkoba ule na kuanza kuukagua kwa umakini sana