Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

RIWAYA : MPANGO WA CONGO

SEHEMU YA 28


*****

Sundi alirejea nyumbani kwake jua likiwa linaelekea kuwa la utosi.

Alifanya haraka haraka na kuelekea jikoni kupika chakula.

Alipokwisha kupika alihitaji kwenda kufungua na kusafisha majeraha ya Salomoni.

Alivaa mavazi maalumu na kuvaa kitambaa maalumu chenye kamba zilizoenda kushika masikio huku kikiwa kimeziba mdomo na pua.

Sundi alifunua mapazia yaliokuwa yamekizunguka kitanda alicholalia Solomoni Bukaba.


Alikuta Solomoni akiwa ameshazinduka kutoka usingizini.

"Wajisikiaje mpenzi!" aliuliza Sundi huku akimtizama Solomoni usoni.

Macho yao yalipogongana yaliongea Lugha ya upendo wa hali ya juu.

Walipendana kiukweli.

"Naendelea vyema hivi sasa mpenzi wangu" alijibu Solomoni kwa uchovu.


"mmh pole,ngoja nikusafishe ili uendelee kupumzika" alisema Sundi huku akimwanamia Solomoni.

Macho yao yaligongana tena.

Solomoni aliona kitu.
Kitu hicho ndicho alichokiona siku anavamiwa ndani kwake.

Macho!!

Uangaliaji ule ulifanana sawasawa na ule alioangaliwa na mwanamke aliekuwa amevaa kininja.

Macho yalikuwa ni yale yale.

Alikumbuka sawia.
.

Akajikaza bila kuuliza hilo jambo.

Sundi aliendelea kumshugulikia Solomoni.

Alimaliza kumsafisha majeraha kisha akavua mavazi aliokuwa amevaa na kuyatundika mle chumbani kisha akamuomba Solomoni aende sebuleni kwa ajili ya chakula.

Solomoni aliamka kivivu na kwenda sebuleni.

Dakika kadhaa badae walikuwa wanakula chakula kitamu alichopika Sundi huku kila mara Sundi akimsaidia Solomoni kumlisha.

Walikuwa wakitaniana hapa na pale ili mradi kila mtu anaonesha kumjali mwenzie.

Walipomaliza kula walielekea bafuni ambako Sundi alimwogesha Solomoni huku wakitaniana hapa na pale huko bafuni.

Walimaliza kuogeshana wakaelekea chumbani na kujilaza kitandani.

"Mpenzi sijakuuliza kilichokupata jana mana niliona ulikuwa hujiwezi kabisa" alisema Sundi.

"Kwani hujasoma magazeti leo!? Nyumba yangu iliungua moto ila kabla nilivamiwa na watu walionishambulia namna hii kama unavyoona" alijibu Solomoni huku akimtizama Sundi usoni.

Sundi alitazama pembeni.

"hao watu walisema wanataka nini kwako?" aliuliza Sundi.

"Hawakusema wanachotaka" alijibu Solomoni alijibu huku akiwa bado anamtazama usoni.


Sundi alikaa kimya kidogo kisha akamchumu midomoni na kumpa ulimi Solomoni ambae nae aliupokea na wakagandana huku mikono yao ikitalii kwenye miili yao.

"Mmh unaumwa Solo wangu, tuishie hapa" alisema Sundi huku akijinasua Mikononi mwa Solomoni.

Kabla Solomoni hajasema lolote kengele ikalia.

Wakaangaliana.

Kengele ikaendelea kulia kwa fujo.

Sundi akatupa kanga aliokuwa amevaa,harakaharaka akavaa suruali aliokota chini na shati pana jeupe hakujali kuvaa hata chupi akaenda kufungua mlango.

Alipigwa na butwaa!!

"Mbona nyinyi leo mnamabalaa hivi" alisema na mtu aliekuwa getini.

"Mambo yanazidi kuwa mabaya tu" alijibu mtu aliekuwa getini.

"Duh afu niliwambiaje kuingia hapa kabla hatujawasiliana?" alihoji Sundi huku akifungua geti.

Alimfungulia Mwasu.

Mwasu alikuwa anamajeraha mwili mzima ya kuchanika chanika hasa usoni.

Haraka akapelekwa kwenye chumba kilichokuwa na vifaa tiba na kuanza kuhudumiwa.

Huduma ilichukua si zaidi ya saa mbili tayari majeraha yalikuwa yamesafishwa na kushonwa vizuri.


Hakuwa na majeraha makubwa sana hivyo akawa yupo timamu kimwili.

Walitoka kukaa sebuleni.

Walimkuta Solomoni akiwa ametulia akitazama runinga.

Mwasu akamtazama Sundi.

Sundi akatoa ishara ya kuwa asijali.

Wakaenda kukaa wote sebuleni huku Mwasu akipeana salamu na Solomoni.


Kitu ambacho Sundi alikijua na Mwasu hakujua kama Sundi anajua ni kuwa katika mipango yao endapo akitokea mtu hatarishi wa kushugulikiwa basi picha yake husambazwa kwa wote na akishakufa pia taarifa hufika kwa wote.

Hivyo Mwasu alishangaa sana kumkuta Solomoni nyumbani kwa Sundi.

Alimchukulia Sundi kama ni msaliti kati yao.

Akapanda kufanya jambo.


Waliendelea kuangalia runinga huku wakisemezana hili na lile.

Mwasu akaomba kutoka nje kidogo akapunge upepo kwa madai amechoka kukaa na majeraha yalimuuma.

Alikubaliwa huku Sundi akijua ni nini Mwasu anaenda kufanya huko nje.

Hakutaka alilowaza litokee.

Mwasu alipofika nje tu akatoa simu yake harakaharaka akatafuta namba za Elchapo ili apige.

Ni wakati simu yake inaita ndipo akajikuta yupo chini bila kupenda.

Sundi alikuwa amempiga teke la mgongoni.

Ngumi zikapangwa na watu walianza kupigana vita ya hatari.

Solomoni Bukaba akisikia vishindo huko nje,mwanzo alipotezea lakini vishindo viliongezeka.

Nae akatoka.


Alijikuta akishuhudia mpambano safi wa wanawake wanaojua vizuri mchezo wa ngumi.

Sundi alikuwa anacheka ili kumgadhabisha Mwasu.

Kicheko chake kilielea vyema kwenye ngome za masikio ya Solomoni.

Alikumbuka kicheko kile.

Ni cha yule yule mwanamke aliemvamia usiku wa balaa kwake.

Ebana eeh!

"Sundi ni nani na anashirikiana na nani!?" alijiuliza Solomoni.

Ni hadi pale alipoona Mwasu akichomoa kisu kutoka maungoni mwake na kwa ustadi wa hali ya juu akakirusha kumwendea Sundi. Na Sundi nae kwa wepesi wa ajabu akajikunja na kisu kikampita sentimita chache tu.

Solomoni hakujua kama Sundi wake laini laini anaweza kuzichapa kiasi kile.

Ilikuwa ni ajabu ila ndivyo ilikuwa.

Sundi alienda juu kama nyani na aliporudi akaachia teke safi lililoishia shingoni kwa Mwasu na kumsambaratisha chini kama mzigo.

Sundi aliona kumwachia Mwasu ni kujizika zaidi yeye hivyo akachomoa bastola ambayo Solomoni hakujua ilitokea wapi mana Sundi alivaa wakati yeye akiwepo na hakuiona.

Hatari hii.

Kisha akashuhudia Sundi akiachia risasi sita bila huruma ambazo zote zilijaa kifuani kwa Mwasu na kumwacha akiwa hana uhai.

"Why!!" aliuliza Solomoni baada ya kuona Sundi amegeuka na kumnyooshea bastola yeye.

Sundi alitamani apasue kichwa cha Solomoni ila nguvu ya mapendo ilizidi utimamu wa akili.

Akajikuta akishusha silaha chini.

"Tuondoke hapa hakutufai" alisema Sandi huku akiishindilia risasi simu ya Mwasu iliokuwa chini.

Iliwabidi kuondoka eneo lile.

Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia - JamiiForums
Aiseeh...mambo ni mazito
 
SASA MZIGO HUU NAO UMESHUKA BEI HADI TSH 500/=

RAHA ILIOJE KUSOMA UHONDO HUU KWA JERO TU.

TUMA HAPA 0758573660 KISHA NITUMIE UJUMBE KWA 0658564341 WHATSAP.

AU UNAWEZA PIA KUTUMA HAPA 0624155629.
NAMBA ZOTE MAJINA NI BAHATI MWAMBA.

KARIBU
 
SASA MZIGO HUU NAO UMESHUKA BEI HADI TSH 500/=

RAHA ILIOJE KUSOMA UHONDO HUU KWA JERO TU.

TUMA HAPA 0758573660 KISHA NITUMIE UJUMBE KWA 0658564341 WHATSAP.

AU UNAWEZA PIA KUTUMA HAPA 0624155629.
NAMBA ZOTE MAJINA NI BAHATI MWAMBA.

KARIBU
Nikituma say buku 2 ntapata story yote au kipande tu?
 
Kama umewahi kununua riwaya kwangu, Tafadhalini, Wasiliana nami whatsapp kwa 0658564341
 
RIWAYA: MPANGO WA KONGO

NA, BAHATI MWAMBA

SIMU: 0758573660.


1
MAUAJI

Ilikuwa ni ndani ya majengo ya ubalozi wa Tanzania yalioko pembeni kidogo mwa mji wa mji mkuu wa Congo DRC katikakati ya mji mdogo wa Ivuba.

Katika moja ya meza zilizokuwa ndani ya vyumba vya juu kabisa ndani ya ubalozi huo kulikuwa kuna mtu amesimama kando ya meza hiyo huku kila mara akijaribu kukuna kichwa chake ambacho hakikuwa na unywele hata mmoja.

Mtu yule hakuwa mtulivu wa nafsi,akili na mwili.Bila shaka kwa sababu kadhaa alizozijua yeye na muda wote aliokuwa amesimama kando ya meza ile alikuwa akitazama dirishani,dirisha ambalo wakati huo lilikuwa lipo wazi na halikuwa limefungwa wala kushushwa pazia kubwa na zito ambalo wakati huo lilikuwa limekunjwa kwa namna fulani hivi kisha likashikizwa na kibanio maalumu ambacho kiliacha pazia lile likiwa limejikunja katikati na kujiachia chini.

Ingekuwa siku zingine bwana huyu angeliweza kumuita mfanya usafi na kumkanya juu ya kusahau kufunga dirisha na kushusha pazia,lakini leo hii hilo hakukumbuka kabisa na badala yake akawa amejielekeza kuwaza na kuwazua jambo fulani tata ambalo kamwe hakudhani linafanyika katika nchi ile ya Congo.

Macho yake yalitazama dirishani tena na hapo akashuhudia jengo lingine refu lililokuwa likitazamana na ofisi zake zile,jengo lile lilikuwa ni hoteli kubwa kabisa ndani ya jiji la Kinshasa na mji ule wa Ivuba.

Tofauti na siku zote ambazo huwa analitazama mara kadhaa huku akiwa na kikombe cha kahawa mkononi,lakini leo hii hakuwa na kikombe na hata yale mawazo yake ya kutaka siku moja yeye au mwanae ajenge jengo kama lile nchini Tanzania hayakuwa kabisa akilini mwake.


Akajikuna kichwa na kujiegemeza kwenye meza iliokuwa kando yake kisha akaketi huku sasa mwili wake ukianza kuhisi joto la ajabu ambalo hakujua ni la uoga ama la joto la ahsubuhi ile ya ajabu kwake.

Akiwa bado anatizama pale dirishani mara mlango wa ofisi yake ukafunguliwa bila mfunguaji kubisha hodi.

Akaingia mwanaume mkakamavu mwenye misuli imara na kusimama nyuma yake.

Balozi Ally Sapi akageuka kutoka kule alikokuwa anaangalia na kumgeukia mwanaume yule.

Walitazamana kwa muda kidogo kisha Balozi Sapi akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kwa mkupuo.

“Alikuwa sahihi yule bwana mdogo” alisema Balozi huku akimtizama usoni mwanaume yule aliekuwa amesimama mbele yake.

“ina maana ndicho kilichotokea kwako sivyo!”alisaili mwanaume yule.

“Haswaa na tena kinaeza kuniondoa duniani masaa machache yajayo!” alisema Balozi huku akimtizama yule mwanaume na kuuona mshituko wa wazi usoni pake.
Ikawa zamu ya yule mwanaume mkakamavu kujikuna kichwa na kushangaa huku nae kichwa kikijaa moto wa joto ambalo hakujua limetokea wapi ahsubuhi ile.

“aaah ina…” akataka kusema yule mwanume baada ya kuwa anahitaji maelezo zaidi kutoka kwa balozi Ally Sapi,lakini hakumaliza kauli yake tayari balozi Sapi alishaanza kusema.

“Nilipokea ugeni jana jioni wakati natoka hapa ofisini,na kabla sijafika nyumbani yakanipita magari sita kwa kasi na kwenda kusimama mbele kisha gari la mwisho likaanza kupunguza mwendo hali ilionifanya nipunguze na mimi pia na kisha nikaona ishara kutoka kwa dereva wa gari la mwisho kati ya yale magari sita akiniashiria nisimame nami nikatii kwa kusimama pembeni hasa kwa kuhisi inaeza kuwa ni heri tu. Kutoka katika magari yale wakashuka wanaume wanne wakaja karibu na gari langu na bila kusema kwa maneno wakanipa ishara nishuke ndani ya gari,nami nikatii,wakaniongoza hadi kwenye gari moja wapo na humo ndani ya gari sikuamini kabisa nilichokiona aisee” alimalizia kwa kusikitika balozi Sapi.

“kwa ikawa vile tulivyowaza na ulichokiona ni kile kile alichosema marehemu Bulembo!” alisema tena yule mwanaume na hapo ikawa ni zamu ya Balozi Sapi kutumbua macho kwa kutoamini alichokisikia.

“ina maana Bulembo amefariki,lini na wapi!” alihoji Balozi Sapi huku macho yake yakiwa bado yapo yanamtazama mwanaume yule bila kupepesa huku moyo wake ukiruka sarakasi kifuani kwake.
Mwanaume yule akajikuna kichwa na kurudi kumtazama Balozi Sapi huku akijaribu kukwepa kumbukumbu mbaya zilizoanza kumrudia kichwani.

“Nilifika kwake leo mapema kabisa, baada ya kuniandikia ujumbe wakunitaka nifike kwake,nikawahi kufika lakini ikawa kazi bure,nilikutana na maiti yake ikiwa imelala sakafuni na tundu kubwa la risasi shingoni lakini pia nilikuta nyumba yake yote imepekuliwa” alisema mtu yule huku kwa mbali machozi yakizilenga mboni za macho yake,akatumia mgongo wa kiganja chake kujifuta.

“sikijua kama inaeza kuwa namna hii na kwa uharaka mkubwa hivyo” alisema Balozi sapi.

“Hakuna namna lazima tutoe taarifa mapema ofisi kuu mheshimiwa” alisema yule mtu.

Balozi akainama kidogo chini ya meza na alipoinuka alikuwa na mkoba mweusi wa ngozi na bila kutoa kilichomo akamkabidhi yule mwanaume.

“kuuawa kwa Bulembo unamaanisha kuwa kuna msaliti kati yetu hapa ubalozini na pia ni ishara kwetu kuwa tayari tunawindwa tusiifikishe taarifa kunakotakiwa,lakini jitihada za Bulembo zimetuongezea uelewa wa hili jambo,hivyo peleka hivi vielelezo ofisi kuu na hakikisha wanahusika na uzuiaji wa hili jambo,msaliti acha aendelee kuwapo hapa ipo siku kiama kitakuwa juu yake…” Balozi Ally Sapi alisema huku akimkabidhi ule mkoba ambao ulikuwa na nyaraka muhimu sana zilizohusu kile walichokuwa wanakizungumzia pale wakati ule.

“kwa walivyokuteka walitaka uwe miongoni mwao sivyo!” alihoji yule bwana huku akipokea ule mkoba na kuutazama.

“Ndio na nilikataa licha ya kuahidiwa mazuri na bwana yule na kukataa kwangu kunamaanisha kifo kwangu hivi karibuni,hivyo basi hakikisha mpango huo unakoma mara moja,nakuamini Honda” alimalizia kusema Balozi Ally Sapi kisha akageuka na kumwacha Honda akigeuka ili atoke ndani ya ofisi zile za ubalozi wa Tanzania nchini Congo.

****

“kuliaa nyuzi sabiniii…hapo!”

“usijali Mimi ndie Kizibo,hata bila ramani yako tayari wamejaa kwenye jicho la mzungu” alijinadi Kizibo huku mkono wake wa kushoto ukiwa unachezea lenzi ndogo iliokuwa inefungwa juu ya bunduki ya kupiga masafa marefu na mkono wake wa kulia ulikuwa umekamata vyema eneo la kufyatulia risasi ya bunduki ile aina ya K2Lapua magnum rifle,bunduki safi ya kisasa ya kudungulia ukiwa umbali wowote ule. Kizibo hakuwa peke yake alikuwa na mtu mwingine eneo lile ambae yeye akikosa kazi huwa anashika kiona mbali na kisha humsaidia Kizibo kusoma masafa ya windo lao.

“Kojo hawa jamaa wanaongea sana,bila shaka wanajadili hii inshu Mzee” alisema Kizibo huku akijitahidi kufinya jicho lake ili kuhakiisha jicho moja linapata nguvu ya kutazama taswira iliojiweka ndani ya lenzi ya bunduki ile ya kudungulia.

Watu hawa walikuwa kwenye lile lile jengo lililokuwa likitazamana na dirisha la ofisi ya balozi Ally Sapi na wakati huu Kojo na Kizibo walikuwa kwenye moja ya vyumba vya jengo hilo la hoteli huku wakiwa wamekwisha kuweka mtego wao usawa wa lile dirisha ambamo kulikuwa kunafanyika mazungumzo kati ya Balozi Ally Sapi na Honda Makubi,mpelelezi na mfanyakazi ndani ya ofisi za ubalozi.

“Huu nao ni mwanya inabidi uzibwe Kizibo”alisema Kojo huku akishusha kiona mbali.

“Yule bwege anae toka na ule mkoba nenda uuchukue kisha utajua cha kumfanya,huyu kipara mimi bamzibua sasa hivi” alisema Kizibo huku akitema mate pembeni na kidole kikielekea kwenye kifyatulio cha bunduki yake alioipenda na kuihusudu sana.

***
Honda Makubi alifika nje baada ya kuwa ameshasaini kitabu cha mahudhurio na wakati huo huo alikuwa anapitisha mawazo ya kurudi nyumbani kwa marehemu Bulembo ama aendelee na taratibu za kupeleka zile nyaraka kuzihifadhi na kufanya utaratibu wa kuzituma ofisi kuu jijini Dar es laam na wao watajua cha kuzifanyia.

Akaingia ndani ya gari lake na kuliondoa kwenye maegesho maalumu kwa ajili ya wafanyakazi wa pale ubalozini,lakini ambacho hakujua japo alihisi ni kuwa watu wawili ndani ya ofisi zile walikuwa wakimtizama wakati akitoka eneo lile na mmoja kati yao akanyanyua simu na kupiga pahali kisha akarudi kuendelea na taratibu zake za kufanya usafi.

***
Baada ya kuhakikisha Honda ametoka ndani ya ofisi zake balozi Ally Sapi alichukua simu yake na kujaribu kumpigia Rais wa Tanzania,lakini ajabu simu yake ilikataa kutoa mawasiliano nje ya nchi ile ya Congo,akachukua tena simu nyingine maalumu ambayo hutumia kuwasiliana na mkurugenzi wa usalama wa Taifa nayo ikagoma.

Akiwa kashikwa na mashangao na hamaki ya kutoamini,Balozi akaanza kuzunguka ofisi yake kama asie amani uwepo wake mle ndani na hapo ndipo akalikumbuka tena dirisha lake na haraka akataka kuwahi kuishusha pazia.
Doh
Alikuwa amechelewa.
Risasi yenye nguvu ikatua katikati ya paji la uso wake na kusambaratisha kichwa chake kisha kumsukuma nyuma kwa nguvu na mwili wake usio na mhimili wa utimamu ukajibwaga chini kwa kishindo kisha kwa jitihada kidogo ukajitikisa kidogo na kutulia na ukawa mwisho wa Balozi Sapi.

Kule risasi ilikotokea,Kizibo akatema mate mengi chini.
“pyutyaaa”
Kisha akajiramba midomo yake na kuinyanyua bunduki yake na kisha akaanza kuitawanya huku akipiga mluzi hafifu wa ushindi.

*****

Honda Makubi aliegesha gari yake ndani ya geti la la nyumba ya marehemu Bulembo ,kisha akashuka taratibu na huku akiangaza huku na huko kwa umakini wa hali ya juu.

Kama alivyokuwa amepaacha ahsubuh na ndivyo alivyopakuta pakiwa katika utulivu wa kifo huku maiti ya mmliki wa nyumba ile akiwa ndani hana uhai japo wa kupigia chafya.
Honda akasimama kuupisha utulivu katika akili yake na muda huo mikono yake ilikuwa ikifanya jitihada za kujivika mipira maalumu ya viganja vya mikono.

Alipohakikisha amevaa sawia mipira ile,akapiga hatua ndefu na kuufikia mlango kisha akaufungua taratibu huku utulivu ukiwa ni ngao yake muhimu wakati ule.
Taratibu akachungulia ndani kwa tuo, na kutoka pale alipokuwa aliona mwili wa mpelelezi Bulembo ukiwa umelala vilevile alivyouacha na pembeni yake aliona mparanganyiko wa sofa ukiwa kama alivyoacha hapo ahsubuhi,akapiga hatua nyingine kubwa na kwa haraka zaidi kisha katika uharaka huohuo mikono yake ikaurudishia mlango na kuacha ukijibamiza kwa nguvu nyuma yake huku yeye akiwa hana habari nao tena.
Akatazama mazingira ya mle ndani,hakuona mabadiliko yoyote wakati ule. Akapiga hatua na kuufikia mwili wa hayati Bulembo,kisha akainama na kuanza kupekua mifuko ya suruali aliokuwa amevaa hayati Bulembo.
Katika dakika za mwanzo hakuona la maana katika jitihada zake za upekuzi katika mwili ule uliolala bila uhai.
Akasimama huku akili yake ikianza kujutia muda aliopoteza kurudi nyumbani kwa hayati Bulembo.
Hakuwa sahihi katika mawazo yake,hadi pale macho yake yalipo elekea miguuni mwa maiti aliokuwa akiipekuwa wakati ule na hapo tena akili yake ikaganda bila kufanya jitihada zozote za kutaka kujilaumu kama mwanzo.
Bila kufikiri zaidi,mwili ukafanya vitendo.
Haraka akainama na kupeleka mikono yake kwenye mguu wa kulia ambao ulikuwa umevikwa soksi huku ule wa kushoto ukiwa hauna soksi.
Akaivuta ile soksi na wakati ikimalizikia kuvuka akaona kikaratasi kidogo kikianguka kutoka ndani ya soksi ile.
Honda Makubi alitabasamu huku sasa akili yake ikijipongeza kwa kuwaza kurudi tena ndani kwa hayati Bulembo.
Akainama kuikota ile katasi na wakati ikiwa imeenea kiganjani kwake na mwili ukifanya jitihada za kunyanyuka baada ya kuwa umeinamishwa kuanzia tumboni kwenda juu,mwili wa Honda haukumaliza hilo tendo na mara hiyo kikafanyika kitendo cha haraka na wepesi wa hali ya juu kutoka kwa Honda japo matokeo yalikuwa ni kukosea hesabu za gafla.
Wakati akitaka kusimama akaona kivuli kikiwa karibu yake na mara hiyo akasikia msukumo mkubwa kutokea kiunoni kwake na haraka akajirusha mzima mzima kwenda mbele na bahati mbaya hakuwa ameiona meza iliokuwa hatua chache kutoka pale alipokuwa na alipotaka kujigeuza ili aone kilichomsukuma akajikuta akisambaratika chini baada ya kuipamia meza na kusambaratika nayo chini.
Hakuzubaa
Muda huo huo akajigeuza kwa namna ya ajabu kabisa kisha akatumia mkono mmoja kukita chini huku umbo lake refu likiwa wima katika nukta iliofuata na macho yake yakashuhudia kasi ya ajabu ya kiumbe mweusi na mrefu akimfuata kwa kasi ya upepo na kabla hajasimama imara akajikuta akipokea mateke mawili yaliopigwa kwa mtindo wa tandika reli nae hakuwa amajiandaa kwa hilo akaenda chini mazima kwa mara ya pili.
Hakuzubaa tena mana alishaona kasi na ujuzi wa adui yake,haraka akajizoa na kusimama wima huku akisikia maumivu yakimtambaa mwili mzima kuanzia kifuani,na hapo akajikuta akimsifu adui yake yule kwa kuwa na kasi na nguvu ya kumtetemesha namna ile.
Akajipanga.
Adui akausoma usimamaji wa Honda na akajua anapambana na mtu wa kiwango chake nae akafanya haraka ya kuokoa muda na hilo likawa kosa upande wake.
Adui akarusha ngumi kwa ustadi kumwelekea Honda,lakini Honda aliiona na kama utani akahepa na ngumi ikapiga hewa kisha kwa usitadi mkubwa akaachia konde lenye uzani uliokadiriwa na likampata adui ubavu wa kushoto na adui akabweka kama malaya kichochoroni.
Honda akaachia tabasamu la upande kisha akachumpa na kusimama nyuma ya adui aliekuwa anafanya jitihada za kupambana na maumivu ya mbavu zake,kisha akaachia teke moja kali lililojikita usawa wa maungio ya kiuno na uti wa mgongo na adui akabweka tena kwa mara ya pili huku Honda akiachia tabasamu lingine la ushindi na akihepa tena kujiweka mbali na adui aliekuwa anageuka kwa gadhabu.
Kisu.
Honda aliona kisu mkononi mwa adui na hapo akajipongeza kwa zile hesabu zake za kuwa mbali na adui.
Adui alitupa mikono harakaharaka kumchanganya Honda kisha akaachia teke kali lililopanguliwa kistadi na Honda kisha adui akatumia nafasi ile kumchapa konde kali la mbavu kama malipizi na huku akiachia ukelele wa furaha kwa lipizi lake.
Honda akayumba kwa kupoteza malengo kisha akafanya jitihada kusimama imara.
Hakufanikiwa.
Adui akatumia nafasi ile kumshindilia tena mateke mawili ya kifua na kumtupa kwa kishindo sambamba na kabati la vioo lililokuwa sebuleni pale na kusambaratika chini huku vioo vikimjeruhi hapa na pale.
Kutoka pale alipokuwa ameangukia,Honda alimshuhudia adui yake akinesa kwa aina ya ajabu kabisa na kumfikia pale alipokuwa huku kisu kikiwa kimeshikwa imara mkononi,Honda hakutaka kufa kizembe kwa nguvu alizobakia nazo akasimama kwa kasi kisha akajirusha huku mikono yake ikimkumbatia adui usawa wa kiuno na bega likijikita katikati ya tumbo na kumbwaga kwa nguvu chini ya zulia.
Ingekuwa ni mieleka basi hii ingekuwa ni Roman spear,ila hii sasa wakati huo ilikuwa ni Honda spear.
Walipoanguka chini Honda alizisikia kelele za adui yake wazi wazi masikioni mwake na na yeye akajinasua haraka kutoka pale chini akabaki akiwa amesimama huku akitweta kwa maumivu ya majeraha ya kukatwa na vioo vya kabati.

“Bwege sana wewe”
Jamaa alibweka pale chini huku akijizoa zoa kutoka chini na hapo Honda akapata kumtazama vizuri adui yake na akaona kovu baya usoni pake ambalo dhahiri lilimpa tabu sana yule jamaa kuliuguza bila shaka na lilielekea kumtoa jicho upande wa kushoto.
Kovu lile liliongezea mvuto mbaya kabisa katika sura nyeusi ya shababi yule.

“aah nusura univunje kiuno haini wewe” jamaa alizidi kulalama huku akifanya jitihada za kuupata mhimili mzuri kwa kusimama.

“unataka nini kwangu!” hatimae Honda aliuliza.
Na hapo akashuhudia yule bwege akikenua vibaya na hapo Honda akapata kuona kinywa kibaya kutoka kwa yule jamaa.
Kinywani hakuwa na meno mawili ya mbele na ulimi ulikuwa mweusi tofauti na ndimi za binadamu wa kawaida.
“nautaka mkoba mweusi komredi”
Jamaa alijibu swali la Honda.
Honda akatumbua macho kwa umakini kisha akauliza tena.
“mkoba upi?”

“ule uliopewa na Balozi”
Eh bana eh
Honda akizubaa kwa nukta kadhaa za kutoamini kilichosemwa na adui yake.
Kwa nini!.

Kwa sababu alipewa mkoba na Balozi Sapi ndani ya nusu saa iliopita na hakuwa amemuonesha yeyote ule mkoba muhimu wakati ule.
Honda akakumbuka aliuacha ndani ya gari huko nje.
Hata!
Akaruka juu kisha akaachia teke kali lilokuwa likimwendea yule jamaa,jamaa akalegea kidogo na kulikwepa lakini hakujua hila za Honda akajikuta anapokea konde zito katikati ya kifua,jamaa akabweka kama ngedere anaeiba mahindi.
Adui akaenda chini mazima.
Honda akamwendea huku akiunguruma kwa gadhabu lakini hakufika kwa adui yake ambae alijiinua kwa mtindo wa aina yake kisha akaruka kama kima na kuufikia mlango na kutokomea nje kwa kasi ya umeme.
Honda hakukubali Nae akapiga tambo kubwa na kuufikia mlango,haraka akatoka,lakini kasi yake haikumpa matunda aliotaka,isipokuwa kitu pekee alichoambulia ni kuona namna yule jamaa alivyokuwa akimalizikia nje ya geti na kuliacha likijipigiza kwa nguvu.
“Mkoba!!” Honda alijisemea huku haraka akikimbilia gari lake na kujilaumu kwa uzembe wa kutokutembea nao.
Akafungua mlango wa gari lake na kitu cha kwanza ni kuelekeza macho yake pale ulipokuwa mkoba ule ambao sasa alianza kuupa manani kwa kuwa kuna adui asie mjua akiuwinda.
Kwanini! Hakujua japo alihisi.
“kina nani hawa?” alijiuliza huku akianza kutoka ndani ya ile nyumba ya hayati Bulembo.
Akiwa tayari ametoka nje ya uzio wa nyumba ile,mara akasikia ving’ora vya magari ya polisi vikielekea kule alikotokea.
“shiit!!!” alimaka kwa gadhabu kwa kutoelewa ni nani aliewapigia polisi wa Congo katika uharaka wa namna ile.
“Mambo yanazidi kunoga aisee” alijisemea huku akiongeza mwendo wa gari lake kurudi kwa balozi Sapi kumpa taarifa ya alichokiona kule kwa Hayati Bulembo.
Hakujua yajayo…
***

Soma hapa pia
Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia - JamiiForums
Big up kk unajua kuandika na kusimulia matukio kwa mtiririko wenye kuleta Mantiki kwa wasomaji
 

Similar Discussions

20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom