Jarida la The Economist leo limemtukana Rais Magufuli kwa kumwita FOOLISH

Vyombo vya habari vina uhuru wa kutosha kwenye Nchi nyingi, hawa huwa nawachambua kila sentensi inayoongewa na mkuu wa Nchi, au kiongozi kwenye heshima yake kwenye jamii. Pengine Wamechambua matamshi yake, vitendo vyake na serikali yake, hivyo wakapata cha kumwita.
Tanzania unaambiwa “ msifikiri kuwa mnao uhuru kivile”

Swali: kuna yeyote anaweza kunisaidia kujua kama kuna gazeti Tz Leo linalo andika habari za kiuchunguzi kama zamani, kulingana na matukio yanayo tokea Nchini ?
HA KU NAAA
 
Dah! Nimeisoma, so sad! Jamaa wametumia lugha kali sana, nadhani Dk Abbas na Palamagamba wanatakiwa kufanya kitu kuwakomesha hawa mabeberu!
At last! wewe tuko kwenye mtumbwi mmoja. Lugha iliyotumika hapo siyo ya kiungwana kabisa. Inaleta picha ya tofauti kidogo, hata kama wanakosoa sidhani kama walikosa maneno mengine ya kutumia.
 
Trump kaitwa majina yooote mabovu, hadi stupid, arrogant, shithole, etc.. Nadhani haina haja ya kulumbana nao, sisi tunajua our President ni mtu makini mno mno, and haijawahi kutokea mzungu kumpenda mwafrika, sahau hilo..!!
 
Mkuu wewe sio nobody .... sauti yako inasikika hadi kuzimu kwa Malcom X na Patrice Lumumba (Hawa wote walikuwa wanaharakati maarufu waropokaji bila kujali wanamropokea nani lakini walikosa busara na akili, yaani unwise and stupid na kwa sababu hiyo hawakufanikisha cha maana), na duniani huku hadi kwa Nape Nnauye na Julius Malema! Kimsingi kuleta hapa hii kitu ungependa wote tushangilie ulichokileta kutoka huko the economist. Ukimkuta mzazi wako anatukanwa nyumba ya jirani nawe ukaja nyumbani kuwaeleza wadogo zako matusi anayotukanwa baba yako hiyo nayo ni unwise and stupid!

Regards
Anakuwa kama yule mtoto wa Noah aliyemkuta baba yake kalewa yuko uchi akaenda kuwaambia wenzie huku akichekacheka
Inasemekana huyo mtoto ndiye baba wa kizazi cha Waafrica

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari,
Leo mapema nilitafuta nakala yangu ya Jarida la The Economist, moja kati ya majarida makubwa kabisa, makongwe na yanayosomwa na wengi ziaidi hapa duniani.

Kama kawaida huwa naenda kuangalia kipengele cha Africa & Middle East. Leo walichokisema kuhusu Tanzania kwenye kichwa cha habari ni kumwita Raisi Magufuli "A Tanzanian despot wannabe"

Ukisoma zaidi wameongelea jinsi anavyowafunga wapinzani na wakafika sehemu wakasema kwamba Mh Tundu Lissu ndiye anamtesa sana Raisi wetu. Wakasema maneno haya kuhusu Lissu "Mr Lissu is back in full cry, with well-aired performances at Western think-tank forums and television abroad"

Lakini katika yote haya, lililolamata sana macho yangu ni hili la kusema kwamba Raisi Magufuli ni FOOLISH. Wamesema hivi " The President has been foolish in Economics matters too" wakimaanisha kwamba Raisi wetu ni mjinga kwenye mambo ya kisiasa waliyoyazungumzia lakini pamoja na yale ya kiuchumi.

Wamezungumzia suala la Gazeti la The Citizen kufungiwa na wakasema kuna mpango wa kuliuza kwa mtu mwenye asili ya Mashariki ya Kati ambaye ni rafiki wa Raisi Magufuli.

Mwisho kabisa wamezungumzia jinsi ambavyo Raisi wetu amegeukia Mashariki ya Kati na Uchina kuomba msaada baada ya kugombana na mataifa ya Magharibi.

MY TAKE:
Wizara ya Mambo ya nje ichukue hatua stahiki kwa haya maneno ambayo Raisi wetu amekashifiwa nayo. Maana neno A Fool kwenye Cambridge Dictionary linasema hivi " A person who behaves in silly way without thinking" na neno Foolish ni "Unwise, stupid or not showing good judgement"

Jamani Raisi wetu katukanwa matusi makubwa sana kwasababu binafsi siamini kwamba Raisi wetu ni mpumbavu au mtu asiye na uelewa wowote ule...

Binafsi siyo mshabiki wa Raisi Magufuli lakini haya matusi kwa jarida kubwa kama hili hayajakaa vizuri. Hatua stahiki sichukuliwe na Wizara Husika.

Nawasilisha.

CC: chige, JokaKuu, Nguruvi3, Pascal Mayalla, introvert, Quinine, technically, Consigliere, Wick, Red Giant
Nenda mahakamani uwafungulie kesi ya kashfa walipe fidia na kifungo juu!
 
Back
Top Bottom