Jaribu hizi tatu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaribu hizi tatu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Aug 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,155
  Likes Received: 5,588
  Trophy Points: 280
  Jaribu hizi tatu!  [​IMG]Kuna baadhi ya wanandoa tena kwa machozi wamekuwa wakilalamika kwamba partners wao hawawezi kuongea nao tena!
  Hawezi kushirikisha kitu chochote (emotions/feelings) ingawa wanaishi nyumba moja, wanakula chakula kimoja, wanalala kitanda kimoja na wengine wana watoto pamoja.

  Wamejikuta ndoto zao zinayeyuka na ladha ya ndoa na maisha kwa ujumla imekuwa chungu.

  Kama unapitia upweke wa aina hii na kujikuta unajuta kuishi na mume au mke wa aina bado kuna matumaini na kuna nafasi kubwa ya kuweza kurudisha kwenye mstari, jaribu kufanya yafuatayo.

  Tembea katika Roho:
  Ndoa si two-way street kutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke au kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume bali ni three way street kati ya mke, mume na Mungu.
  Tunapotembea katika Roho, Mungu anamwaga upendo wa kutosha kati ya mke na mume.
  Breakdown yoyote kati ya mke au mume na Mungu huweza kusababisha wanandoa kuanza kuvurugana ndiyo maana wanandoa ambao hofu ya Mungu, kutembea katika Roho ni Nambari one basi wamebarikiwa kwamba huwezi ukampenda Mungu usiyemuona ukashindwa kumpenda partner wako ambaye unamuona.
  Ukiguswa na Mungu lazima na ndoa yako itakuwa ya tofauti.
  Kumbuka kutembea katika Roho (Roho Mtakatifu) ni kitu tofauti na kujiita Mkristo

  Achana na kukaa kwenye lawama, maumivu, uchungu, kuangalia udhaifu wa partner wako:
  Yeyote ambaye analalamika kwamba ndani ya ndoa yake hakuna upendo ukichunguza kwa makini utakuta amebeba fulushi zito sana la orodha ya mambo mabaya ambayo partner wake anamfanyia au udhaifu wa partner wake.
  Anaongelea huo udhaifu wa partner wake, anasimulia rafiki zake, anauamini, anauwaza, anaukiri kutembea nao kama sala.

  Kumbuka!
  “You are by want you think”
  Biblia pia inasema
  “
  Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo”
  (Mithali 23:7)

  Hisia mbaya (negative thoughts) hata kama ni kweli huwa na matokeo mabaya kwenye feelings.

  Orodhesha vitu 10 vizuri kuhusu mke/mume wako na kiri mara mbili kwa siku kwa siku 21
  Shukuru kwa kila jambo.
  Kulalamika kila siku huweza kuharibu emotions zako bila kujua hata kama mume wako au mke wako hafai kabisa bado unaweza kutumia mambo mazuri aliyonayo kuirudisha ndoa yako kwenye mstari.

  Huwezi ukawa na mawazo tele ya udhaifu wa mke wako au mume wako na wakati huohuo ukamfurahia na kumpenda na kuwa na feelings za upendo wa juu.
  Vita ya upendo huweza kushinda au kushindwa kwa mawazo yako kwani moyo ni mtumishi wa mawazo yako.

  Moyo huamini kile mawazo yako yanakitunza.
  Mtu mmoja (jina limewekewa password) alikiri kwamba hampendi tena mke wake na kwamba ilikuwa ni miezi mitatu kila mmoja alikuwa analala chumba chake, nilipomwambia aandike mambo kumi mazuri kuhusu mke wake kwenye karatasi.
  Tukakubaliana kila siku asubuhi anapoenda kazini kuyatafakari hayo mambo mazuri 10 kuhusu mke wake na pia kuyatafakati tena jioni akirudi kazini anapoendesha gari lake.
  Baada ya siku kumi akakiri kwamba sasa mambo yameiva kwani tumerudiana, zaidi kulala chumba kimoja sasa tunalala kitanda kimoja.

  Na baada ya wiki tatu akakiri kwamba anampenda mke wake kuliko wakati wowote katika maisha yao ya ndoa tangu waoane.
  Alipoulizwa je, umeyashika (memorize) yale mambo 1o mazuri kuhusu mke wako akasema kwamba yale aliyashika siku ya tatu na siku ya nne akaamue kuongeza hadi yakawa 15 na kwa kuwa yalikuwa mtindo wa Cards hivyo alikuwa anayapitia moja baada ya lingine na kuyachanganya na kuyakiri over and over.

  Hakuna binadamu ambaye anaweza kuwa na orodha ya mambo 10 mazuri kuhusu mke au mume wake na akayatamka na kumshukuru Mungu twice a day na kusiwe na kufufuka kwa upendo mpya (compassionate love)

  Kumsifu na kumshukuru mke wako au mume wako mbele za Mungu kwa mambo mazuri aliyonayo ni silaha ya nguvu kubwa ili kuwasha upendo na mapenzi mapya katika ndoa.

  Ubarikiwe na Bwana!
   
 2. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  hili nalo neno.....kwanza kwanini ulimuoa kama kweli kabsaaa humpendi???.....kuna vitu zaidi ya million moja ulivyovipenda kwake na ndio maana mkaamua kuoana...haya ya kumchoka mwenzio ni mawazo hasi na ubinafsi wako ndo unaofanya umwone mwenzi wako hafai kitu.....mungu atangulizwe kwa kila jambo na ndoa itakuwa yenye furaha na upendo wa ajabu
   
 3. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2009
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii ni kweli kabisa,nitaitumia kuadvice marafiki,God bless u.
   
 4. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thank U.
   
 5. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Ngoja niiprint ili niisome nikiwa nimetulia na ikibidi nimfwaxie mwenza.
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Naam,uisome na umfwaxie mwenza ndo mtindo wa kisasa,kitu kizuri kula na mwenzako haaaaaa.
   
 7. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kama sumu kula pekeako....
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,155
  Likes Received: 5,588
  Trophy Points: 280
  Kama sumu kula pekeako....

  Mpaka aje kujua sumu yuko............mwaisela
   
 9. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  ahsante mkuu, lakini ingependeza kama ungetoa ushauri kwa wasio katika ndoa ili wafaidike pia.
   
Loading...