Jaribio: Ukitakujua waTz wengi wana funza kichwani, lidondoshwe gari la mafuta lenye maji, uone kitachotokea

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,002
40,670
Yaani wakati bado hatujasahau; tufanye jaribio hili, tuchukue gari la mafuta halafu tujaze maji yenye rangi na harufu ya petrol, then tulipindue alfajiri kwa kutumia crane la breakdown bila watu kuona, halafu asubuhi tuyafungulie hayo maji/ petroli feki yaanza kutiririka mtaroni, uone watu watakavyojazana na vidumu vya maji kama wapo bombani. Hawatakumbuka ya Msamvu!
=============================
Update: 25/08/2019

==============================
Update:
================================

Mtoa roho amekwisha wasiliana nawe tena! Loh...

Yaani pamoja na watu wa Moro kuteketea kwa moto juzi bado kuna watu huko Kahama walitaka kwenda kuiba mafuta baada ya ajali kutokea! Kweli kusikia kwa kenge...
============================
Update: 27/08/2019
=============================
Update: 01/03/2021
 
Watu wanaweza kwenda kweli
Hahaha...sidhani kama watakuwa na huo ujasiri.
Watu wanaweza kwenda maana Kuna watu akili zao na za kuku hazipishani,kuku wakiwa sehemu halafu mmojawapo akakamatwa na kimburu watatawanyika,lakini baada ya mda mfupi utawaona wamerudi hukohuko.Hivo likitokea tena(Mungu apishe mbali)Kuna watu wanaweza kwenda huku wakisema"kufa kulala bwana".
 
Ikitokea watu wakajitokeza licha ya yote haya kutokea basi ujue watu wamekata tamaa na maisha
 
Inategemeana na huka ya mtu mimi binafsi Sina tamaa naamini hvyo ila waafrica wengi waanaweka pesa mbele kwanza mengine yanafuata
 
Hahaha...sidhani kama watakuwa na huo ujasiri.
Unauliza wakati huyo alirudi eneo la tukio Jana usiku?
IMG-20190811-WA0050.jpg
 
Ikitokea watu wakajitokeza licha ya yote haya kutokea basi ujue watu wamekata tamaa na maisha
Wala wengine sio kukata tamaa bali ni Kama kijitabia tu cha mtu wengine hawatakagi kupitwa na chochote,Yuko tayari kuchukua hata Kama hajui hicho alichokichukua anakwenda kukifanyia nini almuradi kachukua tu.Ni sawa na mwizi anaweza kukuibia kitu hata kisicho na thamani yoyote anaridhika akiiba hata akienda kukitupa hicho alichokichukua anaona Safi tu mradi kaiba.
 
Yaani wakati bado hatujasahau; tufanye jaribio hili, tuchukue gari la mafuta halafu tujaze maji yenye rangi na harufu ya petrol, then tulipindue alfajiri kwa kutumia crane la breakdown bila watu kuona, halafu asubuhi tuyafungulie hayo maji/ petroli feki yaanza kutiririka mtaroni, uone watu watakavyojazana na vidumu vya maji kama wapo bombani. Hawatakumbuka ya Msamvu!
Chief, tatizo la kuwa na funza kichwani kwani linasababishwa na nini?
Nini kifanyike kutoa hawa funzwa vichwani?
 
Yaani wakati bado hatujasahau; tufanye jaribio hili, tuchukue gari la mafuta halafu tujaze maji yenye rangi na harufu ya petrol, then tulipindue alfajiri kwa kutumia crane la breakdown bila watu kuona, halafu asubuhi tuyafungulie hayo maji/ petroli feki yaanza kutiririka mtaroni, uone watu watakavyojazana na vidumu vya maji kama wapo bombani. Hawatakumbuka ya Msamvu!

Yes!

Naunga mkono hilo jaribio.

Ninaamini kabisa kitakachotokea ni kama kile kile kilichotokea jana ukitoa labda mlipuko na majanga yaliyotokea kwa sababu safari haitokuwa mafuta yenye kuwaka moto kirahisi.
 
Ugumu wa maisha..., hata wewe ukifungiwa kwenye pango kwa muda mrefu na ndugu zako usishangae mmoja wenu akipitiwa usingizi mkamfanya kitoweo..., its basic animal instincts when one is desperate...
 
Ugumu wa maisha..., hata wewe ukifungiwa kwenye pango kwa muda mrefu na ndugu zako usishangae mmoja wenu akipitiwa usingizi mkamfanya kitoweo..., its basic animal instincts when one is desperate...
Kwahiyo hii awamu ya 5 kuna watz ni kama wamefungiwa kwenye pango..., aiseee...!!
 
Back
Top Bottom