Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Kina nani hao watu wanaohusiana naye na hayo mahusiano ni ya kivipi na ni watafiti gani wameziomba tena na tena hizo nyaraka na hawakuzipata? Bwana Marables ni mmoja wao?:)

Vimada na nyumba ndogo, wachuchu na vichuchu, Nation of Islam na nation of bodyguards....
:p
 
Kwani ikiwa classified vipi, huwa hazitolewi au kukiwa na sababu gani?

tulikuwa tunazungumza sheria zetu za mambo ya classified materials; na Wamarekani nao wanazo na kwa miaka tofauti tofauti kutegemeana na terms za classification. Uliposema kuwa kuna nyaraka ambazo Wamarekani hawajaziachilia nilidhani umemaanisha kuwa terms zake za kuwa classified zimetimilika na zinatakiwa kuwekwa hadharani lakini serikali ya Marekani imekataa - kitu ambacho naamini kingeleta kesi za "freedom of information".

So.. hizi documents za Malcom X zilikuwa classified zisitolewe kwa muda fulani na muda huo umepita na serikali bado imekataa kuziweka hadharani na hakuna kesi ya Freedom of information ambayo imefikia mwisho?
 
Mwanakijiji:

Sijazisoma profiles za Kambona za CIA. Lakini ni lazima tukumbuke kuwa profile za 1964 za watu weusi zilikuwa flawed. Nikirudi kwa Kambona na Nyerere. Kuna vitu vya kuangalia katika siasa za kiafrika.

Kati ya hawa wawili Nyerere alikuwa anatumia sana intellect, wakati Kambona alikuwa anajichanganya na watu. Siasa zao ni sawa na za Jacob Zuma na Thabo Mbeki. Kwenye mkutano, Zuma anaweza asitoe point yoyote hile ya maana. Lakini akianza kuimba nyimbo za kimapinduzi, tayari watu wanaona he's one of them. Kwa upande mwingine, Mbeki is a western intellect.

Miaka ya Mwanzo Kambona alikuwa amejichanganya vizuri na watu wa kawaida kuliko Nyerere. Na miaka ilivyozidi kwenda Nyerere na Kawawa walimwiga Kambona jinsi ya kujichanganya na watu wa kawaida. Na Kambona alipoondoka kulikuwa na character assassination.

Vilevile watanzania tuna siasa za woga sana. Sioni sababu ya jina la Kambona kufutika katika mitahala ya shule kama vile hakuwepo.
 
Are you serious? Kweli kuelekea uhuru kuna mtu aliyekuwa amejichanganya na watu kuliko Nyerere? au miaka ya mwanzo una maana mara tu baada ya Uhuru?
 
tulikuwa tunazungumza sheria zetu za mambo ya classified materials; na Wamarekani nao wanazo na kwa miaka tofauti tofauti kutegemeana na terms za classification. Uliposema kuwa kuna nyaraka ambazo Wamarekani hawajaziachilia nilidhani umemaanisha kuwa terms zake za kuwa classified zimetimilika na zinatakiwa kuwekwa hadharani lakini serikali ya Marekani imekataa - kitu ambacho naamini kingeleta kesi za "freedom of information".

So.. hizi documents za Malcom X zilikuwa classified zisitolewe kwa muda fulani na muda huo umepita na serikali bado imekataa kuziweka hadharani na hakuna kesi ya Freedom of information ambayo imefikia mwisho?

Tulikuwa tunawekana sawa tu, manake kwanza uli-assume kuwa sheria hiyo ipo Tanzania (mpaka sasa hatuna ushahidi kuwa ipo, kwa miaka mingapi, kwa nyaraka za aina gani, zilizokuwa classified vipi)

Pili hukutoa angalizo lolote kuwa sio nyaraka zote tu zinaweza kutolewa ikiwa tu miaka imepita (kwa Marekani ni miaka 25 na sio 30)

Binafsi niliweka neno "automatically" kuonyesha kuwa sio kila nyaraka huwa inatolewa wazi, ambalo ndilo hili ulilokiri hapa.

Nadhani sasa tupo aya moja sio ukurasa pekee
 
Tulikuwa tunawekana sawa tu, manake kwanza uli-assume kuwa sheria hiyo ipo Tanzania (mpaka sasa hatuna ushahidi kuwa ipo, kwa miaka mingapi, kwa nyaraka za aina gani, zilizokuwa classified vipi)

sija assume sheria kama hiyo ipo Tanzania.

Pili hukutoa angalizo lolote kuwa sio nyaraka zote tu zinaweza kutolewa ikiwa tu miaka imepita (kwa Marekani ni miaka 25 na sio 30)

Sikuwa nazungumzia Marekani nilikuwa nazungumzia Tanzania; kwa Tanzania nyingi ni miaka 30.

Binafsi niliweka neno "automatically" kuonyesha kuwa sio kila nyaraka huwa inatolewa wazi, ambalo ndilo hili ulilokiri hapa.

sikudai kuwa kila nyaraka hata kama muda umepita inatolewa automatically; japo kwa wenzetu Marekani, taasisi zinafanya hivyo kama kutimiza matakwa ya sheria. Ndio maana kwetu nilidokeza haja ya wasomi wetu kudai nyaraka hizo zitolewe. Sijui utaratibu wa kwetu kutoa ukoje itabidi nipitie hiyo sheria tena.

Nadhani tuko ukurasa mmoja, naam.
 
I will go with Kambona.

well.. mtu mwingine anaweza kuchagua Kawawa, mwingine anaweza kuchagua Sykes, mwingine anaweza kusema Paul Boman, mwingine akasema Fundikira.. kama ni kuchagua tu can't argue. Lakini kama ni historia well wanasema even God can't change history.
 
yeah hakujichangana na Wakristu wa Kariakoo wala Wakristu wengine waliokuwa waasisi wa AA, TAAA, na TANU. I agree.

Sheria za siku hizo za Mwingereza hazikuruhusu mkristo kujenga Kariakoo, wote walikuwa wakuja tu. Wao walikuwa na sehemu yao ikiitwa "mission quarter". Ilikuwa ukiona Mkristo anaishi Kariakoo ujuwe kakaribishwa na Muislaam na au mgeni wa Waislaam. Wengine walikuwa wakija asubuhi na kundoka jioni aka "wakuja".
 
Back
Top Bottom