Jaribio la kuiba dhahabu katika mgodi wa Geita (GGM) lazimwa

papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
5,119
5,683
Jaribio la kutaka kuiba kiasi kikubwa sana cha dhahabu ktk mgodi wa Geita mchana huu mida ya 11:30hrs na watu wenye silaha nzito za kivitaa limezimwa na walinzi wa mgodi (snipers & quick respond unit force wakishilikiana na makomandoo walinzi wa ndege inayosafirisha dhahabu) mpaka mida hii imethibitika watu 2 wamepoteza maisha.

Jaribio hilo limefanyika Ktk airport ya mgodini wakati dhahabu hiyo ikipakiwa ktk ka ndege special tayari kwa kusafirishwa kwenda South Africa, hadi mida hii wana Geita bado tunasikia milio ya risasi zikilindima maporini na ving'ora vya ambulance za mgodini zikiwabeba majeruhi wengi wao ni walinzi wa wa mgodi, polisi walitarifiwa mapema kabisa lakini bado wanajipanga namna ya kufika eneo la tukio!


Tutazidi kuajuza kadri nitavyo pata habari zaidi.

UPDATE:
Polisi wamefika eneo la tukio na kwa sasa wanawakamata wakata mbao, wachungaji na wachoma mkaa wakiwatuhumu kwa ‘ujambazi' wakati wapiga deal halisi wameisha sepa , walinzi 8 wa mgodini ( wa kitanzania) wameahidiwa 10,000 USD kila mmoja kwa kuweza kulinda mali ya ' mwekezaji', huku mlinzi mzungu akisafilishwa kurudi RZA kwa matibabu ( huyu jamaa amepigwa kama risasi 3 mkononi na mguuni, na huyu ndio aliyeuwa jambazi baada ya kukabiliana naye uso kwa uso).

Polisi wamekabidhiwa sub machine gun 3, mabomu ya mkono 9 ( moja lilirushwa lakini halikulipuka vizuri) magazine zaidi ya 5 zikiwa na risasi zaidi 100, bullet proof vest 2.

Polisi wanasomeshwa wakubali kuwa wao ndio waliopambana na ku uwa majambazi ili hawa jamaa wanakwepa lawama za mauaji kimtindo, Mwili wa jambazi (kipande cha jibaba lenye asili ya kisomali inaaminiki ndiye alikuwa kiongozi wa uvamizi) umepelekwa mortuary, nikifanikiwa nita upload picha ya maiti yake.

Hali ya hewa imetulia kidogo na shuguli za kumtumikia kaburu zimeanza mnamo 1330hrs, kwa ujumla kulikuwa na vitofali 34 vya dhahabu ( kila kitofali kina 24KG) vilivyo pona pona kutembea ( ila nawalaumu hawa ma intruders kwa uchoyo wao!)

KUTOKA FIKRAPEVU:

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha nzito za kivita, wamevamia Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), na kuiteka ndege ndogo iliyokuwa imebeba dhahabu kutoka mgodini hapo, kwa ajili ya kuikisafirisha kwenda nje ya nchi.

Tukio hilo limetokea hii leo majira ya saa 5:55 asubuhi, katika uwanja wa ndege wa mgodi huo uliopo umbali wa kilomita 5 kutoka katikati ya mji wa Geita, na kwamba majambazi hayo yaliyodaiwa kujifunika nyuso zao, yaliishambulia ndege hiyo kwa risasi za moto, kwa lengo la kutaka kupora dhahabu hizo zenye mabilioni ya fedha.

Habari kutoka eneo la tukio zilizoifikia FikraPevu, zinaeleza kwamba, wakati majambazi hayo yakiimiminia ndege hiyo risasi, huku yakifyatua ovyo risasi nyingine hewani, askari polisi Wilaya ya Geita walifanikiwa kufika eneo hilo haraka, kisha kuanza kupambana na watu hao kwa risasi za moto, kabla majambazi hayo hayajakimbia na kuliua jambazi moja.

Katika majibizano hayo ya risasi, askari polisi walifanikiwa kuliua jambazi moja baada ya kulimiminia risasi kifuani, na kwamba kabla ya jambazi hilo kuuawa na polisi lilikuwa limejeruhiwa vibaya na mmoja wa walinzi wa mgodi huo ambaye ni raia wa nchini Afrika Kusinia.

Dhahabu iliyonusurika kuporwa na majambazi hao inadaiwa kuwa ilikuwa ni zaidi ya kilo 1,000, ambapo ilikuwa imegawanywa katika maboksi 16 huku kila boksi moja likiwa na matofali manne ya dhahabu, na kwamba kila tofari moja linadaiwa lilikuwa na ujazo wa kilo 25.


jambazi-geita.jpg


Pichani: Wakazi wa Wilaya ya Geita mkoani Mwanza, wakiangalia mwili wa mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi (jina hajafahamika), akiwa ni mmoja wa watu wanne waliyovamia mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), akiwa amekufa baada ya kupigwa risasi na askari polisi katika jaribio hilo la kutka kupora dhahabu jana. (Picha na Sitta Tumma)

Habari zaidi - http://www.fikrapevu.com/biashara-n...shambulia-ndege-ya-dhahabu-geita-mmoja-auwawa


PICHA ZAIDI kwa hisani ya
kanta (JF member):

jambazi-geita1.jpg

jambazi-geita2.jpg
 
ayallaaa ndili limezimwa ,ulizia utakuta kuna MKUBWA anahusika hapo,maana ndo Makada wa Magamba huko mikoani,mtu anatoa msaada wa milioni 500 ametoa wapi?Uchumi huu hu wa tanzania?
 
GOOD ATTEMPT. Kama waliofanikisha kulizima sakata hilo ni WATANZANIA, KIFO HALALI YAO. Nategemea waliohusika kuzima watanzania kuchukua MADINI YAO kuwa ni wazungu tu, kwani wanapeleka kwao
 
Lakini wangevuta subira wakalipua hata ndege, halafu wananchi wakawa wa kwanza kufika eneo la tukio kuokota dhahabu.
 
Jaribio la kutaka kuiba kiasi kikubwa sana cha dhahabu ktk mgodi wa Geita mchana huu mida ya 11:30hrs na watu wenye silaha nzito za kivitaa limezimwa na walinzi wa mgodi ( snipers &quick respond unit force wakishilikiana na makomandoo walinzi wa ndege inayosafirisha dhahabu) mpaka mida hii imethibitika watu 2 wamepoteza maisha.

Jaribio hilo limefanyika Ktk airport ya mgodini wakati dhahabu hiyo ikipakiwa ktk ka ndege special
tayari kwa kusafirishwa kwenda South Africa, adi mida hii wana Geita bado tunasikia milio ya risasi zikilindima maporini na ving'ora vya ambulance za mgodini zikiwabeba majeruhi wengi wao ni walinzi wa wa mgodi, polisi walitarifiwa mapema kabisa lakini bado wanajipanga namna ya kufika eneo la tukio!

Tutazidi kuajuza kadri nitavyo pata habari zaidi.
HAO WEZI walikosea stepu gani aisee?
 
Wadau,nasikia GGM kunawaka moto sasa hivi,majambazi wamevamia mgodini na hivi sasa nasikia wanapambana na polisi pamoja na walinzi wa mgodi.Wamevizia msafara wa kusafirisha dhahabu, mtu mmoja ameuwawa na mwingine amejeruhiwa vibaya na hali bado haijakaa sawa.Nitawajuza zaidi endapo waliopo mgodini watanipa taarifa mapema.
 
Hawa watakuwa wanyarwanda.......watanzania hawawezi mikiki hii

watanzania waliotengenezwa na nyerere sio waliozalishwa na mfumo wa mwinyi, mkapa na kikwete, vizazi vitatu hivi wana hasira na wizi unaotendeka ndani ya nchi yao. usijidanganye eti sio watanzania, labda wanyarqwanda wanahusika kufanikisha upatikanani wa armaments tu, lakini uchoraji wa ramani na utekelezaji ni kizazi cha Mwinyi, Mkapa na Mrisho
 
Ni kweli kuna majambazi yamevamia escort ya Gold Shiftment mapambano yanaendelea lkn cjapata taarifa za watu kufa tusubiri tutawajuza
 
Si deal ingetik tu asee... Kama vipi walipue hiyo ndege inayopeleka zawadi zetu kwa makaburu.
 
Wadau,nasikia GGM kunawaka moto sasa hivi,majambazi wamevamia mgodini na hivi sasa nasikia wanapambana na polisi pamoja na walinzi wa mgodi.Wamevizia msafara wa kusafirisha dhahabu, mtu mmoja ameuwawa na mwingine amejeruhiwa vibaya na hali bado haijakaa sawa.Nitawajuza zaidi endapo waliopo mgodini watanipa taarifa mapema.

Mkuu tunasubiri updates,Geita home aiseeee
 
Back
Top Bottom