bmk
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 571
- 857
Habarini za jumapili?
NAOMBA MODS MSIFUTE UZI HUU
Leo nikiwa kanisani aliyehubiri katufundisha somo moja la Macho ya mwilini na macho yasiyoonekana. Macho yasioonekana ni macho yanayokuonyesha toka ndani nini unafanya na unachokifanya ni sahihi ama si sahihi...Binafsi nimejifunza sana kuhusu somo mpaka nikaamua kulibadili kwenye siasa na kuona namna gani macho yangu yanavyonisuta kwa yale hasa tunayafanyayo sisi tulio madarakani.
Ni wazi kuwa wengi wetu tumejaa UNAFKI wa hali ya juu sana, Kuna mambo mengi tunatenda DHAMBI kwa kukusudia kabisa ili kulinda MKATE/PESA/FURSA zipatikanazo huku.
Zaidi sana ya hayo, kuna vitu jamani sisi tulio CCM tunasutwa mioyo yetu kuwa tunakosea sana sana sana...Ni vile tu vyombo vya dola vinatulinda sana...
Kunayo mengine mengi tunayapatia sema tu, hawa wapinzani kila kitu wanapinga hata vilivyo vya haki
mfano: ●ujenzi wa reli (tupo sahihi kabisa)
● ununuzi wa ndege (tumekosea aisee)
● ule mradi wa umeme kule rufiji (tungeachana nao kwa sasa, tuongeze nguvu kwenye umeme wa gesi kama alivyoanzisha kikwete)
● Kuwabana wapinzani na kuwanyanyasa, si haki kwa kweli kwasababu miaka 20 iliyopita karibu wizi mwingi wao ndo waliogundua na kuupigia kelele sana hatimaye wahusika kuwajibishwa
● Ila hili la Lisu jamani, HAPANA HAPANA HAPANA. aliyefanya hivi ni mnyama haswa inabidi atafutwe akamatwe na sheria ichukue mkondo wake...tuna kila sababu ya kukataa unyama kama huu kwa sababu mtu anakukosoa, kama unaona umekosa, jirekebishe, kama hujakosea mpuuzie fanya yako...kwa hili mwenyekiti wetu mstaafu aliliweza sanaa.....
Niseme tu kwamba, hatuwezi kufanya mambo yote kwa usahihi, tunahitaji jicho la pembeni kutukosoa, kutupinga ili turudi kwenye mstari. Lakini UBABE wetu, JEURI yetu nina IMANI kabisa kuna watanzania wengi tunawaumiza ni vile tu WOGA wao ndiyo unaficha haya yote.
Na kwanamna ninavyojua haitakuja tokea watanzania woote siku moja wakajitokeza barabarani kutukataa sisi CCM sina hakika labda baada ya kufariki. Kwanamna nionavyo wamejawa UWOGA/WANAFKI na ndiyo maana tuna nguvu za kufanya chochote tutakacho...
Niwaombe wanachama wenzangu, kuwa KARMA ipo leo twatendea wao haya...kesho/keshokutwa yataturudia sisi vile vile kwa namna tulivyowatendea....Tuache UNAFKI kutetea hata VIBAYA. Haiwezekani watanzania wenzetu wanapotea/wanafungwa/wanapigwa marisasi/wanaonewa na anayefanya yupo ndani yetu..ila tumejawa unafki wa kumtetea kisa kulinda Vyeo/chama/n.k n.k.
KUNA SIKU YETU INAKUJA.
Namshukuru MUNGU nimeyatoa ya moyoni, sijasaliti chama, nimeongea kile ambacho macho yangu yameona, na yananisuta kwa UBAYA HUU TUNAOWAFANYIA WATANZANIA WENZETU huku tukijinadi kuwa TUNAWAJALI MASKINI, TUPO KWA AJILI YAO...
Mungu kibariki chama chetu, ibariki Tanzania.
Ahsanteni.
Sent using Jamii Forums mobile app