Japokuwa upinzani wana mapungufu yao, hata sisi kuna vingi tunakosea

bmk

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
527
1,000
Habarini za jumapili?

NAOMBA MODS MSIFUTE UZI HUU

Leo nikiwa kanisani aliyehubiri katufundisha somo moja la Macho ya mwilini na macho yasiyoonekana. Macho yasioonekana ni macho yanayokuonyesha toka ndani nini unafanya na unachokifanya ni sahihi ama si sahihi...Binafsi nimejifunza sana kuhusu somo mpaka nikaamua kulibadili kwenye siasa na kuona namna gani macho yangu yanavyonisuta kwa yale hasa tunayafanyayo sisi tulio madarakani.

Ni wazi kuwa wengi wetu tumejaa UNAFKI wa hali ya juu sana, Kuna mambo mengi tunatenda DHAMBI kwa kukusudia kabisa ili kulinda MKATE/PESA/FURSA zipatikanazo huku.

Zaidi sana ya hayo, kuna vitu jamani sisi tulio CCM tunasutwa mioyo yetu kuwa tunakosea sana sana sana...Ni vile tu vyombo vya dola vinatulinda sana...

Kunayo mengine mengi tunayapatia sema tu, hawa wapinzani kila kitu wanapinga hata vilivyo vya haki

mfano: ●ujenzi wa reli (tupo sahihi kabisa)
● ununuzi wa ndege (tumekosea aisee)
● ule mradi wa umeme kule rufiji (tungeachana nao kwa sasa, tuongeze nguvu kwenye umeme wa gesi kama alivyoanzisha kikwete)
● Kuwabana wapinzani na kuwanyanyasa, si haki kwa kweli kwasababu miaka 20 iliyopita karibu wizi mwingi wao ndo waliogundua na kuupigia kelele sana hatimaye wahusika kuwajibishwa
● Ila hili la Lisu jamani, HAPANA HAPANA HAPANA. aliyefanya hivi ni mnyama haswa inabidi atafutwe akamatwe na sheria ichukue mkondo wake...tuna kila sababu ya kukataa unyama kama huu kwa sababu mtu anakukosoa, kama unaona umekosa, jirekebishe, kama hujakosea mpuuzie fanya yako...kwa hili mwenyekiti wetu mstaafu aliliweza sanaa.....

Niseme tu kwamba, hatuwezi kufanya mambo yote kwa usahihi, tunahitaji jicho la pembeni kutukosoa, kutupinga ili turudi kwenye mstari. Lakini UBABE wetu, JEURI yetu nina IMANI kabisa kuna watanzania wengi tunawaumiza ni vile tu WOGA wao ndiyo unaficha haya yote.

Na kwanamna ninavyojua haitakuja tokea watanzania woote siku moja wakajitokeza barabarani kutukataa sisi CCM sina hakika labda baada ya kufariki. Kwanamna nionavyo wamejawa UWOGA/WANAFKI na ndiyo maana tuna nguvu za kufanya chochote tutakacho...

Niwaombe wanachama wenzangu, kuwa KARMA ipo leo twatendea wao haya...kesho/keshokutwa yataturudia sisi vile vile kwa namna tulivyowatendea....Tuache UNAFKI kutetea hata VIBAYA. Haiwezekani watanzania wenzetu wanapotea/wanafungwa/wanapigwa marisasi/wanaonewa na anayefanya yupo ndani yetu..ila tumejawa unafki wa kumtetea kisa kulinda Vyeo/chama/n.k n.k.

KUNA SIKU YETU INAKUJA.

Namshukuru MUNGU nimeyatoa ya moyoni, sijasaliti chama, nimeongea kile ambacho macho yangu yameona, na yananisuta kwa UBAYA HUU TUNAOWAFANYIA WATANZANIA WENZETU huku tukijinadi kuwa TUNAWAJALI MASKINI, TUPO KWA AJILI YAO...

Mungu kibariki chama chetu, ibariki Tanzania.

Ahsanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
5,632
2,000
Na Mungu akubariki kama kweli umeweza kuyaona mateso ya watanzania unaosababishwa na chama chako. Uanze kuwaombea wenzako wanaolinda nafasi zao wafunguliwe macho ya rohoni; kwanza hii hali haihitaji hata macho ya rohoni bali yakawaida tu maana kila kitu kipo dhahili. Pia wajazwe na roho za huruma juu ya watanzania wenzao, mama zao, dada, kaka na wadogo zao wanaoteseka kwa kukosa mahitaji muhimu huku wakisikia kuwa kuna trilioni 1.5 alafu tena trillion 2.4 hazijulikani zimetumikaje.
Watanzania hatujazoea kuuwana kisa Siasa.
Mungu atusaidie wote, hii si nchi ya kikundi fulani bali ni ya watanzania wote kwa manufaa ya vizazi vyetu vijavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,916
2,000
Ungesaidia sana kama ungewaambia wenzako kuwa chanzo cha chuki yote hii ni huyo mwenyekiti wenu kuwa na moyo wa kikatili kinyume na mlivyo mfikiria kabla hamja mchagua. Nina hakika tabia hizi zingekuwa wazi pengine hakuna mtu angesema apewe bendera kuwakilisha chama chenu.
Sasa hivi anakunywa damu ya wapinzani wake wa nje, kesho atawageukia wa ndani ya chama chake na kuwatafuna kabisa. Hamko salama hata kidogo, ni sawa na anayefuga chatu maana siku akikua lazima ammeze
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,505
2,000
Habarini za jumapili?

NAOMBA MODS MSIFUTE UZI HUU

Leo nikiwa kanisani aliyehubiri katufundisha somo moja la Macho ya mwilini na macho yasiyoonekana. Macho yasioonekana ni macho yanayokuonyesha toka ndani nini unafanya na unachokifanya ni sahihi ama si sahihi...Binafsi nimejifunza sana kuhusu somo mpaka nikaamua kulibadili kwenye siasa na kuona namna gani macho yangu yanavyonisuta kwa yale hasa tunayafanyayo sisi tulio madarakani.

Ni wazi kuwa wengi wetu tumejaa UNAFKI wa hali ya juu sana, Kuna mambo mengi tunatenda DHAMBI kwa kukusudia kabisa ili kulinda MKATE/PESA/FURSA zipatikanazo huku.

Zaidi sana ya hayo, kuna vitu jamani sisi tulio CCM tunasutwa mioyo yetu kuwa tunakosea sana sana sana...Ni vile tu vyombo vya dola vinatulinda sana...

Kunayo mengine mengi tunayapatia sema tu, hawa wapinzani kila kitu wanapinga hata vilivyo vya haki

mfano: ●ujenzi wa reli (tupo sahihi kabisa)
● ununuzi wa ndege (tumekosea aisee)
● ule mradi wa umeme kule rufiji (tungeachana nao kwa sasa, tuongeze nguvu kwenye umeme wa gesi kama alivyoanzisha kikwete)
● Kuwabana wapinzani na kuwanyanyasa, si haki kwa kweli kwasababu miaka 20 iliyopita karibu wizi mwingi wao ndo waliogundua na kuupigia kelele sana hatimaye wahusika kuwajibishwa
● Ila hili la Lisu jamani, HAPANA HAPANA HAPANA. aliyefanya hivi ni mnyama haswa inabidi atafutwe akamatwe na sheria ichukue mkondo wake...tuna kila sababu ya kukataa unyama kama huu kwa sababu mtu anakukosoa, kama unaona umekosa, jirekebishe, kama hujakosea mpuuzie fanya yako...kwa hili mwenyekiti wetu mstaafu aliliweza sanaa.....

Niseme tu kwamba, hatuwezi kufanya mambo yote kwa usahihi, tunahitaji jicho la pembeni kutukosoa, kutupinga ili turudi kwenye mstari. Lakini UBABE wetu, JEURI yetu nina IMANI kabisa kuna watanzania wengi tunawaumiza ni vile tu WOGA wao ndiyo unaficha haya yote.

Na kwanamna ninavyojua haitakuja tokea watanzania woote siku moja wakajitokeza barabarani kutukataa sisi CCM sina hakika labda baada ya kufariki. Kwanamna nionavyo wamejawa UWOGA/WANAFKI na ndiyo maana tuna nguvu za kufanya chochote tutakacho...

Niwaombe wanachama wenzangu, kuwa KARMA ipo leo twatendea wao haya...kesho/keshokutwa yataturudia sisi vile vile kwa namna tulivyowatendea....Tuache UNAFKI kutetea hata VIBAYA. Haiwezekani watanzania wenzetu wanapotea/wanafungwa/wanapigwa marisasi/wanaonewa na anayefanya yupo ndani yetu..ila tumejawa unafki wa kumtetea kisa kulinda Vyeo/chama/n.k n.k.

KUNA SIKU YETU INAKUJA.

Namshukuru MUNGU nimeyatoa ya moyoni, sijasaliti chama, nimeongea kile ambacho macho yangu yameona, na yananisuta kwa UBAYA HUU TUNAOWAFANYIA WATANZANIA WENZETU huku tukijinadi kuwa TUNAWAJALI MASKINI, TUPO KWA AJILI YAO...

Mungu kibariki chama chetu, ibariki Tanzania.

Ahsanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
woga wetu ndo umasikini wetu, wa watoto wetu na wajukuu zetu.The ball is in our hands
 
okiwira

JF-Expert Member
Jul 23, 2018
1,562
2,000
Hakika Demokrasia imetamalaki CHADEMA vua gamba vua gwanda vaa uzalendo?

Ungesaidia sana kama ungewaambia wenzako kuwa chanzo cha chuki yote hii ni huyo mwenyekiti wenu kuwa na moyo wa kikatili kinyume na mlivyo mfikiria kabla hamja mchagua. Nina hakika tabia hizi zingekuwa wazi pengine hakuna mtu angesema apewe bendera kuwakilisha chama chenu.
Sasa hivi anakunywa damu ya wapinzani wake wa nje, kesho atawageukia wa ndani ya chama chake na kuwatafuna kabisa. Hamko salama hata kidogo, ni sawa na anayefuga chatu maana siku akikua lazima ammeze
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,391
2,000
Huwanawasikiza wafuatao
Job ndugai
Tulia
Livingston... Kibajaji
Jenista mhagama
Msukuma
Juma nkamia
Stellah manyanyaso
Nk

Sielewi na sijuwi mpaka Leo ndani ya akili na vichaa vyao kama kile wakinenacho kinatoka ndani ya roho zaho zako.
 
Ni wachache kati ya wengi waliojaa unafki sana, na hawa watu wanatafuta vyeo kwa kila hali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
doup

JF-Expert Member
Feb 26, 2009
2,171
2,000
Naamini stglers gorge bado mko kwenye right track. Mengine ya kiovu sitaki kuyasema ...
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,391
2,000
Matumizi mabovu ya
polisi
mahakama
Bunge
nk
Dhidi ya Uhuru wa RAIA kujieleza, kukosoa, kuchaguwa na kufanya siasa katika usawa wa vyama vyote.

Tanzania na Watanzania tunaonekana kituko Duniani kote.

CCM wafahamu 100%

Hakuna marefu yasio na ncha

Na lolote lililo na mwanzo halikosi mwisho.
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,505
2,000
Kama imefikia hatua unamfananisha JPM na GADAFFI basi hakika ataenziwa daima wengi watalia kwa ajili yake.
Watalia?labda wafia chama na wafia matumbo yao kama yeye.ila wafia Tanzania hamna hata mmoja huyu jamaa na siasa zake nyepesi anatuharibia nchi na kutuchelewesha sana
 
okiwira

JF-Expert Member
Jul 23, 2018
1,562
2,000
Jpm angekuwa kama Gadaffi Afrika ingejivunia ondoa wachumia tumbo.

Watalia?labda wafia chama na wafia matumbo yao kama yeye.ila wafia Tanzania hamna hata mmoja huyu jamaa na siasa zake nyepesi anatuharibia nchi na kutuchelewesha sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom