Japo wako kimya, Mkapa na Kikwete wanaridhika na hoja ya kutaka kumuongezea muda Magufuli?

Kama JPM akiendelea kuna uwezekano JK nae akaja kungombea tena
Umri utakuwa ushamtupa,vipi Kama aliyepo akaenda Hadi 2040, madaraka ni matamu kwa mwafrika ni ngumu Sana kuachia thus unaona Africa inawaka Moto kila sehemu kugombea kunufaika na Kodi za wananchi.Maana Hakuna biashara yenye ubilionea Mkubwa Kama uraisi
 
Hawa watu wamekuwa disappointment kubwa sana. Baada ya kutuletea hili balaa kubwa sana Nchini wamekuwa kimya sana ukiondoa mara chache ambazo wamezungumza juu juu bila kuweka msisitizo wa nguvu kisha kuingia mitini kwa kipindi kirefu huku dikteta akiendelea kuchezea katiba, Bunge na mahakama.
Ni wanufaika labda tu Kama wangekuwa hawanufaiki wangeshaungana na wananchi.Kila mmoja hapo ana maslai wengine watoto wao ni wabunge,maDC,mawaziri, mwingine mwanae anapigiwa chapuo kurithi Zanzibar.Wakifunua mdomo means ni kuhatarisha vitumbua vya watoto zao.
Waamuzi wa mwisho ni wananchi.
 
Kila zama na zama zake, wao kila mmoja wao alikuwa na zama yake, ukimaliza zama yako inakuwa imepita, unatulia na kujilia vizuri pensheni yako, ya zama ya mwenzio unamwachia mwenyewe.

Aliyetaka katiba ibadilishwe ili Magufuli aendelee sio Magufuli ni Mbunge na Spika akaridhia kuwa hoja hiyo iletwe Bunge lijalo, lakini rais Magufuli hajataka yeye, na hata hoja hiyo ikiletwa na ikapita, maadam rais Magufuli aliisha toa msimamo wake kuhusu hili, then muda wake ukifika hatazidisha hata sekunde moja!.
P
Umeshakuwa lumumba buku saba
 
Mkwere hawezi kuacha kumpigia chapuo yule niguse ninuke Memba tunaambiwa ni dugu yake baba moya mama moya , dugu wa damu nae Mkaa hapa anafagilia kiroho Mkulu aongezwe muda sababu za kidini na kiseminari! bongo raia akili kubwa!
Mbona JPM sio mseminari
 
Ni wanufaika labda tu Kama wangekuwa hawanufaiki wangeshaungana na wananchi.Kila mmoja hapo ana maslai wengine watoto wao ni wabunge,maDC,mawaziri, mwingine mwanae anapigiwa chapuo kurithi Zanzibar.Wakifunua mdomo means ni kuhatarisha vitumbua vya watoto zao.
Waamuzi wa mwisho ni wananchi.
Kuna mtoto wa Mkapa anayefaidika na hii mifumo ya kiupendeleo ?
 
Najiuliza tu.

Kama Nyerere angetaka kuendelea mwaka 1985.

Kama Mwinyi angetaka kuendelea mwaka 1995.

Kama Mkapa angetaka kuendelea mwaka 2005.

Kama Kikwete angetaka kuendelea mwaka mwaka 2015.

Je ramani ya Tanzania kisiasa ingekuwaje leo?
 
Uko sahihi P
Kila zama na zama zake, wao kila mmoja wao alikuwa na zama yake, ukimaliza zama yako inakuwa imepita, unatulia na kujilia vizuri pensheni yako, ya zama ya mwenzio unamwachia mwenyewe.

Aliyetaka katiba ibadilishwe ili Magufuli aendelee sio Magufuli ni Mbunge na Spika akaridhia kuwa hoja hiyo iletwe Bunge lijalo, lakini rais Magufuli hajataka yeye, na hata hoja hiyo ikiletwa na ikapita, maadam rais Magufuli aliisha toa msimamo wake kuhusu hili, then muda wake ukifika hatazidisha hata sekunde moja!.
P
 
Hoja ya kuongezewa muda hata Rais Mkapa akiwa madarakani ilitolewa na mmoja wa mawakili nguli Masumbuko Lamwai na wengine wengi. Rais Mkapa aliheshimu katiba na kuondoka madarakani.
Hoja ya kuongeza muda wakati wa JK napo iliibuka, yet JK akaheshimu katiba.

Nataka kuamini JPM ni mtu muungwana na mara kwa mara amekuwa akijinasibu kuunga mkono mema mengi yalioasisiwa na Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere. Kwa kuwa Mwl. Nyerere alikuja na hoja ya kutaka Rais akae madarakani kwa mihula miwili 5+5; bila shaka JPM akaondoka madarakani 2025 baada ya uchaguzi mkuu.

Tanzania imekuwa nchi ya mfano wa kukabidhi madaraka na wanaokabidhi madaraka wakaishi kwa amani pasi kubugudhiwa na kutokea kwenye hafla mbalimbali pale inapohitajika.

Tujipe muda, nadhani, mzee atakuwa anapatikana Chato mara baada ya kumaliza ungwe yake.
Umeongea vizuri haya huwa yanasemwa sana
 
Wanataka aendelee kwa sababu ni katika kipindi cha Magufuli ndio wana uhakika wa kuendelea kula, kinyume na huyo watahangaika sana
 
Back
Top Bottom