Japo Valentine's ilikuwa tarehe 14 February, kwa TotalEnergies bado wanaendelea kumwaga zawadi za Valentine's hadi Tarehe 27 Februari

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,557
22/02/2022 TotalEnergies Kuendeleza Valentine Hadi Tarehe 27 February

Japo Sikukuu ya wapendanao, yaani Valentine Day, huadhimishwa kwa siku moja tuu, siku ya tarehe 14 ya Mwezi Februari kila mwaka, lakini ili kueneza upendo zaidi na zaidi kwa Watanzania, Kampuni ya mafuta ya TotalEnergies imeamua kuiendeleza sikukuu hii hadi mwisho wa mwezi huu wa Februari, kwa kuendelea kugawa zawadi za Valentine katika vituo vya mafuta vya TotalEnergies hadi tarehe 27 ya mwezi huu.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total, Getrude Mpangile, katika kituo cha mafuta cha TotalEnergy Samora jijini Dar es Salaam.


TotalEnergy Valentine- Photo 1 .jpg


Mpangile amesema, kwa kampuni ya mafuta ya Total, kwao Valentine sio maadhimisho ya siku moja tuu, kwa TotalEnergies, Valentine ni msimu, hivyo kampuni hiyo imeamua kuuendeleza msimu wa Valentine hadi tarehe 27 Mwezi huu wa February kwa wateja wa huduma za mafuta na bidhaa katika maduka ya Bonjour yaliyopo kwenye vituo vyote vya Total, kuendelea kujipatia zawadi za Valentine.

Meneja wa Maduka ya Bonjour, ya Kampuni ya mafuta ya TotalEnergies, Jane Mwita, amesema zawadi hizo sio kwa wenye magari tuu, bali watu wote, watakaonunua bidhaa kwenye maduka ya Bonjour, watapatiwa zawadi ya maalum yenye ujumbe wa kueneza na kuendeleza upendo kwa jamii.

Promotion hii ya kuendeleza upendo kupitia vituo vya mafuta vya TotalEnergy, inafanyika katika vituo vyote zaidi ya 100 vya TotalEnergy nchi nzima na itaendelea hadi tarehe 27 February, 2022.

TotalEnergy Valentine Photo 2.jpg
TotalEnergies Valentine Photo 6.jpg
TotalEnergies Valentine Photo 5.jpg
Totalenergy Valentine Photos 7.jpg

Changamkia fursa.
Paskali
 
Mkuu kuna vijana wengi ni majobless humu..kama ikikupendeza wape connection kaka,najua una ushawishi mkubwa kwa hao jamaa..
 
Back
Top Bottom