#COVID19 Japo Chanjo ni hiyari, ila ni muhimu. Hupandi Ndege bila cheti cha Kupima COVID19. Kama unasafirisafiri, Chanjo ni Muhimu

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Déclaration of Interest.
Mimi Pascal Mayalla ni pro Vaccination ya Covid 19 na nimechanja chanjo ya Corona, na nawahimiza Watanzania, tuchanje.

Niko hapa Terminam 3 Airport ya DIA, nimeshuhudia baadhi ya watu wachache wakirudi makwao kwa kakataliwa kusafiri kutokana na kutokuwa na cheti cha kipimo cha Corona hivyo kurudishwa nyumbani na mabegi ya, hivyo kosa la kukosa cheti cha kupima Covid 19, kunaweza kukusababisha safari yako ya ulaya kuishia Airport !.

Kumbe japo chanjo ya Corona ni hiyari, lakini kwa watu wanaotumia usafiri wa anga, ndege, au kukwea pipa kwa safari za kimataifa, chanjo hii ni muhimu. Ili upande ndege, ni lazima upime Corona na kupewa cheti kinachoonyesha hauna Corona. Hivyo chanjo ya Corona ni muhimu ili kujiihakikishia usalama usiipate Corona kirahisi , kwasababu siku hizi, ili usafiri nje, ni lazima upime Corona , na kuonyesha cheti kuwa umepima Corona na huna Corona ndio unapanda ndege. Ukichanja chanjo ya Corona, unazuia uwezekano wa wewe kupata Corona kwa urahisi.

Mtu hupandi ndege bila ya kuwa na cheti kupima Corona!, hivyo ili usipate Corona ni muhimu sana kuchanja chanjo ya Corona ili kujiepusha na kupata Corona.

Zamani ukiingia tu Airport unawahi counter ya check in. Sasa ukiingia Airport unaanzia meza ya vérification ya cheti cha kupima Corona. Baada ya kuwa cleared kuwa umepima Corona na umekutwa hakuna ndio una proceed to check in counter.

Hivyo natoa wito, kama wewe ni mtu wa kusafiri safiri, au kazi yako inahusisha safari za nje ya nchi, hata kama umeamua kuitumia hiyari yako kutochanja nakushauri nenda kachanje, ili kuwa na uhakika umejikinga Corona ili ukipata safari, uweusije na uhakika wa Usalama wako dhidi ya Corona, kwa maana utapima na kukutwa hauna, usije kulia na kusaga meno, kama jana pale airport.

Japo chanjo ya Corona ni hiari, kwa watu wanao safiri safiri, chanjo ya Corona ni muhimu sana, hivyo hata kama ulipanga kuitumia hiyari yako usichanje, nakushauri kachanje!

Paskali

Update 1
UFAFANUZI WA WIZARA YA AFYA

Hakuna sharti la chanjo ya Corona kwa wasafiri wanaokwenda nje ya nchi. Ni vema msafiri akauliza shirika la ndege analokwenda nalo pamoja na masharti ya nchi anayotembelea. Kwa zile nchi ambazo zinahitaji kipimo cha UVIKO-19 msafiri afanye kipimo hicho ndani ya masaa 24 hadi 48 kabla ya kuanza safari. Upimaji unafanyika kwa msafiri kufanya booking kupitia pimacovid.moh.go.tz ambapo atachagua kituo cha upimaji . Baada ya upimaji majibu yatatumwa kwake kwa njia ya barua pepe aliyotumia wakati wa booking. Akifika Airport cheti hicho kitahakikiwa katika dawati la afya. Unashauriwa kujiepusha na vyeti feki.

Kuhusu uzushi unaoenea kwamba Chanjo ya UVIKO-19 inatolewa mashuleni hiyo sio kweli,Chanjo zote zinatolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoainishwa na Chanjo hiyo inatolewa kwa makundi Yale matatu yalivyotangazwa.

Watoto sio walengwa wa Chanjo hii na vilevile hakuna kituo kwenye shule.

Imetolewa na ;
Catherine Sungura
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Afya
8/8/2021

UPDATE 2
Kufuatia upotoshaji uliotokana na thread hii, pale mwanzo kabla haijarekebishwa, mimi Pascal Mayalla naomba kuomba radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa na taarifa ya awali ambayo haikuwa sahihi. Naahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa serikali yetu kupitia Wizara ya Afya, na kushiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu na taarifa sahihi kuhusu chanjo ya Corona.

Kunapotokea kosa lolote, katika jambo lolote, kitu muhimu sio tuu kuangalia kosa lililotendeka, (actus reus), bali nia ya mtenda kosa, kama alikuwa na nia ya kutenda kosa (mens rea).

Na mwisho naomba kusisitiza kuwa japo kwa sasa chanjo ya Corona ni hiari, kitu kinachohitajika kabla ya kusafiri nje ni cheti cha kupima Corona, huko tuendako tutafikia mahali cheti cha chanjo ya Corona kitahitajika kabla ya kupata Visa za kuingia nchi fulani fulani, hivyo utafika muda chanjo ya Corona itakuwa ni hiari ya lazima.

Pasco Mayalla

Threads Nyingine za mwandishi huyu kuhusu Chanjo ya Corona



 
Chanjo ni muhimu sana kwa ustawi wa jamii na uchumi binafsi na taifa kwa ujumla hasa ikizingatiwa madhara ya uviko 19, lakini isiwe sababu ya kuingilia uhuru na uhiari wa watu.

Naomba kuuliza, watu wanapimwa ikiwa wanamaambukizi au hawana kabla ya kukwea pipa? Hilo ndio lingekua jambo la muhimu, kuhakikisha watu wanaopanda kwenye chombo hawana maambukizi. Kisha ije hilo la chanjo, ikumbukwe hata ukichanja unaweza kupata maambukizi na kuambukiza wengine.

Wakifanya hivyo nnachokiona watu watavipata hivyo vyeti vya kuonyesha umechanjwa hata kama kiukweli haujapatiwa chanjo, wale waliosafiri kwa kuwa na kadi za yellow fever bila kuchanjwa ni wengi tu.

Nna mfano hai wa mtu aliyechanjwa AstraZeneca, ikawa ndio kama ametibua ugonjwa. Tunapoongea ametoka kwenye mitungi jana.

Kwa utaratibu ulivyo, ntajisaliji kupata chanjo, ntaweka appointment, kituoni watafungua batch husika, kitavunjwa hicho kihifadhia dawa ya chanjo na sitachoma ila itaingizwa kwenye kumbukumbu kuwa ni miongoni mwa waliochanjwa.

Tusipoteze lengo kuu la kutokomeza na kupambana na huu ugonjwa, biashara na maslahi binafsi vikighubika huu mchakato tutegemee wengi kuutilia shaka na kutokuupokea.
 
Mkuu,

Hili la hiari ni la muda tu, tunakoelekea itakuwa ni lazima. Ulisikia jana CNN walimtimua mfanyakazi ambaye hajachanjwa? This is just a beginning, chief.

Kejuu
 
Back
Top Bottom