Uchaguzi 2020 Japo anafanya utani lakini ni kweli chakula kwa wanafunzi ni jambo la muhimu

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Mgombea wa Urais kupiti CHAUMMA amekuja na sera ya chakula kwa wanafunzi. Hii kitu niliielewa tangu awali lakini mahojiano yake ya dk 45 ITV yalinifanya nione kuwa mzee hayuko serious, wala hana mkakati wa kufikia anachokiwaza.

Nafsi iliniambia kuwa ni kweli chakula kwa wanafunzi ni shida sana,, hii ni kwa wote, wanafunzi wa kutwa na wa Bweni, kuanzia shule ya msingi hadi Chuo.

Wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari shule za kutwa hupewa pesa kidogo ya kununua karimati, bagia au mihogo ndio maisha yaliyoko kwenye shule zetu nyingi za binafsi na serikali. Sasa tufikirie kwa ukweli mtu kula muhugo na anashinda kutwa shuleni akisoma madubwasha ya tofauti tofauti.

Ukija kwa shule za bweni, binafsi na serikali chakula kipo ila sio cha kutosha. Kwa wale ambao mmesoma shule za bweni hasa za serikali mtakuwa mnajua misamiati ya kipindi kile kama 'kumiss' au 'Kupigwa panga' yaani unaweza kosa chakula au ukapunjwa chakula. Maisha yanakufundisha Survival kwamba lazima uwe mbabe au kiongozi ili upate zaidi.

Maisha haya ndio tulioshi ukirudi nyumbani umekonda unaambiwa unasoma sana kumbe na kukosa chakula bora inachangia, au kwa wale mlioko kazini hebu angalieni picha zenu mlipokuwa shuleni then ufananishe na picha zenu baada ya kuingia kazini na kula vizuri.

Niliona mantiki kubwa kwenye hoja za Rungwe na kama angesimamia kiasi cha kuistua serikali ingeweza kuchukua hoja na kuweka chakula kizuri shuleni.

Mimi nakumbuka miaka ya 2010 nikiwa Advance shule moja, Mbeya tulidai mboga za majani, walivyozileta ilikuwa ni kabichi ambazo mtu unawaza bora hata tusingedai, kabichi haikatwi yaani kama imepigizwa ukutani then wanachanganya na maharage.Siku ya kande ilikuwa ni siku ya kinyonge sana, kande mimoshi maharage ya kutafuta, yaani mchuzi mweupe, ratioya debe moja ya mahindi kwa maharage robo. Siku za nyama na wali zilikuwa ahueni lakini, juzi nilienda kujaribu kula nyama za sampuli ile hadi nikawaza nilikuwa napigania nini nilipokuwa shule.

Kwa wale mliopita shule za boarding, za serikali hasa vijijini ambazo zilikuwa na mashamba, mtakuwa mnakumbuka wizi ambao wanafunzi wanafanya kwa mashamba ya shule kama kuiba mahindi kabla hayajaiva na kuchoma ili kufanya maisha yaende, aidha wakati mwingine wanafunzi huiba kwenye mashamba ya wanakijiji mradi tu wajaribu kuongeza kitu kwenye msosi.

Hoja ya chakula ni nzito sana, Ukitaka waangalie sasa wanafunzi wa kkutwa wakiwa wanarudi kutoka shuleni mchana, nyuso zao zimechoka, wanasumbuliwa na kiu na njaa kiasi ambacho wanagombana na wazazi wao kinapokuja kipengele kwamba wabadili sare kabla ya kula.

Narudia kusema ndugu zangu! Mbali na utani anaofanya mzee Rungwe kwenye hoja zake, lakini hoja ya chakula kwa wanafunzi ni ishu serious.

Na tukumbuke msosi shuleni ni mbovu, kwa shule za serikali ni mbovu zaidi, kwa kipindi hiki ambacho tunataka kutokomeza zero, kweli tuangalie swala la chakula.

Natoa wito kwa Haki Elimu kuhusu hoja ya chakula
Wito kwa wanaharakati wa haki za binaadamu
Wito kwa wanaharakati wa watoto

Kulitazama swala hili kwa jicho pevu...

Namnukuu ndugu yangu mmoja kuhusu chakula, 'Hapa Tanzania wanaokula vibaya ni walioko jela, wakifuatiwa na wanafunzi'.

Signed

Oedipus
 
Ukipiga ubwabwa na maharage, kitaeleweka tu. Mzee Rungwe ana Sera zenye upekee sana
 
Kuna mwanafunzi yeyote kafa kwa njaa au utapia mlo? Mpaka afanye sera?
 
Mtoto wa chini ya miaka 14, jambo lake muhimu kabisa baada ya mama yake ni Msosi.

Rungwe asibezwe!!
 
Kweli aisee,

Kinaachotofautisha boarding schools na days schools ni availability ya msosii aisee
 
Back
Top Bottom