Japhet Kaseba atajinasuaje na tuhuma za kuteka na kutesa watu?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,794
FB_IMG_1522637303445.jpg

Hii kwanza ni kashfa kubwa kwake kwa chama cha ngumi Tanzania, wadau ndugu jamaa na marafiki.... Kwamba kazi yake rasmi sasa sio mchezo wa ngumi tena au ngumi mateke bali ameajiriwa kutesa na pengine kuua kabisa...
Akiwa ni kijana aliyependa sans mchezo wa kickboxing alifikia kilele cha mafanikio wakati wa kipindi cha Kikwete (rais)... Akiitangaza vema nchi yake kwa mialiko ya mapambano nje ya nchi... Ana mataji ya ushindi mengi tuu
Kipindi hicho hamasa ya michezo ilikuwa juu na vipaji vingi viliibuliwa... Kaseba alikuja kumalizia kipaji chake kwa kuacha kickboxing na kuingia kwenye ngumi za ridhaa kisha akapotea kwenye ramani ya michezo

Kuna video na mada hapa JF, ya mtu anayetuhumu kudhulumiwa mali zake na kutishiwa kuuliwa huku akiwahi kutekwa Beach na kupelekwa kuteswa kwenye nyumba moja huku mtesaji mkuu akiwa ni bondia Japhet kaseba
Kama hili ni kweli na kwa mafanikio aliyopata Kaseba enzi zake leo hii hakupaswa afanye kazi anayotuhumiwa kuifanya.. Kwa nafasi yake alitakiwa awe na uwekezaji fulani kwenye tasnia ya michezo.... Lakini maisha ya mastaa wa kiafrika yanatia simanzi sana....
Kaseba ni mfano wa wanamichezo wengi waliowatajirisha wengine huku wao wakiishia kufanya kazi chafu na kufa fukara....
Kila mtu anatamani kuishi maisha fulani na ku keep status... Lakini ikifika mahali hupati unachotaka kwa njia halali basi hujikuta mtu anajilipua na kufanya kazi yoyote alimradi tu anapata anachotaka
Je tuna wana michezo wangapi leo hii ambao hawajulikani walipo na shughuli wanazofanya? Kuna mambo muhimu kama taifa tumeyapa kisogo na kuamua kuifanya siasa ndio kila kitu....
Tuhuma hizi za Kaseba ni DOA kubwa kwa wanamichezo wetu lakini je... Baada ya hili ninini hatima yake!?
IMG_20180402_024554_664.jpg

Habari zaidi, soma=>Maovu ya GSM yaanikwa: Wahusishwa na watu wasiojulikana, Makonda aonywa kuwa karibu nao
 
Wakati ni kweli namlaumu Kaseba hebu tujiulize wanamichezo wetu huwa wanafaidika katika lipi zaidi yakuwa maarufu wasio na kitu?
Kuna haja ya kuangalia sera zetu na taratibu zetu za michezo na sanaa. Wana michezo wa bongo ni maskini wakiwa wanacheza na maskini zaid wakiwa wame staafu. Tupitie sera zetu upya. La si hvo tuta fuga kina kaseba wengi zaidi, tena kwa usawa huu wa vyuma kukaza! Lazma tutafutane.
 
Katika nyakati hizi ambapo siasa ndio kila kitu ni vigumu sana sekta nyingine kukumbukwa na hata zikikumbukwa ni kisiasa zaidi
 
Hii kwanza ni kashfa kubwa kwake kwa chama cha ngumi Tanzania, wadau ndugu jamaa na marafiki.... Kwamba kazi yake rasmi sasa sio mchezo wa ngumi tena au ngumi mateke bali ameajiriwa kutesa na pengine kuua kabisa...
Akiwa ni kijana aliyependa sans mchezo wa kickboxing alifikia kilele cha mafanikio wakati wa kipindi cha Kikwete (rais)... Akiitangaza vema nchi yake kwa mialiko ya mapambano nje ya nchi... Ana mataji ya ushindi mengi tuu
Kipindi hicho hamasa ya michezo ilikuwa juu na vipaji vingi viliibuliwa... Kaseba alikuja kumalizia kipaji chake kwa kuacha kickboxing na kuingia kwenye ngumi za ridhaa kisha akapotea kwenye ramani ya michezo

Kuna video na mada hapa JF, ya mtu anayetuhumu kudhulumiwa mali zake na kutishiwa kuuliwa huku akiwahi kutekwa Beach na kupelekwa kuteswa kwenye nyumba moja huku mtesaji mkuu akiwa ni bondia Japhet kaseba
Kama hili ni kweli na kwa mafanikio aliyopata Kaseba enzi zake leo hii hakupaswa afanye kazi anayotuhumiwa kuifanya.. Kwa nafasi yake alitakiwa awe na uwekezaji fulani kwenye tasnia ya michezo.... Lakini maisha ya mastaa wa kiafrika yanatia simanzi sana....
Kaseba ni mfano wa wanamichezo wengi waliowatajirisha wengine huku wao wakiishia kufanya kazi chafu na kufa fukara....
Kila mtu anatamani kuishi maisha fulani na ku keep status... Lakini ikifika mahali hupati unachotaka kwa njia halali basi hujikuta mtu anajilipua na kufanya kazi yoyote alimradi tu anapata anachotaka
Je tuna wana michezo wangapi leo hii ambao hawajulikani walipo na shughuli wanazofanya? Kuna mambo muhimu kama taifa tumeyapa kisogo na kuamua kuifanya siasa ndio kila kitu....
Tuhuma hizi za Kaseba ni DOA kubwa kwa wanamichezo wetu lakini je... Baada ya hili ninini hatima yake!? View attachment 731832
Halafu huyu jamaa amedanganya umri huyu. Hajazaliwa 1979, kaseba ni mzaliwa wa kuanzia mwaka 1974 kwenda chini.
 
Aisee, basi ujue siku zake zinakaribia Kwisha hapa duniani, mkuu hebu niwekee hapa hiyo clip au link niione
 
Jamaa Hapa Ndo Njia Yake Kubwa,anaendesha Rvr Sijui Gari Gani Hata Sielewi,life Style,kukosa Ufahamu Uchumi,na Kuwaza Kupanga Miaka Zaidi Ya Kumi Toka Hapa Nitakuwa Wapi,bado Kijana Na Ana Nguvu Ajirekebishe Alipokosea
 
J. Kaseba inaweza kusemwa ni sehemu ndogo, ndogo sana lakini muhimu, ya jambo kubwa zaidi. Picha imekuwa wazi zaidi. "Dude" limeamshwa!!

State Capture!!

Tukiwa wakweli, ni nani asiyeijua hii story Ofisi zinazohusika pale Mambo ya Ndani?
 
Hatari sana,watu tuliodhani wana hekima na heshima kumbe ni magaidi!!
Tumeshuhudia kwenye vyombo vya habari mbalimbali wakiiwakilisha nchi kwenye michezo kitaifa na kimataifa huku wakivalishwa bendera na Viongozi wakubwa,ajabu sana.
Watakufa midomo wazi.
 
Yule jomba aiyetoa ile video simuelewielewi.

Tusihukumu mapema, inawezekana hii ni sinema mpya ya April.
 
Tuguma ziwe za kweli ama za uwongo lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hawa wasanii na wanamichezo wetu na wanamuziki hujikuta hawanufaiki na wanavyovifanya mwisho wa siku hufanyishwa mambo ya ajabu ajabu kama hayo
 
Thomas mashali alikuwa kibaka magomeni kagera ,manzese na mwaka Jana akauliwa kwa wizi

Hawa mabondia akili finyu kwenye peak yao waliingiza pesa ila kutokuwa na manager ni tatizo na kutojielewa

Nasubiria abdallah ostaz rais wa chama cha ndondi atakavyotoa povu na kulaumu
 
Back
Top Bottom