Japhet Justine, Mkurugenzi mkuu wa benki mdogo kuwahi kutokea Tanzania!

jidanganye ukienda shuke ukatike mikono, uwe kipofu au kilema chochote halafu uendelee kuwa ceo.. labda kampuni iwe yako au ya baba yako

point yangu ni miaka 34 sio mtoto. kina ngowi hawajafika hiyo wana kampuni zao za mabilion..

Mkuu nakubaliana na wewe. lakini kama wenzangu walivyosema. Kila binadamu ana fungu lake. Ndo maana Macron amekuwa Rais wa Ufaransa ana miaka 39 wakati Trump amekuwa Rais akiwa na miaka 70.

Narudia, kila mtu ana fungu lake na amepangiwa jinsi atakavyofanikiwa. Yeye kuwa CEO na miaka 34 unaona ni mzee....wengine wanaona ni inspiration. In all tusilinganishe maisha. Kila mtu ana safari yake. Mafanikio hayana umri.
 
Watanzania tupunguze wivu kwa kijana mwenzetu

Tujifunze ku fight kama yeye
Mimi sina wivu maana hata mimi nina mafanikio yangu ambayo wewe huyajui, lakini mtu hawezi kupongezwa sababu ya umri mdogo tu. Hata mimi nikitaka sifa, nitaweka vyeti vyangu hapa ambavyo vina zaidi ya A 30! Kumbe kitu kizuri zaidi ni kuonyesha hizo A thelathin zimelisaidia nini taifa. Kwahiyo mimi siwezi kumuonea wivu huyo jamaa, labda C students ndo wataona maajabu na labda watakuwa na wivu.
 
Japhet Justine kwa mara nyingine tena amevunja rekodi za nchi hii baada ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa benki ya wanawake (TWB)...
Kiumri, ni kijana mdogo kabisa ( his age is around 34 yrs) kuwahi kushika cheo cha juu kama hicho katika sekta ya benki hapa nchini.
Ni kijana mdogo kiumri ila kichwani yuko very very smart...
Alimaliza shahada yake ya Bcom pale UDSM mwaka 2008, baadaye akafanya kazi ya uhasibu British council kabla ya kuhamia benki ya NMB. Huko nako alifanya vyema mpaka akapanda cheo na kufikia hatua ya kuongoza idara kubwa ya benki hiyo ya NMB.
Baada ya hapo pia alifanya kazi na benki ya ABC katika cheo kikubwa kabisa akiongoza kanda ya Mara....
Taarifa zinaonesha kuwa amepata pia mafunzo kwa ngazi ya masters nchini Afrika kusini.

View attachment 526837 View attachment 526838

Kabla ya Justine kuvunja rekodi hii, taarifa (nilizonazo) zinaonesha kuwa Patrik Schoeneborn ndiye alikuwa mkurugenzi mkuu mdogo kuliko wote hapa nchini, akiwa ni raia wa Ujerumani na mkurugenzi mkuu wa benki ya Access kabla ya kurudishwa kwao Ujerumani kushika nyadhifa za juu kwenye group!

View attachment 526839

Tunamtakia utendaji mwema kijana mwenzetu Justine katika kuingoza benki ya wanawake!
Kila laheri akaokoe jahazi maana hiyo Bank ilibaki hohe hahe kama Pale Mwanza ukiangalia branch yao yaani kama Frame ya M-pesa
 
miaka 34 ceo mshahara milion 15... samatta miaka 20 tp mazembe mshahara milion 20.. na baadae genk mshahara kwa wiki hatari..

hasheem miaka 20 nba mshahara milion 200...

diamond miaka 28 utajiri wa bilion...

kweli shule zinachelewesha maisha.. miaka 34 eti ni mdogo wakati umri wa kustaafu huo akifika samatta
Kwenye uchumi tunaita opportunity cost mkuu
 
Mkuu hivi umeelewa alichoongelea mtoa mada? Amesema mkurugenzi mkuu wa benki mdogo kuwahi kutokea. Hao unaotutajia ni wakurugenzi wakuu wa benki gani?
Kijamaa kina roho ya kutu kweli kwa umri huo lazima aitwe mdogo kwa cheo chake ni sawa na kusema Tanzania ya sasa ipate raisi mwenye 40 yrs au Macron kwa mfano lazima tumuite mdogo kwa nafasi ile hata kama anazidiwa hela na Mbape
 
Mimi sina wivu maana hata mimi nina mafanikio yangu ambayo wewe huyajui, lakini mtu hawezi kupongezwa sababu ya umri mdogo tu. Hata mimi nikitaka sifa, nitaweka vyeti vyangu hapa ambavyo vina zaidi ya A 30! Kumbe kitu kizuri zaidi ni kuonyesha hizo A thelathin zimelisaidia nini taifa. Kwahiyo mimi siwezi kumuonea wivu huyo jamaa, labda C students ndo wataona maajabu na labda watakuwa na wivu.
Mbona wamesema kwamba aliweza kupandshwa vyeo katika taasisi tofaut tofaut alizofanyia kaz kutokana na utendaji uliotukuka.
maana yake ni kwamba anafanya majukumu yake katika ubora unaotakiwa.
 
Mkuu nakubaliana na wewe. lakini kama wenzangu walivyosema. Kila binadamu ana fungu lake. Ndo maana Macron amekuwa Rais wa Ufaransa ana miaka 39 wakati Trump amekuwa Rais akiwa na miaka 70.

Narudia, kila mtu ana fungu lake na amepangiwa jinsi atakavyofanikiwa. Yeye kuwa CEO na miaka 34 unaona ni mzee....wengine wanaona ni inspiration. In all tusilinganishe maisha. Kila mtu ana safari yake. Mafanikio hayana umri.
Kula like milioni
 
Kwanini anaongoza Benki ya Wanawake au na yeye ni Mwanamke?,
 
Back
Top Bottom