Japan yasaidia Mwanza, Mara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Japan yasaidia Mwanza, Mara

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jun 6, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  SERIKALI ya Japan imetoa msaada wa zaidi ya Sh. Bilioni 14 kwa ajili ya kusaidia miradi ya maji katika vijiji 44 vilivyopo Mkoani Mwanza na Mara. Msaada huo ulitolewa jana na makabidhiano ya msaada huo ulifanyika katika ofisi ya Wizara ya Fedha na Uchumi jijini Dar es Salaam.

  Katika hafla hiyo ya makabidhiano, Balozi wa Japan Nchini Toshihisa Hasegawa alikabidhi msaada huo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Ramadahni Kijja.

  Katika hafla hiyo Wizara hiyo ilisaini misaada ya makubaliano kwa niaba ya Serikali.

  Balozi Hasegwa alisema kuwa wametoa fedha hizo ili kuweza kusaidia ujenzi wa miradi kadhaa ya maji safi na salama katika baadhi ya wilaya ya mikoa hiyo.

  Amesema lengo la kutoa misaada hiyo ni kutimiza ndoto ya Ubalozi huo kuondoa idadi ya watu ambao hawapati maji safi na salama.

  Amesema kuwa miradi hiyo ikikamilika kama ipasavyo watu watakaokuwa wakipata maji safi wataongezeka kutoka watu elfu tisa hadi kufikia elfu 55.

  Naye Katibu Kijja amesema kuwa wameshukuru kwa msaada huo waliopokea toka katika ubalozi huo na moja kwa moja fedha hizo zitaanza kazi stahili ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.
   
Loading...