Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Hizi fedha zanzibar wanapewa mgao mkubwa , wanatumia formula gani kuzigawa? Ukubwa wa eneo? Idadi ya watu? Au Maza hajui hesabu?
Labda wanalipwa na mgao wa "areas" yaani mgao wa zamani ambao hawakuupata, japo hawakushiriki kuulipa!! Najaribu kuwaza tu kigezo kinachotumika kuwapa Zenji mgao mkubwa sana ukizingatia ni "kasehemu" kaduchu sana ukilinganisha na Tanganyika!!
 
Hoja zako zipo wapi?
Je, Zanzibar wana Bajeti ya Ulinzi , Mambo ya ndani, nje, Wizara za muungano na taasisi zake?

Hoja yangu ni kwamba hayo mambo uliyoyataja ni masuala ya Muungano, yanahudimiwa kutokana na mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayahudumiwi na Tanganyika wala na Zanzibar. Zanzibar Ina Mambo yake ya kuhudumia.

Kuna sehemu umetaja kwamba elimu sio suala la Muungano. Hapo umepotosha. Elimu ya msingi ndio ambayo sio ya Muungano.

Umezungumzia wanufaika wa Bodi ya Mkopo wa Elimu ya Juu kuwa Mkopo ule kwao ni Grants. Hivi hua mnalipwa kuandika uongo na kueneza chuki kwa wananchi?

Na hata habari ya umeme umeizungumzia ki upotoshaji.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Yanahudumiwa na Tanganyika kwa sababu mambo yote ya Tanganyika yamewekwa kwenye serikali ya muungano!! Hapo ndipo kiini macho kilipo!! Hata bajeti ya kujenga choo cha ofisi ya kata ni suala la muungano!! Hii ni kwa sababu hakuna serikali ya Tanganyika!!
 
Labda wanalipwa na mgao wa "areas" yaani mgao wa zamani ambao hawakuupata, japo hawakushiriki kuulipa!! Najaribu kuwaza tu kigezo kinachotumika kuwapa Zenji mgao mkubwa sana ukizingatia ni "kasehemu" kaduchu sana ukilinganisha na Tanganyika!!
Mkuu udogo wake unakuzwa sana na kile wanachodai.

Vigezo vinavyotumika ni sehemu ya kero na mikopo na misaada ilikuwa lalamiko la Zanzibar.
Utashangaa Wazanzibar hawaulizi madeni nani analipa.
Wazazibar hawaulizi nani anaendesha muugano na kwa rasilimali zipi

Wao wapo ndani ya muungano kudai kugawana mikopo, misaada na nafasi za ajira na fursa tu

Kero 11 zimemalizwa kwa siri sana, hakuna anayejua nini kimeamuliwa na Mtanganyika aliwakilishwa na nani. Ndani ya kamati ya VP wapo Wazanzibar sasa Mtanganyika anawakilishwa na nani na nani alikuwepo kulinda masilahi ya Tanganyika

Hii siri ya kero za muungano haizungumzwi Wabunge CCM hawataki kuhoji.

Ni mbunge mmoja tu aliyejali masilahi ya Tanganyika, Mh Ali Kessy wa Sumbawanga ambaye CCM iliamua kumtosa tu kama walivyofanya kwa marehemu Kitwana Kondo.
 
Hoja yangu ni kwamba hayo mambo uliyoyataja ni masuala ya Muungano, yanahudimiwa kutokana na mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa gavana wa BoT marehemu Ndulu , Zanzibar haichangii katika muungano.
Kwa taarifa za TRA pesa hubaki Zanzibar, kama zinaletwa Dar twambie ni kiasi gani.

Zanzibar hawana mchango katika muungano nani analipia gharama za muungano zikiwemo Wizara na Taasisi? Jibu ni rahisi, Tanganyika ndiyo inagharamia Muungano

Tanganyika imebaki JMT kwasababu Zanzibar ina kila kitu chake.
Zanzibar kuitumia JMT katika mafao tu, kuwajibika hawapo

Hiki ndicho kiini cha kuhoji, mikopo inalipwaje? Zanzibar wakichukua bilini 280 wanarudisha kwa utaratibu gani? Hakuna formula, deni ni la JMT ambalo ni Tanganyika, na inalipa

SMZ ilishindwa kulipa Tanesco Bilioni 60! Matokeo yake deni hilo likarudishwa kwa Wananchi wa Tanganyika na bila kujali ni CCM, Chadema,ACT au TLP wamelipa

Hakuna Wilaya , Tarafa, kata au kijiji cha Tanganyika kinacholipiwa umeme na JMT, iweje nchi ya Zanzibar ikiwa na kila kitu ilipiwe umeme !
 
Pia ule mradi wa maji victoria kuleta shy tabora dodoma,
Shida watu wa bara tuna roho za kwanini sana,,, yaani hatuna ustaarabu kabisa wala hikima, tumekaa kaa kama watindiga fulani,,,
Wakati tunavuta maji toka lake victoria , wazanzibar hawakulalamika,,, wao pia wanalipa kodi,
Hujaelewa point inayozungumziwa. Tatizo si kupelekewa maji au kupata mikopo!
Huo mradi wa Dodoma gharama zote wanabeba Watanganyika kupitia Hazina na BoT

Tunachouliza hapa ni kuwa Zanzibar itarudisha mkopo au deni hilo kwa utaratibu gani?
Hatujawahi kuambiwa Zanzibar inalipaje madeni kutokana na mikopo, tunaambiwa wanagawiwa kitu gani.

Pili, Wazanzibar wakiongozwa na AG wakati huo Othman Maosud walifanya mambo haya
1. Kuondoa mafuta na gesi kutoka mambo ya muungano bila majadiliano
Maana yake ni kuwa hawakutaka kuchangia kama sehemu ya muungano

2. Wakataka wakope bila kupitia JMT kwa maana ya deni watalipa wao kwa mafuta na gesi.

Hoja zinazofuata ni hizi, ikiwa hawataki 'chao' kiingie mfuko wa pamoja na ikiwa walitaka kukopa wenyewe, ni kitu gani kinawasukuma kukubali na kupewa deni kupitia JMT ?

Ni utaratibu gani utakaotumika kuhakikisha wanarudisha deni hilo bila kumtwisha Mtanganyika gharama kama ilivyo kawaida?

3. Kuna watu wanahoji kuwa ikiwa hilo ni deni la ''JMT'' ambalo ni la Tanganyika iweje eneo dogo na watu chini ya milioni 1 wapewe kiasi hicho ikijulikana hawachangii muungano ?

4. Mikopo na Madeni ni malalamiko ya Wazanzibar kwa maana ya kero na hili lilikuwa miongoni mwa kero 11. Mbona kero hizo zimetatuliwa kimya kimya ? Nini kiliamuliwa kuhusu misaada, mikopo na madeni?

Rasimu ya Warioba iliweka wazi mambo 7 ya muungano. Ikitamka kurejeshwa kwa Tanganyika ili ikae meza moja na Zanzibar katika hali kama iliyopo. Hiyo ndiyo njia sahihi na wala si kuwalaumu unaowaita Wabara! ni Watanganyika kwasababu Wazanzibar hawataki kuwa wa visiwani
 
Siasa za kijinga zitatuponza!! Zenji sasa inapaa kajimkoa kanajazwa mihela alafu ulipaji unakuwa wetu.
Bara kilaleo watu wanajiua au kuuana hovyo kutokana na kukata tamaa kwa ugumu wa maisha lkn znji mambo nswano na tuna mavi ongozi kaziyao kusifu tuu miradi wao wanalipwa mamishahara na marupurupu makubwa.
 
Wizara nzima ya fedha wanashindwa kushauri ugawaji ambao hauwi tishio kwa Muungano wetu kwa tamaa zao za vyeo.
Mgawo wa namna hiyo ni tishio. Population iwe kwenye factor yao ya ugawaji. Equation utengenezwe ambayo utaifa utakuwa na factor yake, population factor yake na factors zingine zingine.
Hatuwezi kuiumiza Tanganyika kwa kuifurahisha Zanzibar.
Ni ujinga kutoweka population katika factors za ugawaji wa fedha.
Ni upendeleo wa kijinga kama ule ule tuliokuwa tunaupinga juu ya Chato.
 
Kwa mujibu wa gavana wa BoT marehemu Ndulu , Zanzibar haichangii katika muungano.
Kwa taarifa za TRA pesa hubaki Zanzibar, kama zinaletwa Dar twambie ni kiasi gani.

Zanzibar hawana mchango katika muungano nani analipia gharama za muungano zikiwemo Wizara na Taasisi? Jibu ni rahisi, Tanganyika ndiyo inagharamia Muungano

Tanganyika imebaki JMT kwasababu Zanzibar ina kila kitu chake.
Zanzibar kuitumia JMT katika mafao tu, kuwajibika hawapo

Hiki ndicho kiini cha kuhoji, mikopo inalipwaje? Zanzibar wakichukua bilini 280 wanarudisha kwa utaratibu gani? Hakuna formula, deni ni la JMT ambalo ni Tanganyika, na inalipa

SMZ ilishindwa kulipa Tanesco Bilioni 60! Matokeo yake deni hilo likarudishwa kwa Wananchi wa Tanganyika na bila kujali ni CCM, Chadema,ACT au TLP wamelipa

Hakuna Wilaya , Tarafa, kata au kijiji cha Tanganyika kinacholipiwa umeme na JMT, iweje nchi ya Zanzibar ikiwa na kila kitu ilipiwe umeme !
Deni la TANESCO walisamehewa kwa kushindwa kulipa sijui haya mengine itakuwaje..
TOZO za bara na kodi ndio zitalipa deni huu muungano kizungumkuti.
Akitoka saa 100 wazee wa uamsho walianzishe tena kudai Zenji yenye mamlaka kamili.
 
Mama anasema mara kwa mara kwamba kuna nchi moja tu duniani inayoitwa Tanzania. Kama namuelewa vyema, anajaribu kunyamazisha watu juu ya utanganyika na uzanzibar. Lakini sasa kwanini kwenye mgawo wa fedha wanachotewa nzima nzima? Kwanini uhitaji haungaliwi kama ambayo uhitaji unaangaliwa pia kwa maeneo mengine hapa bara? Sisi Tanzania hatugawani rasilimali kwa kuangalia maeneo yetu ya kijiografia. Tunagawana rasilimali kulingana na uhitaji. Ndio maana mgawo wa fedha za Covid kwa mikoa yetu, haikuangalia ukubwa wa mkoa au idadi ya watu wala uchangiaji kodi. Umeangalia uhitaji.
Sasa hii staili ya ugawaji inatoka wapi na inatupeleka wapi?
Je, sio operation ya siri ya kutikisa Muungano?
 
Tanganyika hatukujifunza juu ya kuvunjika kwa EAC ya awali na Kenya kuhodhi mali nyingi za EAC hiyo.
Labda Zanzibar watatufundisha siku watakayo bwaga manyanga na kutuachia madeni lukuki.
 
Haya ndo mambo ambayo Hangaya kayafanyia kazi! a.k.a kero za muungano yaani Tanzania bara inapata billion 540 na zanzibar wanapata karibia billion 220 huu ni upuuzi wa hali ya juu! Watanganyika mnachekelea tu!
Unataka watanganyika wafanyaje .?
 
Zanzibar haifiki hata nusu wa wakazi wa dar

Huu muungano wa kinyonyaji

Watanganyika tudai nchi yetu

Ishakuwa too much sasa
 
Back
Top Bottom