Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,204
42,063
Serikali ya Japan imeipatia Tanzania mkopo wa shillingi billion 761.8 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo nchini!

Katika mkopo huo kisiwa cha Zanziba kimepewa mgao wa Tsh billion 218+

Kazi iendelee...

=====

Screenshot_20220205-033912_Firefox.jpg


Serikali ya Tanzania na Japan zimesaini mikataba mitatu ya mkopo na msaada yenye thamani ya Yen za Japan bilioni 37.9 sawa na takriban shilingi bilioni 761.8 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ukarabati wa Bandari ya Kigoma, uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na Ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili.

Mikataba hiyo imesainiwa jijini Dar es Salaam, kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan, Bw. Naofumi Yamamura, kwa naiaba ya Serikali ya Japan.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mikataba hiyo, Bw. Tutuba alisema kuwa Mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma utatekelezwa kwa msaada wa Yen za Japan bilioni 2.73 sawa na takriban shilingi bilioni 54.79, ukihusisha Ukarabati wa gati za mashariki na kaskazini mwa Bandari ya Kigoma, ukarabati wa majengo ya kushushia abiria na mizigo, ukarabati wa barabara zilizopo katika Bandari hiyo na ujenzi wa majengo mapya ya abiria na mizigo.

“Bandari ya Kigoma ilijengwa katika kipindi cha mwaka 1912–1927 na imekuwa bandari muhimu katika kusafirisha mizigo na abiria kwenda nchi jirani za Burundi, DR Congo, Zambia na mikoa iliyopakana na Kigoma, hivyo kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo kutachangia kuongeza ufanisi wa Bandari, kutoa fursa za ajira, kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kuchochea shughuli za kiuchumi na kuchochea biashara kati ya Tanzania na nchi hizo jirani” alisema Bw. Tutuba

Alisema kuwa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji Zanzibar, utatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Yen za Japan bilioni 10.86 sawa na takriban shilingi bilioni 218.382 ambapo mradi huo utahusisha kujenga na kukarabati miundombinu ya maji Mjini Zanzibar.
 
Serikali ya Japan imeipatia Tanzania mkopo wa shillingi billion 761.8 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo nchini!

Katika mkopo huo kisiwa cha Zanziba kimepewa mgao wa Tsh billion 218+


Kazi iendelee....View attachment 2107913
View attachment 2107914
Haya ndo mambo ambayo Hangaya kayafanyia kazi! a.k.a kero za muungano yaani Tanzania bara inapata billion 540 na zanzibar wanapata karibia billion 220 huu ni upuuzi wa hali ya juu! Watanganyika mnachekelea tu!
 
Back
Top Bottom