Japan: Shirika la Reli laomba radhi treni kuondoka sekunde 20 mapema

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Shirika moja la reli Japan limeomba radhi baada ya moja ya treni zake kuondoka sekunde 20 mapema.

Wasimamizi wa shirika la treni za reli ya Tsukuba Express kutoka Tokyo hadi Tsukuba wanasema wameomba radhi sana kwa usumbufu ambao huenda waliwasababishia wasafiri.

Kupitia taarifa, shirika hilo limesema treni hiyo ilikuwa imepangiwa kuondoka saa 9.44.40 (Saa tatu na dakika arobaini na nne na sekunde arobaini na nne) lakini iliondoka saa 9.44.20.

Wengi wa watu mitandaoni, hasa kutoka mataifa mengine wameshangazwa sana na hatua ya shirika hilo.

Shirika hilo limesema kosa hilo lilitokana na hatua ya wafanyakazi wake kutoangalia vyema ratiba ya treni kabla ya kuondoka.

Wameongeza kwamba hakuna mteja yeyote aliyelalamika kutokana na hatua ya treni hiyo kuondoka mapema kutoka kituo cha Minami Nagareyama kaskazini mwa Tokyo.

Tsukuba Express huwasafirisha abiria kutoka Akihabara mashariki mwa Tokyo hadi Tsukuba kwa dakika 45.

Ni nadra sana kwa treni Japan, nchi iliyo ya mfumo wa treni wa kuaminika sana duniani, kuondoka wakati ambao haipangiwi kuondoka.

Reli ya Tokkaido, inayotoka Tokyo hadi Kobe, husafirisha watu karibu 150 milioni kila mwaka.

BBC Swahili
 
Tuna la kujifunza hapa katika hili???

Shirika laomba radhi treni kuondoka sekunde 20 mapema

Screenshot_20171116-212205.png
 
Uku kwetu Bonbadier inamsubiria kigogo wa serikali kwa zaidi ya dakika 40 bila ya kujali kama abiria wengine wanachelewa.
 
sweden treni ikichelewa unachukua taxi, shirika linakulipa pesa yako ya taxi
kwa sababu niusumbufu wao na pia umeme ukikatika muda wa masaa mawili shirika linalipa kila mtu kwa ajili cha chakula kwenye fridge
 
Tsukuba Train express ni kampuni inayotoa ya huduma ya usafiri katika jiji la Tokyo nchini Japan.
Siku chache zilizopita treni yake iliwahi kuondoka katika kituo cha Minami- Nagareyama ,ilitakiwa kuondoka saa 9:40:40 lakini yenyewe ikawahai kuondoka kwa sekunde 20 kabla yaani 9:40:20.
Uongozi wa kampuni hiyo uliomba radhi kwa tukio hilo la kuwahi kuondoka kwa sekunde 20.
Funzo tunalolipata hapa hapo ji UWAJIBIKAJI uliopo katika nchi za wenzetu.
Ni utamaduni uliojengeka vizazi kwa vizazi hawasubiri wawajibishwe bali wanajiwabisha wenyewe.

Hali hii ndio naiona katika fikra za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr.John Pombe Magufuli.
Anahimiza kila mtu au taasisi ya Serikali iwajibike pale ilipo.Wajue majukumu yao na wayafanye kwa weledi wa hali ya juu.

Kama ni taasisi iliyopewa dhamana ya kuwapa wananchi nishati basi ihakikishe inatimiza majukumu hayo kwa ufanisi wa hali ya juu , kama ni taasis yenye dhamana ya kutoa maji kwa wananchi nao halikadhalika .

Nchi za dunia ya kwanza zimepiga hatua kubwa kimaendeleo kutokana na mambo makubwa mawili,UWAJIBIKAJI na kujali MUDA.

Uwajibikaji ukiwepo ,basi uzembe na uvivu katika ofisi za Serikali hautakua na nafasi.
Zile tabia za mtu anaripoti Ofisini halafu ndio anaenda kunywa chai ni mojawapo ya tabia isiyo na tija katika kutimiza malengo na kuleta ufanisi Serikalini.

Utamaduni wa kujituma unatakiwa uingie katika nyoyo za watanzania wote.
Kila mtu atimize wajibu wake pale alipoaminiwa na kupewa dhamana tena kwa uadilifu na uaminifu mkubwa kw Tanzania ya kesho tuitakayo yenye ustawi .

Wasalaam,
Augustino Chiwinga

0756810804
 
Alikuwa Binti ambae sasa anavaa tenite na anatemea mate kwa pembeni.....utamuachaje mzazi mwenzake na mfalme?? Hujui hizo bomba dear ni zao? Wamenunua kwa pesa zao.....bomba dear ni suala la familia....maana aliezichota ni mpwa akampa uncle akalipa cash.... chao kikaletwa kwa nyuma na sasa zinazungushwa nchini!! Mtasubiri tu hata masaa 3 mnaenda wapi nyie wa Tanzania wapiga deal??
 
Huku kwetu ni faidi kuondoka mapema pesa hairudishwi kwa mtu aliyechelewa.
 
Hakuna siku inayopita pale JNIA bila Bombardier kutoa taarifa (sio kuomba radhi) kwamba itachelewa kuondoka (au kuwasili) hivyo abiria watulie; haielezwi itachelewa kwa muda gani.
 
Tsukuba Train express ni kampuni inayotoa ya huduma ya usafiri katika jiji la Tokyo nchini Japan.
Siku chache zilizopita treni yake iliwahi kuondoka katika kituo cha Minami- Nagareyama ,ilitakiwa kuondoka saa 9:40:40 lakini yenyewe ikawahai kuondoka kwa sekunde 20 kabla yaani 9:40:20.
Uongozi wa kampuni hiyo uliomba radhi kwa tukio hilo la kuwahi kuondoka kwa sekunde 20.
Funzo tunalolipata hapa hapo ji UWAJIBIKAJI uliopo katika nchi za wenzetu.
Ni utamaduni uliojengeka vizazi kwa vizazi hawasubiri wawajibishwe bali wanajiwabisha wenyewe.

Hali hii ndio naiona katika fikra za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr.John Pombe Magufuli.
Anahimiza kila mtu au taasisi ya Serikali iwajibike pale ilipo.Wajue majukumu yao na wayafanye kwa weledi wa hali ya juu.

Kama ni taasisi iliyopewa dhamana ya kuwapa wananchi nishati basi ihakikishe inatimiza majukumu hayo kwa ufanisi wa hali ya juu , kama ni taasis yenye dhamana ya kutoa maji kwa wananchi nao halikadhalika .

Nchi za dunia ya kwanza zimepiga hatua kubwa kimaendeleo kutokana na mambo makubwa mawili,UWAJIBIKAJI na kujali MUDA.

Uwajibikaji ukiwepo ,basi uzembe na uvivu katika ofisi za Serikali hautakua na nafasi.
Zile tabia za mtu anaripoti Ofisini halafu ndio anaenda kunywa chai ni mojawapo ya tabia isiyo na tija katika kutimiza malengo na kuleta ufanisi Serikalini.

Utamaduni wa kujituma unatakiwa uingie katika nyoyo za watanzania wote.
Kila mtu atimize wajibu wake pale alipoaminiwa na kupewa dhamana tena kwa uadilifu na uaminifu mkubwa kw Tanzania ya kesho tuitakayo yenye ustawi .

Wasalaam,
Augustino Chiwinga

0756810804
Na aanze kujiwajibisha yeye Kwa maovu aloyatenda tutakua kweli anataka watu wawe waadilifu
 
sweden treni ikichelewa unachukua taxi, shirika linakulipa pesa yako ya taxi
kwa sababu niusumbufu wao na pia umeme ukikatika muda wa masaa mawili shirika linalipa kila mtu kwa ajili cha chakula kwenye fridge
Aiseee
 
Tsukuba Train express ni kampuni inayotoa ya huduma ya usafiri katika jiji la Tokyo nchini Japan.
Siku chache zilizopita treni yake iliwahi kuondoka katika kituo cha Minami- Nagareyama ,ilitakiwa kuondoka saa 9:40:40 lakini yenyewe ikawahai kuondoka kwa sekunde 20 kabla yaani 9:40:20.
Uongozi wa kampuni hiyo uliomba radhi kwa tukio hilo la kuwahi kuondoka kwa sekunde 20.
Funzo tunalolipata hapa hapo ji UWAJIBIKAJI uliopo katika nchi za wenzetu.
Ni utamaduni uliojengeka vizazi kwa vizazi hawasubiri wawajibishwe bali wanajiwabisha wenyewe.

Hali hii ndio naiona katika fikra za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr.John Pombe Magufuli.
Anahimiza kila mtu au taasisi ya Serikali iwajibike pale ilipo.Wajue majukumu yao na wayafanye kwa weledi wa hali ya juu.

Kama ni taasisi iliyopewa dhamana ya kuwapa wananchi nishati basi ihakikishe inatimiza majukumu hayo kwa ufanisi wa hali ya juu , kama ni taasis yenye dhamana ya kutoa maji kwa wananchi nao halikadhalika .

Nchi za dunia ya kwanza zimepiga hatua kubwa kimaendeleo kutokana na mambo makubwa mawili,UWAJIBIKAJI na kujali MUDA.

Uwajibikaji ukiwepo ,basi uzembe na uvivu katika ofisi za Serikali hautakua na nafasi.
Zile tabia za mtu anaripoti Ofisini halafu ndio anaenda kunywa chai ni mojawapo ya tabia isiyo na tija katika kutimiza malengo na kuleta ufanisi Serikalini.

Utamaduni wa kujituma unatakiwa uingie katika nyoyo za watanzania wote.
Kila mtu atimize wajibu wake pale alipoaminiwa na kupewa dhamana tena kwa uadilifu na uaminifu mkubwa kw Tanzania ya kesho tuitakayo yenye ustawi .

Wasalaam,
Augustino Chiwinga

0756810804
Nakuhurumia tu kwa matusi utakayoyapata.

Tatizo si kwa fikra hizi za mtanzania anayeamini katika siasa kuliko uwajibikaji na utendaji.

Ikumbukwe asilimia tisini ya wafanya kazi wa tanzania hufanta kazi ambazo hazikuwa ndoto yao, wao wameenda huko kulingana na sababu moja ama nyingine. Ki ukweli wengi huishia kufanya kazi kwa hasira huku mioyo yao ikitamani kazi ile.

Kitu cha pili
Tunarudi nyuma kiuchumi kwa sababu asilimia tisini ya vijana wamewekeza maisha yao kwenye siasa hususani wasomi ambao wamegeuza siasa kama suruhisho la matatizo ya maisha yao na si kuitegemea taaluma zao,
Matokeo yake hushitukia wakiombea taifa mambo mabaya na furaha yao kupatikana kutokana na changamoto za Taifa letu
 
Back
Top Bottom