“Japan Bible Institute Graduate School of Theology” ni feki JIHADHARINI ----- TCU YANENA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

“Japan Bible Institute Graduate School of Theology” ni feki JIHADHARINI ----- TCU YANENA

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MKL, Mar 6, 2012.

 1. MKL

  MKL Senior Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imepokea taarifa kupitia matangazo yanayotolewa na chuo kinachojiita “Japan Bible Institute Graduate School of Theology” kikijitangaza kwamba kinatoa shahada mbalimbali za uzamivu (PhD) kwenye nyanja za dini na jamii. Chuo hiki kinajitangaza kwamba kinawakilisha tawi la taasisi iliyopo nchini Marekani na kwamba makao yake makuu kwa bara la Afrika yapo Dar es Salaam, pamoja na kwamba eneo halisi ofisi zao zilipo haijaelezwa kwenye matangazo yao.
  Tume inachukua fursa hii kuuarifu umma kwamba chuo hiki hakitambuliki kwa mujibu wa sheria na kwamba wamiliki wa Japan Bible Institute Graduate School of Theology hawana kibali cha kutoa elimu ya chuo kikuu ambayo inatambuliwa hapa nchini. Tume inatoa tahadhari kwa umma kuepuka ulaghai ambao unafanywa na watu katika eneo hili la elimu ya juu na hivyo umma unashauriwa kuchukua tahadhari kwani vyeti watakavyotolewa havitambuliwi na Tume na hivyo haviwezi kutumika hapa nchini.Pia, wamiliki wa chuo hiki na wawakilishi wake waliopo Tanzania wanapewa onyo kuacha mara moja kutoa matangazo ya shahada za aina hiyo hapa nchini bila kufuata taratibu. Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakaye kwenda kinyume na tangazo hili.Aidha, Tume inapenda kuwaarifu watu wote wenye lengo la kuanzisha vyuo vikuu nchini au kutoa programu za vyuo vikuu wawasiliane na Tume ili kupata maelekezo juu ya taratibu zinazotakiwa kufuatwa. Pia umma unasahauriwa kutoa taarifa kwa Tume ama vyombo vingine vya dola pale ambapo wana wasiwasi na uhali wa programu ama tuzo inayotangazwa au kutolewa na taasisi yoyote bila kufuata taratibu.Imetolewa na:
  Katibu Mtendaji
  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
  S.L.P. 6562
  DAR ES SALAAM
   
 2. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="width: 100%"] Hivi ndivyo eti wanasema juu ya PhD zao za heshima; soma hapa: ( Japan Bible Institute - Free Bible Course - Free Christian Online Ordination -Accredited Courses - Bible College - Clergy Ordination - Ministry materials - End time Pible Prochey - Life Experience Degrees - Japan Wedding Misitry Training):


  HONORARY DOCTORIAL DEGREE PROGRAM

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 100%"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 100%"] If you are a Pastor, Evangelist, or Leader of an active Christian ministry, The Japan Bible Institute may be able to grant you an Honorary Doctorial Degree on the basis of I Timothy 5:17, if you meet the following qualifications:

  • Must be at least 30 years old.
  • Produce evidence that you are a licensed and ordained minister of the Gospel.
  • Verify that you have at least 10 years of full-time or part-time ministerial experience.
  • Prepare a TYPED one-page summary or resume of your work for the Lord.
  • Secure the endorsements of two other licensed or ordained ministers or other prominent Church leaders.
  • Make a $275 contribution to the furtherance of The Japan Bible Institute.
  • There is a discount for two Honorary Doctorial Degrees for a Married Couple.
  You may request an application by Postal Mail or E-Mail attachment.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 100%"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 100%"]
  USE OF YOUR TITLE
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 100%"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 100%"] Only about 5% of ministers in major cities have Doctor Degrees---but it’s rapidly increasing.
   
  If you receive a Doctorate from The Japan Bible Institute, you have a legitimate right to use the title in your public life either before or after your name, such as: Dr. Joe Smith, Joe Smith, DTh., or Rev. Dr. Joe Smith. You are honestly and ethically entitled to use your title on your business cards, letterhead, brochures, the phone book, road signs, and “Public Service Announcements” in the newspapers, if you so choose.
   
  It’s only reasonable and proper for others to address and introduce you as “Doctor so and so...” Your degree will often win you instant respect from most dignified people. It means you have spent hundreds of hours studying hundreds of Bible verses and answering hundreds of questions correctly!


  ******************************
  Hakika hii staili ya kununua PhD kwenye mitandao ndio utapeli na upumba..wa mwisho. Kama wewe ni mtu wa maadili huwezi kamwe kuhudhudhuria wala kutetea shahada za kipumbavu za hivyo eti zikitolewa kesho hapa Dar. Ukitaka heshima ya kisomi, soma hakuna short cuts!!

  Hivi hakuna vyama vya Maprofesa na Wasomi nao waandamane, wakigoma na kushinikiza serikali kuwanyofoa wote wenye digrii feki na kufutilia mbali kabisa vyuo vya mitandaoni (visivyo) na accreditation kama hivi?

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 5,773
  Likes Received: 3,246
  Trophy Points: 280
  Waandamane wapi wakati hizo doctorate hazihusiki na mambo secular? Waachane wafu wazikane wenyewe!
   
Loading...