January, Zitto live TBC1 wakizungumzia hoja binafsi

Mh Zitto Kabwe amewadanganya vijana wa kitanzania,baada ya kuwaahidi kuwa atapeleka bungeni hoja binafsi kuhusu tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekuwa ni disaster kwa sasa..badala yake amesikika akipeleka hoja binafsi ya mambo ya kilimo cha mkonge na kupuuzia ile hoja ya ajira kwa vijana aliyowahaidi kupitia chombo kimoja cha redio hapa Tanzania..

Namuomba Zitto na wanasiasa wengine vijana msiwatumie vijana wenzenu kwa maslahi yenu binafsi,kama mmeshindwa kuwapigania basi waacheni waendelee ku-hustle kimpango wao msijifanye mnaumizwa sana na matatizo yao ikifika suala la kuwawakilisha inakuwa usanii mtupu..vijana ni waelevu wanausoma tu mchezo.
Fikiria nje ya box Mkuu, utabaini kuwa hiyo hoja inalenga kuongeza ajira
 
Akili yako ni utumbo kweli, hakuna kitu ambacho kitaongeza ajira kwa watanzania kama kufufua zao la mkonge, strategy aliyoitumia zitto na mahususi kabisa ikilenga eneo la uzalishaji wa mkonge ambao utatoa ajira za kutosha mashambani, viwandani na katika sekta ya nishati kupitia mkonge. Ameleta hoja ya kuinua ajira kimkakati zaidi badala ya kuwa kama lowassa unalalamika kuwa ajira kwa vijana ni bomu lakini husemi tuanawezaje kutengeneza ajira mpya.
pole ndugu yangu kupoteza muda wako. we ushaskia mtu anajiita matumbo, unadhani anawaza nini zaidi ya kuletewa chakula bure.
 
misifaz jazz band..........

jamani tuache ushabiki usiona sababu.hivi kweli kwa mtu mzalendo watu wanajadili vitu mhimu kama vile unawaita misifaz jazz band kweli? Hivi wewe hapo ulipo hujapanga nyumba, fikiri kidogo tu namna madalali wanavotusumbua mtaani. kwa nini mtu kama makamba aje na hoja ya namna ya kurasimisha mfumo wa upangaji nyumba umdhihaki kiasi hicho, tafadhali watake radhi waheshiwa na wanajf kwa ujumla.

Hizi mi hoja mhimu kwa sasa kwa sababu mijadala yote sasa hata ndani ya bunge imekuwa sio namna ya kuzalisha na kukuza uchumi badala yake tumekuwa na mijadala isiyokuwa na tija mfano mijadala ya chinichini ya nani anapigania nafasi ya uraisi 2015.

Kwa waheshimiwa kuja na hoja za uzalishaji na kukuza uchumi ni jambo la kujivunia, tuwatie moyo vijana ili waendelee kuangalia mianya ya kukuza uchumi wetu na kuisemea ili serikali iamke.Nafarijika namna wabunge hawa vijana wanavyotoa takwimu mfano mh.Makamba anasema asilimia sitini ya wakazi wa mjini wamepanga na vipato vya wakazi hawa asilimia arobaini wanatumia kwa kulipa pango, taarifa hizi kazitoa chama cha wapangaji.Kwa mtazamo huu wakazi asilimia sitin ni uchumi wa taifa huu kwa maana ya nguvu kazi na vitu vingine kama watu hawa hawaishi kwa amani hawawezi kuzalisha vya kutosha

kwa upande wa Mh.zitto hoja yake pia ni ya msingi.Kilimo cha katani hakika kiliinemesha Tanga yetu, angalia sasa Tanga ilivo, uchumi wake unategemea nini sana.bandari haiko bize sana kama wakati huo, ansema namna katani inavoweza kupandisha thamani ya madafu yetu ambayo kila kukicha inaporomoka. na namna ya pekee ya kuipandisha shilingi yetu ni kuongeza mauzo nje ya nchi, sasa ukiangalia haraka haraka sasi kama tanzania share yetu kwenye soko la dunia tuuze nini ili tupate ulali mzuri wa biashara, unaweza kutumia kufikiria usipate jibu la haraka haraka kama wewe uchumi wa tz huujui.Ukiachilia mbali madini tuliyonayo ambayo yangetubeba sana na ambayo serikali inajifanya haioni kitu moja wapo ni zao hili la katani.Kama takwimu za mh.zitto ni sahihi tunaweza kuwa leading country kwa kuzalisha na kuuza nje zao hili na hatimaye uchumi wetu ukaimarika.

Kimsingi, kama nchi sasa tuache siasa na tufanye kazi.narudia tena Mkurungezi mkuu wa taasisi iliyoko Austaralia iitwayo LIW anasema kwenye kitabu chake kiitwacho KEEP CALM AND CARRY ON LEADING akikalibisha mwaka 2012 anasema viongozi wakiafrica wafanye vitu vitatu tu navyo ni BETTER THINKING,CUSTOMER FOCUS NA EXCUTION.

Kwa kumalizia, jukwaa hili liendelee kuwa chachu ya hoja za nguvu na sio kukejeliana na kukandamizana, mwenye mawazo mazuri tumpe credit na mwenye mawazo potofu tumfundishe na aelewe kama anafundishika.

Thankx
 
Them belly full, but we hungry;
A hungry mob is a angry mob.
A rain a-fall, but the dirt it tough;
A yot a-yook, but d' yood no 'nough.
 
Akili yako ni utumbo kweli, hakuna kitu ambacho kitaongeza ajira kwa watanzania kama kufufua zao la mkonge, strategy aliyoitumia zitto na mahususi kabisa ikilenga eneo la uzalishaji wa mkonge ambao utatoa ajira za kutosha mashambani, viwandani na katika sekta ya nishati kupitia mkonge. Ameleta hoja ya kuinua ajira kimkakati zaidi badala ya kuwa kama lowassa unalalamika kuwa ajira kwa vijana ni bomu lakini husemi tuanawezaje kutengeneza ajira mpya.

usinitusi mkuu,hapa tunajadiliana tu tena unajadiliana na mtu muungwana sana,alafu ishu za Lowassa zinaingiaje hapa mkuu?usichukulie kila hoja kichamachama..
Back to the topic,usichukulie tatizo la vijana kiivyo hapa unazungumzia robo tatu ya population ya Tanzania ambao ni vijana,kwa akili yako isiyo utumbo unafikiri kufufua zao la mkonge ndio suluisho pekee la ajira kwa vijana kwa sasa?
 
Kwani mkonge ukifufuliwa, ajira kiasi gani zitapatikana? Sio lazima apige kelele kusema ajira bila kuonesha ni vpi zitapatikana. Kama hoja hiyo itajadiliwa vizuri, hata reli inaweza kufufuka, hivyo ajira zitakuwa katika nafasi zifuatazo
1. Wafanyakazi wa reli
2. Wafanyakazi mashambani-wengi zaidi
3. Wafanyakazi viwandani
4. Wauza vyakula nao watauza, mashambani, reli, na viwandani. Tayari atakuwa amefanikisha kuwapatia watanzania/vijana ajira. Hajadanganya mkuu

naposema amedanganya namaanisha mkuu.
Pamoja na yote nimekusoma,ila kumbuka unapoongelea vijana uelewe unazungumzia population kubwa inayojenga Tz,cha kusikitisha hii number kubwa imebaki kama watazamaji kwenye ujenzi wa taifa lao.
 
Ni uelewa finyu tuu,Lakini hajadanganya mkuu

usiwe na shaka kuhusu uelewa wangu,ungebahatika ata kuukalibia ungenielewa au ungeuliza usipoelewa..
Zito alisema na kuhaidi atapeleka hoja binafsi juu ya tatizo la ajira kwa vijana na akasema ataomba lishughulikiwe kama ishu ya dharura,leo anakuja na maswala ya mkonge...hapo ajadanganya?
 
misifaz jazz band..........

huu ni upumbavu ulioandika hapa, sitegemei mtu na akili zako ukawa unaleta kejeli kama hizi naomba wakati mwingine uwe unanyamza kimya usipende kupandisha hasira za watu na kuwasababishia BAN zisizo na msingi kuna majukwaa ya mzaha kama CHIT CHAT na UDAKU... unaweza ukapeleka ujinga wako kule
 
Ulitaka afikishe hoja kwa style ipi? Kuomba wote waajiriwe serikalini?

jifunze kuufikirisha ubongo wako hapa hatuko chit-chat..ila acha nikueleweshe.

Sikutaka aombe vijana wote waajiriwe serikalini..nilitaka atimize ahadi yake ya kupeleka hoja binafsi kuhusu ajira kwa vijana tena aliahidi ataomba lishughulikiwe kama jambo la dharura,leo mnaomjibia mnasema ooh ameli-link na kufufua zao la mkonge mbona konekshen ipo kwa mbali ukitizama vijana kwa population yake..
Kingine bibiye tunapozungumzia ajira kwa vijana hatuzungumzii sekta rasmi au za serikali pekee hapa tunagusa ata sekta zisizo rasmi,ambazo nazo zinashindwa kuajiri vijana kwa sasa kwa sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wa vijana.
 
Mh Zitto Kabwe amewadanganya vijana wa kitanzania,baada ya kuwaahidi kuwa atapeleka bungeni hoja binafsi kuhusu tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekuwa ni disaster kwa sasa..badala yake amesikika akipeleka hoja binafsi ya mambo ya kilimo cha mkonge na kupuuzia ile hoja ya ajira kwa vijana aliyowahaidi kupitia chombo kimoja cha redio hapa Tanzania..

Namuomba Zitto na wanasiasa wengine vijana msiwatumie vijana wenzenu kwa maslahi yenu binafsi,kama mmeshindwa kuwapigania basi waacheni waendelee ku-hustle kimpango wao msijifanye mnaumizwa sana na matatizo yao ikifika suala la kuwawakilisha inakuwa usanii mtupu..vijana ni waelevu wanausoma tu mchezo.
Bwn Matumbo vipi kwani kilimo cha mkonge si ni ajira hiyo, creation of labor for the youth si anajaribu kila option???????
 
Bwn Matumbo vipi kwani kilimo cha mkonge si ni ajira hiyo, creation of labor for the youth si anajaribu kila option???????

angesema basi wakati anajibu maswali ya watu redioni kwamba atalioanisha na kufufua zao la mkonge,sio kama alivyoliweka...

Na mimi nafikiri tatizo la ajira ni kubwa zaidi ya hoja ya kufufua zao la mkonge kuibeba.we unafikiri kufufua zao la mkonge uko Tanga na Morogoro ndio suluisho pekee la kumaliza tatizo la ajira kwa vijana??
 
tuuze jengo la bunge tuwalipe madakatari na walimu, hivi wabunge wanatusaidia nini hasa? wawepo wasiwepo yote sawa, SIASA ZA TANZANIA NI BIASHARA, hivi mbona wenzetu KENYA wanatushinda kwa kuwa na misingi imara ya uelewa wa kidemokrasia na elimu ya uraia, WATANZANIA TUMELAANIWA
Mkuu PhD katiba mpya ndio mambo yote, miundo ya utawala, miundo ya mishahara, marupurupu na posho, utawala bora, mikataba ya madini, umiliki wa aridhi yetu,ngawanyo wa mali zetu, yote hayo yatakuwa kwenye katiba mpya sio ubabaishaji!!!!!!!!!!! Tupambane kupata katiba mpya period!!!!!!!!!!

angesema basi wakati anajibu maswali ya watu redioni kwamba atalioanisha na kufufua zao la mkonge,sio kama alivyoliweka...

Na mimi nafikiri tatizo la ajira ni kubwa zaidi ya hoja ya kufufua zao la mkonge kuibeba.we unafikiri kufufua zao la mkonge uko Tanga na Morogoro ndio suluisho pekee la kumaliza tatizo la ajira kwa vijana??
At least to a certain extent, ukifanya research zao la mkonge lilitoa ajira kubwa kwetu hapa Tanganyika enzi hizo, the second exporter of sisal in the world was Tanganyika apart from Brazil!!

Zitto Kabwe na January Makamba njooni Kariakoo Mtaa wa Aggrey na Likoma muone vijana wenzenu wanavyoteseka na KODI kubwa, kachumba kiduchu million tano na wanataka kodi ya mwaka, vijana wanakopa leo kehso wanakosa marejesho. Wenye Nyumba wengi wanaibia TRA na Ardhi kwa Mikataba feki. Majengo mengi mikataba inasema robo ya kitu kizima, mfano:- Dalali anatafuta chumba cha biashara kwa shilling laki nne kwa mwezi, dalali anapewa sh. laki nne kwa kuongea tu alafu wewe unatoa tena laki nne x 12 yaani kwa mwaka, lakini mwenye nyumba anakuandikia kodi ya mwaka laki (nane)800,000.00 ili kukwepa kodi ya TRA alafu katika laki nane anakuambia ukalipe TRA W/Tax ya laki nane. Wengi wa vijana wemebaki kuuza simu mikononi au kutembea na nguo mbili. Njooni tuwape orodha ya Madalali na wenye nyumba matapeli. Yaani ni wizi mtupu naweza hata kutoa nyumba ploti no. mikataba yao feki.
 
Back
Top Bottom